Friday, March 29, 2013

picha kumi za video mpya ya wizkid "lagos to soweto

cheki picha za utengenezaji wa video mpya( behind the scenes) wizkid "lagos to soweto".

                                           






Thursday, March 28, 2013

Ona madhara ya pombe

   picha sita za matukio ya watu baada ya kunywa pombe hebu zione na ufurahie.Pombe ni raha ya muda ambayo baadae huleta kujilaumu bora uwe soba chonde chonde ulevi noma cheka na picha hizi hapa.                                                  
                                               
                                                   
                                             
                                                         
                                                                                                                                                                                     



Wednesday, March 27, 2013

Mabinti waongoza kwa maambukizi ya ukimwi

Ripoti ya viashiria vya Ukimwi nchini katika mwaka 2011/12 imeonyesha kuwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 23 na 24 wameambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 6.6, ikilinganishwa na wavulana wa umri huo ambao ni asilimia 2.8. Akisoma ripoti hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania, (Tacaids), Dk Fatuma Mrisho alisema kiwango cha wasichana wa umri huo wenye virusi ni mara mbili zaidi ya wavulana.

Akizindua ripoti hiyo, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza Watanzania na sekta zote zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi, zitilie mkazo umuhimu wa kukomesha unyanyapaa na kuhamasisha upimaji wa hiari.

“Watanzania zaidi ya milioni mbili wamefariki tangu Ukimwi ugundulike miaka 30 iliyopita, tunatakiwa tupambane kwa dhati kabisa,” alisema Rais Kikwete.
Alipongeza ongezeko la idadi ya watu waliopima kwa hiari na kuwataka wanaume kupima badala ya kuwaachia jukumu hilo wanawake.

Rais pia alizitaka taasisi za Ukimwi, kudhibiti kasi ya maambukizi katika miji mikubwa na katika barabara kuu zikiwemo za Chalinze na Njombe.
“Maeneo hayo yanahitaji nguvu zaidi, hata maeneo yenye kiwango kidogo cha maambukizi nayo yasibweteke yanahitaji tahadhari,” alisema.

Kuhusu tohara kwa wanaume, Rais Kikwete alisisitiza zaidi tohara kwa wanaume na kwamba wasiotahiriwa wanaongeza kasi ya maambukizi kwa asilimia 60 na wanaotahiriwa wanapunguza kwa asilimia 60 pia.

Kwa upande wake, Dk Kikwete alisema maambukizi kwa vijana wenye umri mdogo yanatokea wakati vijana hao wana umri wa kati ya miaka 15 na 19 na matokeo yake kuwa wazi katika umri wa miaka 23 na 24. Alisisitiza kuwa matokeo haya ni kama ya sensa na kwamba si kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 14 hadi 49 amepimwa.

“Kwa jumla asilimia 2.0 ya wasichana na wavulana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wana maambukizi ya virusu,” alisema. Hata hivyo ripoti hiyo ilionyesha kuwa kasi ya maambukizi kwa Tanzania nzima, imepungua kutoka asilimia 5.8 mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/2012.

Utafiti wa kwanza wa aina hii ulifanywa mwaka 2003 -2004 ambapo maambukizi yalikuwa asilimia 7.06.
Utafiti mwingine ulifanyika mwaka 2009-2010 ambapo maambukizi yalishuka toka asilimia 7 hadi asilimia 5.8

Pia, ripoti hiyo ilionyesha kuwa asilimia tisa ya wasichana na 10 ya wavulana wenye umri wa miaka 15 na 24 walianza kujamiiana kwa mara ya kwanza kabla ya kutimiza miaka 15.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa Mkoa wa Njombe una maambukizi ya juu zaidi ya asilimia 14.8 ya maambukizo kuliko mikoa yote Tanzania.

Maeneo ya visiwani yana asilimia ndogo zaidi ya maambukizi ambapo Unguja ilikuwa na asilimia 1.2 na Pemba asilimia 0.5 tu
“Matokeo ya ripoti hii yatatupa mwanya zaidi wa kujua nini kifanyike na wapi nguvu iongezwe katika kupambana na maradhi haya hatari,” alisema Kikwete.

Takwimu za sasa zinaonyesha kuwa maeneo ya mijini yana maambukizi mengi zaidi ambapo kwa wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.8
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa zaidi ya robo ya Watanzania walioko kwenye ndoa wana maambukizi ya Ukimwi.




huyu ndio mwafrika tajiri mwaka 2013

Gazeti la forbes limemchapisha mwafrika anayeongoza kwa utajili afrika. 
Forbes magazine Declared Aliko Dangote is currently the richest man in Africa in 2013. He is a billionaire from Nigeria, trading goods such as flour, sugar and Large cement industries like Dangote Cement, is Whole Africa’s largest cement manufacturer, with operations in 14 African countries.Dangote is also African Continent Richest man for 2013 year also.

55 years old Aliko Dangote Net worth about $12.2 billion his income source from cement, sugar, flour industries. Aliko Dangote is Africa’s and Nigeria’s Richest Man as of 2013 according to Forbes Magazine with a net worth of $12.2 billion.

Read More at richestman2013.com/richest-man-in-africa-2013/ © Top Richest
                                                                      Aliko Dangote

Cheki haya maajabu yaliyopo Tanzania


WILAYA ya Rungwe Jijini Mbeya ina mambo mengi ya kustaajabisha na miongoni mwa mambo hayo yapo kwenye Mto Kiwila
 Mto Kiwira unazidi kupanda chati kuliko mito mingine wilayani humo kutokana na kuwapo kwa Daraja la Mungu.
 Lakini pia karibu na daraja hilo yapo maajabu mengine yakiwamo ya chekeche la uchafu unaokusanywa na maji  kabla ya kuingia eneo maarufu la Kijungu.
 Kijungu nayo ni sehemu ya Mto Kiwira, ni eneo la ajabu kwa sababu mwamba wake umeumba kitu kama chungu kinachopokea maji yote na kuyapeleka chini bila kupitisha juu ya mwamba
Inaelezwa kwamba mtu anayetaka kuvuka salama kwenye mwamba juu ya Kijungu kutoka upande wa Mashariki lazima atumie mguu mmoja wa kulia na akitokea Magharibi atumie mguu wa kushoto tu ili asitumbukie.

Maajabu mengine ni kuwapo kwa taarifa zinazodai mtu akizama kwenye mto huo, lazima afuatwe mzamiaji mmoja aliyerithi kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo,  aliyezama hawezi kuonekana mpaka siku saba zitakapopita.

Lakini jambo kubwa linaloonekana na kustaajabisha ni  kuwapo kwa daraja  linaloaminiwa na wakazi wa eneo hilo na wilaya nzima ya Rungwe kwamba lilitengenezwa na Mungu  kwenye eneo la  Mto Kiwira unapotenganisha Vijiji vya Lugombo kwa upande wa Mashariki mwa mto huo na kile cha Mboyo  kilichopo Magharibi.


Mafunzo ya JKT yazinduliwa rasmi na Mheshimiwa Raisi Kikwete


Pwani na Handeni.  Amiri Jeshi Rais Jakaya Kikwete, amezindua rasmi mafunzo ya miezi mitatu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa  vijana  wa mujibu wa sheria na vijana.
Jumla ya vijana 1,222 wanashiriki mafunzo hayo.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, pia   amefunga rasmi mafunzo maalumu ya JKT yaliyowashirikisha wabunge 47.
Mafunzo hayo ya awali, yalidumu kwa wiki tatu na yalifanyika katika vikosi mbalimbali nchini.
Hata hivyo, ni wabunge 23 tu waliofanikiwa kuhitimu mafunzo hayo jana.
Rais aliwasili katika Viwanja vya Ruvu JKT kwa helikopta na kisha kupewa taarifa ya jeshi hilo na baadaye kuzindua mafunzo ambayo alisema ni kwa nchi nzima na yatahusisha vijana 4,710 wa mujibu  wa sheria.
Alisema vijana wengine 6,722 watakuwa ni wa kujitoleana kwamba tayari wameshatawanywa katika vikosini. Rais Kikwete alisema uzinduzi huo ni wa kihistoria kwa sababu  mafunzo ya JKT ndiyo sasa yanaanza tena baada ya kufutwa kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita kutokana na kuyumba kwa uchumi.
Alisema hata hivyo  kutokana na umuhimu, Serikali sasa imeamua kurudisha mafunzo hayo ingawa bado kuna  changamoto ya fedha.
Kwa mujibu wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ni kiasi cha Sh7.5 bilioni  tu ndizo zilizotengwa kwa shughuli hizo.
Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Muhuga alisema mafunzo hayo  yatafanyika kwa miezi mitatu na baada ya muda huo vijana wengine watachukua nafasi.
Alisema utaratibu wa vijana kujiunga na jeshi, utakuwa unafanyika kabla ya vijana kwenda vyuo vikuu.
Katika risala yao wahitimu tisa wa Kikosi cha Ruvu JKT, waliishauri Serikali kuboresha masilahi ya askari.
Wabunge hao ni Ester Bulaya, Halima Mdee, Neema Hamid, David Silinde, Murtaza Mangungu, Livingston Lusinde, Yusuph Khamis, Said Mtanda na Mendrad Kigola
                                   
.

aliyemgonga trafiki kizimbani


Dereva Jackson Simbo (43), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, kujibu shtaka la kusababisha kifo cha askari wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani, Elikiza
                                         Mshtakiwa huyo, alifikishwa mahakamani jana.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ladislous  Komanya, alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Machi 18 mwaka huu, katika  eneo la Bamaga, Barabara ya Bagamoyo.
Wakili Komanya alidai kuwa  pamoja na shtaka  hilo, mshtakiwa  pia anakabiliwa na shtaka la kuingilia msafara wa kiongozi, kinyume na sheria. Wakili alidai kuwa akiwa katika sehemu hiyo ya  Bamaga, mshtakiwa  aliingilia msafara wa kiongozi na kushindwa kuheshimu maelekezo yaliyokuwa yakitolewa kwa ishara na askari huyo.
Komanya  aliendelea kudai,  Simbo pia anakabiliwa na  shtaka la  shindwa kutoa taarifa katika kituo chochote cha polisi hadi alipo tafutwa na vyombo vya dola.
Hata Hivyo kwa upande wake, mshtakiwa alikana tuhuma dhidi yake na Hakimu  Kwey  Lusemwa aliahirisha kesi hiyo hadi  Aprili 15, mwaka huu.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana baada ya wakili wake Edward Chuwa kuomba adhaminiwe kwani ametimiza masharti ya kupata mdhamana

Saturday, March 16, 2013

Picha za nusu utupu za Rihana zamnyima raha mama yake

Kwa kawaida mtoto anapoharibika kitabia huonekano ni tatizo la mama hakumfunza.Hiki ndicho kinachomkuta mama yake Rihana .Msanii huyu asiyeishiwa visa na mikasa kama kupiga picha anavuta bangi hata kusababisha kuhahirisha shoo zake sababu ya mafua yaliyosababishwa na uvutaji wa kupindukia wa bangi.
                                                                                                                                                                         
Picha hizo alizoziweka Rihana katika mtandao wa instagram si tu zili muudhi mama yake bali pia zilizua ugomvi kati yake yeye na mama yake .Alipohojiwa na gazeti la Elle UK mchumba huyo wa Cris Brown alisema ''mama yangu alinipigia simu na kuniita nyumbani na kunieleza kuhusu picha za utupu nilizoweka instagram alichanganyikiwa sana  kuhusu mimi nilijiona ameniaibisha sana kama kunichapa fimbo mbele ya darasa shuleni mi simuogopi mtu yoyote kwenye dunia hii ila nilipata hofu kwa mama yangu''.
                                                                                                                                                                   
Hakuishia hapo tu bali mwimbaji huyo wa shine like diamond alisema picha za Rihana akiwa nusu utupu ni nyingi hivyo hazizuiliki kuwa mitandaoni na watu wanazipenda (huku akitabasamu).

Mwonekano wa mtoto wa Kanye na Kim atakapozaliwa

Ni Muafrika mu Amerika Kanye West huku Kim Kardasian ni mtoto wa kizungu yani mu Amerika mweupe ana matiti makubwa huku West akiwa na sura na mdomo mpana .Kim alishawahi kuigiza filamu ya ngono na msanii Ray J aliekua mpenzi wake wa zamani Kanye kaiona mara nyingi ila hajamwacha wala kuchukizwa naye bado anampenda kwa thati na anatarajia mtoto naye.Dunia bado ina maswali mwezi July atakapozaliwa mtoto wa wapenzi hawa maarufu wawili atakua na mwonekano upi.
                                         
 Nikollet Me'r'esz na Nickolay Lamm watafiti kutoka kutoka myvouchercodes.co.uk wamejaribu kuhisi jinsi gani mtoto wa Kanye na Kim atakavyokua katika umri wa miaka 25. Kama akiwa wa kike katika umri wa utoto atafanana na wazazi wake vitu kama nywele , rangi na sura kama hivi mtoto wa kike atakua na sura ya mviringo kama ya baba yake na wa kiume atakua na macho ya rangi na makubwa mchanganyiko kwa mama na baba yake huku nusu ya sura yake ikiwa sawa na ya Kanye West.
                                             
Katika umri wa miaka 25 watafiti hao wanazidi kunyambua mwonekano atakao kua nao mtoto wa wapenzi hao, wanasema Kim aliyejichubua sana uso wake kwa sasa huwezi kujua ataonekana vipi kama asingetengeneza uso wake ,anaonekana kama mtu wa mashariki ya kati kwa rangi yake kama ya muizraeli huku Kanye akiwa ngozi nyeusi hivyo mtoto wao anaweza akawa mweusi kuliko Kim lakini si mweusi sana na atakua na mchanganyiko  wa rangi za wazazi wake na mwonekano kama nywele za kishombe huko inasemekana kuwa hatofanana sana na Kim kutokana na ukweli kuwa Kim amerekebisha kwa kiasi kikubwa mwonekano wake kama kwa kufanyiwa upasuaji wa pua

Thursday, March 07, 2013

Kutoa mvi

Sura iliyojikunja  na michiri ya ngozi kuchoka hivi vyote huashiria dalili za mtu kuzeeka pia mvi nazo ni dalili ya mtu kuzeeka na husemekana kuwa ni busara ila kwa kizazi hiki sa hivi mvi sio kigezo cha busara wala uzee kuna vijana wa miaka kumi na tatu wana mvi tena nyingi zaidi ya za wazee.
Kuwa na mvi ni kigezo cha mwili wa binadamu kushindwa kutengeneza kemikali aina ya MELANIN inayofanya kazi kutengeneza rangi ya asili katika nywele.Kemikali hii inapatikana katika vyakula vya vitamini B12 je kama kijana ungependa kurudisha nywele zako za asili na usichekwe na wenzako kwa kuitwa babu fuata njia zifatazo ili kutoa kabisa mvi katika kichwa chako:-
                         
                              KUBADILI RANGI YA NYWELE AU MTINDO WA NYWELE.
Kama kijana ukijiona mvi zinakuja ndani ya kichwa chako na uzitaki badilisha rangi ya nywele kwa kupaka rangi tofauti za nywele kama piko wengine wanaweza kubadili stairi ya nywele kabisa kwa kunyoa vipara kuzuia nywele kuota hapo utazuia tatizo hilo la mvi.


                            TUMIA SHAMPOO ZA NYWELE ZA KUTOA MVI.
Kuna shampoo madukani za kutoa mvi zenye vitamini B12 na omega 3's kwa kwetu Tanzania hizi zina gharama sana zinafika hadi 30,000 pesa ya Kitanzania ila zinasaidia kama hii hapa Emu oil shampoo .Onyo sio shampoo zote zinaweza kutoa mvi na kufanya kazi kwa haraka ivyo pata ushauri wa wataalamu wa nywele kwanza.

                               TUMIA VYAKULA VYA VITAMINI B12
Vyakula vyote vyenye vitamini B12 kama samaki;wote, nyama, maziwa ,siagi kama vile blue band vinatakiwa kuwepo katika mlo wako wa kila siku hivi vitasaidia kuongeza madini ya melanin kwa ajili ya kutengeneza rangi ya nywele hii itasaidia kutoa kabisa mvi .
Kijana fanya hivyo urudishe ujana wako na usijifiche kuogopa kuchekwa na rafiki zako kwamba una mvi zitoe sasa na ufurahie ujana wako.

HEALTH BENEFIT OF SEX

When you are in the moody extend well beyond the bedroom turns out sex is good for you in ways you may never have imagine it is a sure that the last thing on your mind is boosting your immune system or maintaining a health weight yet good sex offer those health benefits and more.Among the benefits of health loving in a relationship are:-

                                             1:SEX RELIEVES STRESS.
An important benefit of sex is lower blood pressure and overall stress reduction, according to the researchers from scottland they studies 24 women and 22 men who kept record on their sexual activities. Then the researchers subjected them to stressful situations such as speaking in public and doing verbal arithmetic and noted their blood pressure response to stress as those who had intercourse had better responses to stress than those who engaged in other sex behaviour.
Another study published in the same year by the same journalist that frequent intercourse was associated with lower diastolic blood pressure in cohabiting participants.yet other research found a link between partner hugs and lower blood pressure in women.
                       
                                            2:SEX BOOST IMMUNITY.
Good sexual health may mean better physical health.Having sex once or twice a week has been linked with higher levels of an antibody called immunoglobulin A or Ig A which can protect you from getting colds and other infections.Scientist at Wilkes University took sample of saliva which contain Ig A from122 college students who reported the frequency of sex they had .Those in frequent group once or twice a week had higher level of Ig A than those in other groups who abstain from having sex less than once a week.
                                       
                                                 3:SEX BURN CALORIES.
Thirty minutes of sex burns 85 calories or more.It may not sound like much but it adds up to 45 half hour session will burn 3570 calories more than enough to lose a pound .Doubling up you could drop that pound(kilo) in 21 hours long session.
Sex is agreat mode of exercise says "Patt Brighton" a PhD Loss Angels sexiologist and president of the American association of sexuality.