Monday, September 28, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 8

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 8
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Hayo yalikua magumu maamuzi ila Irene alipofiri na kuona mbali hiki ndicho alifanya
Irene: Shikamoo mwalimu
Mwl.Mnubi: Irene nimesema sitaki
Shikamoo yako kama hauna majibu ya
kuniridhisha.
Irene: mwalimu hata kabla sijajibu jamani
Mwl.Mnubi: usinipotezee muda Irene na si
unajua mlifanya mtihani juzi juzi hapa ngoja
nikuonyeshe sasa kama hupati zero.
Irene: haaaa mwalimu hapana hapana
kabisaaaa mi nimekubali nimekubali kabisa
ila kwa sharti moja tu nitachagua eneo la
kukutana.
Mwl.Mnubi: Hahahaha umeshanyooka
tembo hashindwi na mkonga wake shika hii
elfu Mbili utatafuta chumba hee ( huku
akimshikashika)
Irene: sawa
Ulikua ni mtego alioutega Irene kumkomesha mwalimu Mnubi alimwambia mwalimu mkuu na mwalimu mkuu kwa kuwa alikua ni mama aliona uchungu na kuwaalifu polisi hivyo walisubiri muda
muafaka wamkamate kweli mida ya jioni walikutana kwa kuwa Irene aliishi shule haikua tabu kuonana na Mwl.Mnubi wakaenda hadi kishamapanda guest house iliyokua mtaa wa uhuru kweli taratibu zote
zilifatwa na ulikua ni muda wa mwalimu Mnubi kula kisamvu cha kopo weee kwani mwalimu mkuu alipoteza muda sasa hapo hapo kabla ya tendo aligonga mlango akiwa na polisi kadhaa maskini mwalimu Mnubi kiulaini akakamatwa kwanza kazi akafukuzwa na kifungo cha miaka 30 juu Irene alionekana shujaa na mfano wa kuigwa kwa mabinti wenzake sasa kila mvulana na hata walimu wa kiume
waliogopa kumtongoza na kumfata.Hicho kilimuhakikishia kusoma bila tabu shuleni. Dayness alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike jina lake Martha mtoto wa kike mzuri sijapata kuona mweupee acha tu. Adam
aliendelea na masomo yake hadi akamaliza masomo yake ya kidato cha sita na Irene pia akamaliza kidato cha nne ila hakupenda kuendelea na kidato cha tano kwa sababu mzee Shaban aliyekua tegemeo lake kubwa alifariki dunia maskini atafanya nini Irene tegemezi lake ndio hilo lilifutika kama
mshumaa hakuwa na jinsi Irene alilia sana ila akajikaza na kumchukua mwanae wakaishi mjini wote mwanae kwa sasa alikua kafika darasa la tatu huwezi amini jinsi mzee shaban alivyompenda Irene
kabla ya kifo chake alimpa kwa siri Vatican pesa nyingi sana na kumwambia atampa mama yake na zitawasaidia baadae. Irene kwa kuwa hakuwaamini sana wake wenzake aliona bora awaachie kila kitu .
Yeye na mwanae Vatican walienda kuishi mjini Vatican alimwambia mama yake kuhusu pesa alizopewa na mzee Shaban ilikua ni kiasi cha laki tatu kwa miaka ile ilikua ni pesa kubwa sana.Irene alifika na
kupanga chumba mjini kwa elfu moja kwa mwezi pia aliitumia pesa hiyo kujenga nyumba na kununulia kiwanja jumla elfu 80 hivi kisha pesa zilizobaki alimpeleka mwanae shule na pia yeye alijisomesha kwa kwenda chuo cha ualimu butimba.Adam aliendeleza umaarufu wake sasa kwa kupasua na kwenda chuo. Haya ndio yalikua maisha mapya ya mwalimu mtarajiwa Irene mwanzo wa chuo ulikua changamoto sana kwake ila alivumilia kwa yote na kujitesa usiku na mchana kusoma kwa bidii ili atimize malengo yake kweli miaka miwili ilipita na Irene akafanikiwa kupata ualimu wa daraja la kwanza au ualimu wa shule ya msingi na alipangiwa kufundisha shule ya msingi kitangiri.Adam sio siri alizidi kupasua tu sasa alibakisha mwaka mmoja amalize chuo yeye alisomea masomo ya biashara yani uhasibu na kwa kuwa hesabu hazikumpiga chenga yani ilikua mterezo kama kumpiga chura mateke hahahahaha mambo ya Adam hayo. Kama unavyojua mtoto lazima aige kwa Baba daaah acha kabisa Vatican aliwatesa vibaya sana wenzake darasani kwa kushika nafasi ya kwanza kila mtihani aliopewa. Martha naye ndio alikua anakua kua kidogo kidogo miaka ikasonga Adam sasa alimaliza masomo yake ya chuo kikuu na kuajiliwa kama mwasibu mkuu wa TBL kampuni ya bia mwanza .Huko alijijenga kimaisha na akaweza kuhama kwa Paschal na kuanza kujitegemea yeye na familia yake mwaka mmoja baadae Adam rasmi aliuacha ukapera na kufunga pingu za maisha na mama Martha a.k.a Dayness ilikua ni ndoa takatifu katika kanisa watu walifurahi kula kucheza kunywa hadi wengine wakashindwa kutembea kama Rwambo na Marwa ambao walikunywa kreti tatu wawili kama kawaida Derick alizama show mjini na kuwa best man wa Adam kwenye harusi hiyo . Mafanikio kwa Irene kama mama mpambanaji yalianza kujitokeza kwani Irene alitangazwa rasmi kuwa mwalimu mkuu wa kitangiri shule ya msingi aisee ilikua ni hatua kubwa sana kwa Irene ambae alikua bado binti sana kupata nafasi hiyo ila ndio bahati yake hiyo

0 comments:

Post a Comment