Wednesday, March 27, 2013

Cheki haya maajabu yaliyopo Tanzania


WILAYA ya Rungwe Jijini Mbeya ina mambo mengi ya kustaajabisha na miongoni mwa mambo hayo yapo kwenye Mto Kiwila
 Mto Kiwira unazidi kupanda chati kuliko mito mingine wilayani humo kutokana na kuwapo kwa Daraja la Mungu.
 Lakini pia karibu na daraja hilo yapo maajabu mengine yakiwamo ya chekeche la uchafu unaokusanywa na maji  kabla ya kuingia eneo maarufu la Kijungu.
 Kijungu nayo ni sehemu ya Mto Kiwira, ni eneo la ajabu kwa sababu mwamba wake umeumba kitu kama chungu kinachopokea maji yote na kuyapeleka chini bila kupitisha juu ya mwamba
Inaelezwa kwamba mtu anayetaka kuvuka salama kwenye mwamba juu ya Kijungu kutoka upande wa Mashariki lazima atumie mguu mmoja wa kulia na akitokea Magharibi atumie mguu wa kushoto tu ili asitumbukie.

Maajabu mengine ni kuwapo kwa taarifa zinazodai mtu akizama kwenye mto huo, lazima afuatwe mzamiaji mmoja aliyerithi kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo,  aliyezama hawezi kuonekana mpaka siku saba zitakapopita.

Lakini jambo kubwa linaloonekana na kustaajabisha ni  kuwapo kwa daraja  linaloaminiwa na wakazi wa eneo hilo na wilaya nzima ya Rungwe kwamba lilitengenezwa na Mungu  kwenye eneo la  Mto Kiwira unapotenganisha Vijiji vya Lugombo kwa upande wa Mashariki mwa mto huo na kile cha Mboyo  kilichopo Magharibi.


0 comments:

Post a Comment