Kuwa na mvi ni kigezo cha mwili wa binadamu kushindwa kutengeneza kemikali aina ya MELANIN inayofanya kazi kutengeneza rangi ya asili katika nywele.Kemikali hii inapatikana katika vyakula vya vitamini B12 je kama kijana ungependa kurudisha nywele zako za asili na usichekwe na wenzako kwa kuitwa babu fuata njia zifatazo ili kutoa kabisa mvi katika kichwa chako:-
KUBADILI RANGI YA NYWELE AU MTINDO WA NYWELE.
Kama kijana ukijiona mvi zinakuja ndani ya kichwa chako na uzitaki badilisha rangi ya nywele kwa kupaka rangi tofauti za nywele kama piko wengine wanaweza kubadili stairi ya nywele kabisa kwa kunyoa vipara kuzuia nywele kuota hapo utazuia tatizo hilo la mvi.
TUMIA SHAMPOO ZA NYWELE ZA KUTOA MVI.
Kuna shampoo madukani za kutoa mvi zenye vitamini B12 na omega 3's kwa kwetu Tanzania hizi zina gharama sana zinafika hadi 30,000 pesa ya Kitanzania ila zinasaidia kama hii hapa Emu oil shampoo .Onyo sio shampoo zote zinaweza kutoa mvi na kufanya kazi kwa haraka ivyo pata ushauri wa wataalamu wa nywele kwanza.
TUMIA VYAKULA VYA VITAMINI B12
Vyakula vyote vyenye vitamini B12 kama samaki;wote, nyama, maziwa ,siagi kama vile blue band vinatakiwa kuwepo katika mlo wako wa kila siku hivi vitasaidia kuongeza madini ya melanin kwa ajili ya kutengeneza rangi ya nywele hii itasaidia kutoa kabisa mvi .
Kijana fanya hivyo urudishe ujana wako na usijifiche kuogopa kuchekwa na rafiki zako kwamba una mvi zitoe sasa na ufurahie ujana wako.
0 comments:
Post a Comment