Monday, September 28, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 8

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 8
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Hayo yalikua magumu maamuzi ila Irene alipofiri na kuona mbali hiki ndicho alifanya
Irene: Shikamoo mwalimu
Mwl.Mnubi: Irene nimesema sitaki
Shikamoo yako kama hauna majibu ya
kuniridhisha.
Irene: mwalimu hata kabla sijajibu jamani
Mwl.Mnubi: usinipotezee muda Irene na si
unajua mlifanya mtihani juzi juzi hapa ngoja
nikuonyeshe sasa kama hupati zero.
Irene: haaaa mwalimu hapana hapana
kabisaaaa mi nimekubali nimekubali kabisa
ila kwa sharti moja tu nitachagua eneo la
kukutana.
Mwl.Mnubi: Hahahaha umeshanyooka
tembo hashindwi na mkonga wake shika hii
elfu Mbili utatafuta chumba hee ( huku
akimshikashika)
Irene: sawa
Ulikua ni mtego alioutega Irene kumkomesha mwalimu Mnubi alimwambia mwalimu mkuu na mwalimu mkuu kwa kuwa alikua ni mama aliona uchungu na kuwaalifu polisi hivyo walisubiri muda
muafaka wamkamate kweli mida ya jioni walikutana kwa kuwa Irene aliishi shule haikua tabu kuonana na Mwl.Mnubi wakaenda hadi kishamapanda guest house iliyokua mtaa wa uhuru kweli taratibu zote
zilifatwa na ulikua ni muda wa mwalimu Mnubi kula kisamvu cha kopo weee kwani mwalimu mkuu alipoteza muda sasa hapo hapo kabla ya tendo aligonga mlango akiwa na polisi kadhaa maskini mwalimu Mnubi kiulaini akakamatwa kwanza kazi akafukuzwa na kifungo cha miaka 30 juu Irene alionekana shujaa na mfano wa kuigwa kwa mabinti wenzake sasa kila mvulana na hata walimu wa kiume
waliogopa kumtongoza na kumfata.Hicho kilimuhakikishia kusoma bila tabu shuleni. Dayness alifanikiwa kujifungua mtoto wa kike jina lake Martha mtoto wa kike mzuri sijapata kuona mweupee acha tu. Adam
aliendelea na masomo yake hadi akamaliza masomo yake ya kidato cha sita na Irene pia akamaliza kidato cha nne ila hakupenda kuendelea na kidato cha tano kwa sababu mzee Shaban aliyekua tegemeo lake kubwa alifariki dunia maskini atafanya nini Irene tegemezi lake ndio hilo lilifutika kama
mshumaa hakuwa na jinsi Irene alilia sana ila akajikaza na kumchukua mwanae wakaishi mjini wote mwanae kwa sasa alikua kafika darasa la tatu huwezi amini jinsi mzee shaban alivyompenda Irene
kabla ya kifo chake alimpa kwa siri Vatican pesa nyingi sana na kumwambia atampa mama yake na zitawasaidia baadae. Irene kwa kuwa hakuwaamini sana wake wenzake aliona bora awaachie kila kitu .
Yeye na mwanae Vatican walienda kuishi mjini Vatican alimwambia mama yake kuhusu pesa alizopewa na mzee Shaban ilikua ni kiasi cha laki tatu kwa miaka ile ilikua ni pesa kubwa sana.Irene alifika na
kupanga chumba mjini kwa elfu moja kwa mwezi pia aliitumia pesa hiyo kujenga nyumba na kununulia kiwanja jumla elfu 80 hivi kisha pesa zilizobaki alimpeleka mwanae shule na pia yeye alijisomesha kwa kwenda chuo cha ualimu butimba.Adam aliendeleza umaarufu wake sasa kwa kupasua na kwenda chuo. Haya ndio yalikua maisha mapya ya mwalimu mtarajiwa Irene mwanzo wa chuo ulikua changamoto sana kwake ila alivumilia kwa yote na kujitesa usiku na mchana kusoma kwa bidii ili atimize malengo yake kweli miaka miwili ilipita na Irene akafanikiwa kupata ualimu wa daraja la kwanza au ualimu wa shule ya msingi na alipangiwa kufundisha shule ya msingi kitangiri.Adam sio siri alizidi kupasua tu sasa alibakisha mwaka mmoja amalize chuo yeye alisomea masomo ya biashara yani uhasibu na kwa kuwa hesabu hazikumpiga chenga yani ilikua mterezo kama kumpiga chura mateke hahahahaha mambo ya Adam hayo. Kama unavyojua mtoto lazima aige kwa Baba daaah acha kabisa Vatican aliwatesa vibaya sana wenzake darasani kwa kushika nafasi ya kwanza kila mtihani aliopewa. Martha naye ndio alikua anakua kua kidogo kidogo miaka ikasonga Adam sasa alimaliza masomo yake ya chuo kikuu na kuajiliwa kama mwasibu mkuu wa TBL kampuni ya bia mwanza .Huko alijijenga kimaisha na akaweza kuhama kwa Paschal na kuanza kujitegemea yeye na familia yake mwaka mmoja baadae Adam rasmi aliuacha ukapera na kufunga pingu za maisha na mama Martha a.k.a Dayness ilikua ni ndoa takatifu katika kanisa watu walifurahi kula kucheza kunywa hadi wengine wakashindwa kutembea kama Rwambo na Marwa ambao walikunywa kreti tatu wawili kama kawaida Derick alizama show mjini na kuwa best man wa Adam kwenye harusi hiyo . Mafanikio kwa Irene kama mama mpambanaji yalianza kujitokeza kwani Irene alitangazwa rasmi kuwa mwalimu mkuu wa kitangiri shule ya msingi aisee ilikua ni hatua kubwa sana kwa Irene ambae alikua bado binti sana kupata nafasi hiyo ila ndio bahati yake hiyo

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 7

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 7
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Adam sasa alizidi yani alimgeuza Dayness mke kabisa yani ilikua kazi na dawa hatimaye Dayness akapata ujauzito.Siku ya kwanza shule ndio hii kwa Irene na alipokua kwenye mstari mara ghafla. Wapeni wali wao waulao wale. Hahahaha
sio ulichofikiria bali Irene alimwona mwalimu mnubi aliyemfundisha shule ya msingi na akaenda mjini kusoma sasa alikua ni mwalimu wa sekondari Irene alishangaa kumwona kwani ilikua ni muda  tangu waonane hiyo ilimpa furaha kwani alipata mwenyeji mjini na asingesumbuka sana kuizoea shule na kizuri zaidi alikua ndio mwalimu wake wa darasa sasa kibaya kilikua ni hiki mwalimu huyu alikua anampenda Irene tangu zamani shule ya msingi na alishawahi kumshawishi afanye mapenzi naye zamani sasa hiyo ilikua changamoto kwake ila hakusita kuionyesha furaha yake hivi
Irene: mwalimu Mnubi jamani Shikamoo
mwalimu
Mwl.Mnubi (huku akitaka kumpotezea)
marahaba panga mstari vizuri haa nani
Irene marahaba za siku
Irene: nzuri mwalimu za mjini
Mwl.Mnubi: nzuri Karibu mjini Karibu sana
Irene: Ahsante mwalimu
Mwl.Mnubi: sawa upo darasa gani
Irene: form one B
Mwl.Mnubi: haya ntakutafuta (huku akiamlisha mguu pande mguu sawa)                               Shule haikua tabu sana kwake Irene kwa kuwa alipata kila alichokihitaji na mzee Shaban alihakikisha anampa matumizi Irene kwa muda muafaka ila huwezi amini Irene hakuwahi kukutana kabisa na Adam kwani Mwanza sekondari ilikua shule kubwa sana iliyokua na wanafunzi zaidi ya elfu tatu hivyo wanafunzi waliingia kwa zamu asubuhi na jioni hivyo kidato cha nne wakiingia saa 1 asubuhi basi cha kwanza waliingia mchana saa 6 hivyo ilikua ngumu kwa wawili hao kukutana hadi Adam akamaliza hapo kidato cha nne.Irene yeye aliendelea na masomo yake.Adam aliukubali ujauzito wa Dayness kwani alimpenda kweli na muda wa kujifungua nao ndio huo ulikaribia sasa kituko ni kwamba Dayness alifukuzwa kwao baada ya ujauzito kujulikana na sasa aliishi na Adam pamoja na paschal ila Paschal alichukia basi tu hakutaka kuonyesha hasira zake kwa Adam. Mwalimu mnubi naye aliona ndio muda muafaka wa cheo kutumika vibaya kwa Irene ni pale mwalimu Mnubi alipo muomba penzi Irene tena na sasa alimtishia kumfelisha kama asingekubali jamani jamani yalikua maamuzi magumu kwa Irene kufanya na alipewa siku tatu tu kufanya maamuzi hayo Kweli Irene alifikiria na hiki ndicho alicho mjibu mwalimuMnubi. Maamuzi ya kupanda mnazi hufanywa namkwezi muuza mbaazi kakupa mashuzi.Hayo yalikua magumu maamuzi ila Irene alipofiri na kuona mbali hiki ndicho alifanya

Sunday, September 27, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 6

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 6
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com
Kilichoendelea humo mi na we hatukifahamu labda hiki kilichokua kinataka kuendelea kwa Adam , siku hiyo bwana Adam kipindi anatoka shule Dayness aling'ang'ania kwamba ampeleke Adam akapaone kwao Adam naye akasitasita mara aliposhikwa mkono tu na Dayness kwani alisema chochote huyoooo akawa mlaini wakaenda wote. Dah kwao Irene kwa kitajiri sana ona mazingira ya nje na ndani yalivyokua mazuri alijisemea Adam akiwa amekaa sebuleni anashangaa TV ya Sony black & white yani isiyo na rangi mara Dayness si huyo kapita mara kaenda jikoni mara chooni mara bafuni mwishowe ikawa kero sasa kumbe yeye yupo kwenye show kumteka akili Adam ili amtamani mara akamletea soda ya fanta kipindi kile zipo kwenye chupa kubwa sana kama ya kupimia mafuta ya kura fanta sa hivi duuuu Adam akashangaa kweli kweli , sawa maisha haya alishaanza kuyazoea alipokua kwa Paschal ila leo kwa Dayness daaaaaaah Adam alishangaaa sana na kwa bahati nzuri au mbaya siku hiyo wazazi wa Dayness hawakuwepo nyumbani walikwenda kwenye harusi hivyo wangerudi usiku sana sasa lindo halina mlinzi nafasi kwa wezi kuchukua vya wazi. Kabla hata hajamaliza soda tayari Dayness mara kakaa juu ya kiti mara kapanda juu ya meza na sketi yake fupi ya shule Adam alikua anaona kabati wazi wazi mamaaaaaaaa sasa hili jaribio la mwisho ndio lilikua kali zaidi baada ya Adam kuepuka majaribio yote haya Dayness si akaaga kama anakwenda kuoga ghafla kajimwagia maji tu haraka haraka akatoka mamamamamamama kanga ilivyokua imemshika kisha akapita sebuleni hapo hapo alipokua Adam na ghafla Kama jadi ya Adam hua aachii nafasi wazi kama hizo pole pole akamvuta Dayness hadi karibu na Kochi alipokua amekaa akamsukuma kwa nguvu hadi akalala chali kwenye kochi na kwa vile alikua kavaa kanga moja haikua kazi ngumu kwa Adam kutoa nuksi daaaah mtendwa katendewa tendo lililotendeka katika amri kumi za Mungu moja ikavunjika siku hiyo . Vatican naye ndio huyo anaiona ona dunia malezi mazuri ,ulinzi afya na chakula bora vyote alivipata hivyo alikua mtoto mwenye afya mnene si mchezo. Baada ya Adam kumfukuza mchawi sasa rasmi alitangaza mahusiano sasa hivi ilikua rahiiiiiisi kweli wala hata hakuhangaika na ndio ulikua mara ya kwanza kwa Adam kutongoza na kumtamkia msichana kwamba anampenda na alitamka kwa Dayness. Miaka ikasonga sasa na Adam akafanikiwa kufaulu darasa la saba na kujiunga na kidato cha kwanza shule ya Mwanza sekondari. Kwa bahati mbaya Dayness yeye mambo kwake yalimuendea kombo hakupata nafasi ya kwenda kidato cha kwanza hivyo akawa mama wa nyumbani tu ila mapenzi yao na Adam hayakuisha.Irene naye sasa aliamua kulivalia njuga swala la yeye kurudi shule basi mzee shabani baada ya kuona usumbufu sana alimrudisha Irene shule na alianza darasa la nne, shule kwake ilikua changamoto kwa kuwa tayari alikua ni mama hivyo alikua na majukumu mawili na muda mwingine alipokua shule alikua anamuwaza mwanae nyumbani.Miaka ilisogea Vatican naye akazidi kukua na sasa mama yake alihitimu darasa la saba na kufanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza ila sasa shule aliyochaguliwa ilikua ile ile anayosoma Adam na Adam kwa kipindi hicho alikua tayari kafika kidato cha nne. Kweli taratibu zilifanywa na mzee Shaban kuhakikisha mke wake anakwenda mjini kusoma ila Vatican ndio ivyo alikua anaachwa mpweke bila ya mama ambaye ndio alikua kila kitu kwake ila kwa sasa umri wake ulikaribia aanze shule ya msingi kwani tayari alikua na miaka sita hivyo haikua tatizo sana kwake kuachwa na mama bali upweke kwa kuwa alimzoea sana mama yake kuliko mtu mwingine katika familia ya mzee shaban si mama zake wengine yani wake wa mzee shaban au hata ndugu zake watoto wa mzee shaban.Irene leo ndio ilikua safari yake kwenda kuanza shule mjini Mwanza aliwaaga ndugu jamaa na marafiki na kwenda.Alifika salama na alitakiwa kuripoti shule siku hiyo hiyo ili apewe chumba chake kwa kuwa yeye alitakiwa kulala hapo shule yan boarding.Adam sasa alizidi yani alimgeuza Dayness mke kabisa yani ilikua kazi na dawa hatimaye Dayness akapata ujauzito

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 5

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 5
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Ndivyo alivyofanya mzee Shabani na akamuoa Irene kama mke wake wa tatu. Kuolewa kwa Irene kulimrudishia heshima yake sana kijijini hapo watu walianza kumuheshimu na kumuona mama mwenye ndoa yake hata baba yake pia alirudisha mapenzi yake kwa mwanae na kumpa onyo kwamba hata siku moja asije akajaribu kurudiana tena na Adam hata kama akirudi kijijini hapo.Maisha yalimwendea vizuri sana Irene na alipendwa sana na jamii nzima nzima iliyomzunguka miezi tisa ya furaha Irene alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume jina lakeVatican kwa kuwa siku anajifungua alipata uchungu karibu na kanisani na ma sister wamissionari ndio waliomsaidia kujifungua hivyo wakampa jina Vatican yani mtakatifu aliyezaliwa kanisani.Adam masomo kwake yalikua kama mtelezo alijijengea uaminifu kwa Paschal kwamba kweli hatorudia kosa kama la kijijini kumbe wapi alificha makucha tayari alikua naye ameshampenda Dayness aliekua anajipendekeza kwake.Sema tu Adam kwenye kuongea yeye alikua mwoga kazi yake yeye alikua mtu wa matendo kama alivyofanya kwa Irene . Masomo kwa Adam aliyapa umuhimu sana kipindi hiki labda ni kwa sababu sasa alikua mtu mzima kwani tayari Adam alikua na umri wa miaka 19. Umri huo ulimtosha kupambanua mengi na kuelewa mengi zaidi, kijijini napo nderemo na vifijo vya hongera vilitawala pale Vatican alipoiona dunia kuzaliwa kwake kulileta mabadiliko mapya katika maisha ya Irene sasa Irene alikua mpya mwenye furaha na huru kwani sasa hakufungwa na mimba tena kama zamani hivyo alidhani angepata muda wa kusoma baadae kwa kuwa alipenda sana shule na alijua umuhimu wa shule katika maisha yake kwani alishaona jamii jinsi ilivyomtenga mwanzoni hivyo msaada wake pekee ulikua elimu .Irene alijaribu kumshawishi mume wake wa sasa mzee Shaban kuhusu masomo ilikua hivi siku hiyo mzee Shaban alikwenda kumtembelea Irene kwenye chumba chake kwa kuwa yeye alikua na wake watatu hivyo kila mwanamke alikua na zamu yake kulala kwake katika wiki siku mbili na siku hiyo ilikua zamu ya mzee Shaban kulala kwa Irene wakati wakiwa kitandani Irene akaanza
Irene:mmhhmhhhhmhhh (akijikoholesha) unajua baba Vatican unaonaje mi nikirudia shule nisome kidogo
Mzee Shaban: hapana hapana kabisa kwa hilo wala hata sitaki kulisikia unataka urudishe mambo kama yaliyokupata mwanzo huko shule hakuna faida sipendi kabisa urudi tena shule yani ukapewe mimba nyingine mi nije nileee heeee ndo unataka hivyo au sababu mi nimezeeka ndio unanidharau.
Irene: sio hivyo baba Adam jamani mi nakuheshimu sana hayo yametokea wapi tena mi niliomba tu kama ingewezekana nikarudi shule na wala siwezi kurudia makosa ya zamani naapa kwa Mungu huo ulikua utoto tu kwanza we nani kasema mzee ng'ombe tangu lini azeeke maini .
Mzee Shaban: si ndio hapo nilitaka kushangaa mke wangu tena mambo gani hayo ananiletea sasa
Irene: mhhhhhhhhhhhh
mzee Shaban : we mwenyewe umelitambua hilo kwamba ng'ombe hazeeki maini sogea basi karibu tuwaumize wachawi.
irene: mhhhhhhhh we mzee nawe nilijua tu shida yako nini yani umezunguka kumbe shida yako ndogo tu wazee bwana waoga kweli kusema ila jamani hata sijapona vizuri.
Mzee Shaban: haaaa hivyo hivyo kwanza si kidogo tu utaponea huko huko bwana hebu njoo(huku akijifunika shuka) .                                                                                       Kilichoendelea humo mi na we hatukifahamu labda hiki kilichokua kinataka kuendelea kwa Adam

Friday, September 25, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 4

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 4
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Jimmy ndiye aliyesuka mipango ya kumtorosha Adam usiku wa manane na kumpeleka mjini .walikwenda kwa miguu hadi wakafika pasiansi Mwanza kutoka kwao kijijini Kayenze nyafura.Jimmy alimuaga Adam ili arudi nyumbani na kumwachia shillingi ishirini kama ya kutumia akiwa mjini. Huku kijijini napo kesho yake wanagundua kwamba Adam hayupo ndani ya kijiji kile kwamba alishatoroka baba yake Irene alimgawia Irene urithi wake kwa kumpa kiwanja ,shamba , na mtoto wang'ombe mdogo ili aaanze maisha kisha akamfukuza na kusema hamtambui kama mtoto wake sio yeye tu bali kijiji kizima kilimtenga na ukoo wake pia allionekana kaiaibisha jamii hiyo nzima na pigo kubwa la mwisho Irene alifukuzwa shule alijuta kwa nini alinasa katika mapenzi na Adam aliyemtelekeza. Sasa alikua na kazi mbili moja ni kuhakikisha anapata chakula na pili kutunza ujauzito wake na kupata mahali pa kulala.Siku moja Irene akiwa kisimani mara akasikia vicheko'' hehehehheeee ndege mjanja kanaswa kwenye tundu bovu kumbe ndio wanayosoma shule hayo'' alikua ni Magreth na Rachel kiukweli ilimuuma sana akikumbuka kisha ye mwenyewe akaanza kuwaza moyoni akijisemea ''yani ilikua mara moja tu tena mara ya kwanza hii mimba imetokea wapi'' hakujua jibu lake kwani hakuna na elimu ya uzazi. Adam naye huko mjini alianza maisha mapya ya kuishi mitaani pesa aliyopewa na kaka yake sasa ilikwisha uwezekano wa kula ukapungua hapo ndipo Adam alipoamua kuanza kuosha magari na kufanya vibarua ili apate chochote tumboni. Wote wawili Irene na Adam waliishi maisha ya tabu hadi walikumbuka nyumbani walipopata ugali wa bure kila siku ila walikua walishamwaga ugali na familia zao zikamwaga mboga.Kama bahati nzuri akiwa mjini Adam alipata ahueni ni kama bahati Adam alikutana na Paschal mtoto wa mzee Wamichongo aliyekua jirani yao na Adam huku kijijini.Paschal alikutana ma Adam car wash alipopeleka kuosha gari lake alishangaa kumuona Adam mjini ila kitu cha kwanza ilibidi ampeleke nyumbani kisha baada ya kupata chakula paschal akamuuliza Adam:-
 Paschal: ehehe habari za nyumbani Adam                                                                              Adam: kwa kweli ni salama kwao ila sio kwangu.
Paschal: unamaanisha nini
Adam: mimi kaka nyumbani nilitoroka nilipata matatizo
Paschal: matatizo gani mdogo wangu.
Adam: kaka nilimpa mimba Irene wazazi wakanilazimisha nimuoe na niache shule ili nilime nimtunze na mimi ninapenda sana shule nikaamua kukimbilia mjini huku ili nisome.
Paschal: pole sana mdogo wangu hapa sasa umefika nyumbani hapa utasoma vizuri tu ila nisingependa urudie kosa ulilolifanya kijijini.
Adam: ahsante kaka naahidi sitarudia kosa la kumpa mimba binti yoyote .
Paschal: sawa mdogo wangu pumzika kesho tutaona mpango wa shule.
Adam: ahsante kaka usiku mwema.
Paschal : nawe pia usiku mwema Adam.
Paschal alikua anafanya kazi benki kama bank teller wa benki ya posta hivyo pesa haikua tatizo kwake naye pia alitorokea mjini zamani na kuja mjini kama Adam.Irene aliendelea kupata shida na matatizo kila kukicha alikwenda mbali kuchota maji , kujipikia kukata kuni na kulima na kuitunza mimba yake siku moja alipokwenda kisimani Irene alikua kabeba ndoo nzito ya maji alipofika kwenye mpando ghafla alijikwaa na kuanguka Mungu wangu Irene akutikisa hata kiungo baada ya kuanguka alikua kimya kama bahati mabinti wawili waliokua wakienda kisimani walimuona mama mjamzito akiwa amelala chini kalowana mwili mzima haraka haraka walipiga kelele za kuomba msaada kwa watu waliokua Karibu wanaume kadhaa walijitokeza na kutoa msaada wa kumpeleka kwa mganga aliyekua karibu na kijiji hicho huko alimaliza siku saba bila kuamka ilikua kama kupima kifo au nusu kifo kabisa.Mjini nako Adam alifanyiwa mpango wa shule na paschal na alipelekwa shule ya msingi mwenge ili aanze shule .Pia Paschal alihakikisha Adam anapata mahitaji yote ya shule .Huko kijijini Irene akazinduka baada ya siku nyingi za kuzimia mhhhh Irene naye alizinduka kwa aina yake ilimshangaza mganga ila ndivyo ilivyokuwa Irene alinyanyuka haraka alipokua amelazwa kama anataka kukimbia huku akiita Adam Adam Adam sijui ni Kwa nini ila ni ndoto aliyoiota Irene kabla hajazinduka ndio ilimfanya awe hivyo.Irene aliota yupo na Adam msituni wamekaa pamoja wakicheza na kufurahi kama wapenzi Adam si akaanza kumuimbia nyimbo Irene kwa lugha ya kisukuma daaah kama nachi vile za wahindi sasa katika kucheza mara ghafla Adam alianguka kwenye shimo refu sana Irene aliogopa na kuanza kuita Adam Adam Adam huuuuhuu kumbe ilikua ndoto masikini Irene alishindwa kuvumilia kuonyesha huzuni yake kwa kumwaga chozi ilikua ni kilio kama cha mtoto achomwapo sindano anavyolia Irene alilia akikumbuka mambo aliyofanya na Adam na moyo mpweke alikua nao kwa sasa nani wakutuliza moyo huo mpweke hakuwepo basi ilibaki ni maumivu tu kwa Irene.Siku hiyo hiyo  ndio siku ambayo Irene alipata fahamu na baada ya siku tatu Irene aliruhisiwa na mganga Jedi kwenda nyumbani.Masomo Kwa Adam yalianza vizuri shuleni kama unavyojua bwana kijana mtanashati siku zote hakosi wa kumtaka handsome boy Adam kama alianza shule na bahati hivi kwanza alivyokua ameng'aa kwa sare zake zilizokua mpyaaa kabisa shati lake jeupe lililong'aa mithiri ya shati la tomato sasa hivi na kaptula yake ya kaki ndefu soksi nyeupe fupi na viatu vyeusi vilivyong'aa havikumzuia Adam kuonekana mtanashati na hicho ndicho kilichomfanya Dayness kujipendekeza kwa msafi Adam.Huko kijijini Irene sasa naye alipata bahati. Ni bahati ya kutaka kuolewa ni mzee Shabani aliyekua mfanyabiashara anapeleka mazao mjini alipenda amuoe Irene hii ilikua kama bahati kwa kuwa Irene hakuwa na jinsi sababu mimba hiyo aliwaza angekaa nayo hadi lini bila msaada wowote kweli mzee Shabani alipomwambia Irene hakusita kukubali haraka na kama unavyojua wazee wa zamani walikua hawazunguki kwenye kutongoza kwa kudanganya au kuhangaika sana kama vijana wa siku hizi wao kama mtu kampenda binti fulani anaenda kwao na kujitambulisha kisha atatoa mahali na kufanya taratibu zote we binti utashangaa tu unachukuliwa na kufanyiwa sherehe basi ndio ndoa yako hiyo.Ndivyo alivyofanya mzee Shabani na akamuoa Irene kama mke wake wa tatu.

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 3

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 3
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com
popote haraka bila kupoteza muda fundi akuchezea spana Adam akapandisha sketi ndefu ya Irene hadi mapajani kwake kisha si akashika ile nguo ya mwisho kuvuliwa kabla hajaivuta mshituko ghafla haaaa,Hahahaha sio ulichofikiria ndio Adam kilimshitua bali ni hodi iliyosikika nje ya mlango wa chumba kile Adam haraka haraka akamwachia Irene ambaye naye aliwahi kushusha sketi yake ikae vizuri ajisitiri .Adam kufungua tu mlango kumbe ni kaka yake ndio alikua anagonga
Adam: vp tena mapema hii kuna kitu ulisahau au, sababu umekuja bila taarifa yani ungejua hesabu ilivyokuwa imekubali nilikua namfundisha Irene magazijuto.
Jimmy: sasa mdogo Wangu hizo magazijuto gizani kuna kuelewa kweli au , mi leo shambani kazi zilikua chache ndio maana unaniona mapema nimekuja kupumzika.
Irene: Shikamoo kaka Jimmy
Jimmy: marahaba Irene habari za nyumbani
Irene: nzuri mi naenda (huku akiondoka)
Jimmy :nisalimie wote nyumbani
Irene : sawa
Nafasi ya pili hiyo Adam kaikosa na mipango yake imefeli. Walipokutana Adam na Irene walichekana sana wakikumbuka walichotaka kufanya .Mipango mipya ya Adam ilipangwa sasa hivi Adam alipania kweli kweli haya Mungu Hamtupi mja wake Irene mwenyewe kajileta hadi kwao Adam kisha akaingia hadi ndani mida hiyo wazazi wa Adam walikua shambani na ilikua siku ya mapumziko kwa Adam hakwenda shule hivyo aliachiwa nyumba achunge. Akiwa bado haamini haamini hivi mara Adam akasikia
Irene: Adam Adam(Adam bado kashangaa)
Adam: naam unaniita, mawazo haya mabaya sana.
Irene: we mtoto mdogo nawe uwaze nini sasa sikia tumalizie pale tulipoishia siku ile tukashindwa.
Adam: wapi tena mi nimeshasahau
Irene:si hapa bwana njoo uone. 

Mungu wangu Adam alishituka mapigo ya moyo yakaongezeka kwa kile alichokiona kwa Irene ni kifua kilichozungukwa na miduara mithiri ya vifuu vya nazi vimechomoza vigumu kama mianzi haaa kweli Mungu kaumba dunia na maajabu yake Adam hakusita kuhakikisha kama sio feki  kwa kuyashika taratibu kwa mikono miwili asalale ni miguno ya aina mbali mbali ilitoka kwa kupokezana kama sauti ya kinanda kilichotoa mziki laini kwa kuwa mnazi haumshindi mkwezi vya wazi vililiwa na nzi Adam alipasua mbaazi we maumivu yake kama ajali ila kwa kuwa utamu ulizidi asali hakuna aliyejali watu waliendelea kula ugali.Hayo yakaishia hapo ila mwisho wa furaha ni majuto Irene alipokuja kugundua kwamba tayari kapoteza heshima  alilia sana kwa kuwa aliogopa wazazi wake hasa mama yake kama angegundua kwamba kafungua mlango wazi kabla ya mgeni hajaingia kwani enzi hizo msichana aliolewa akiwa na heshima yake na Irene alikua tayari ashaipote huo ndio ulikua mwanzo wa kumchukia Adam hata salam kukawa hakuna tena na misukosuko ndio ukapamba moto kwa Irene hajui wapi aanzie kitu kimoja tu ndio kilimrudisha Irene kwa Adam nacho kilikua ni ujauzito aliougundua wiki tatu baadae .Mama yake Irene aligundua dalili mapema kuwa mwanae alikua na ujauzito hatua iliyochukuliwa ilikua ni kumfahamu baba wa mtoto ili familia ya Irene isiaibike.Adam alikalishwa katikati ya kikao cha wazazi kumuhoji na kumkabidhi mke kwa sababu wakati ule ukimpa mimba binti kabla ya ndoa ulikabidhiwa binti umuoe kwa lazima.Hicho ndicho alichoambiwa Adam na wazazi wa pande zote mbili aisee kwake lilikua swala gumu sana na Adam alivyokua akipenda shule hakuwa tayari kuiacha na kuanza maisha ya kuwa baba na kulima.Hivyo alipanga atoroke na kwenda mjini ili kuepukana na dhama hiyo aliyoileta. Jimmy ndiye aliyesuka mipango ya kumtorosha Adam usiku wa manane na kumpeleka mjini 

Thursday, September 24, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 2

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 2
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com


Adam:mhhh nani tena mapema yote hii (huku akificha shuka uvunguni)
Derick: ni mimi Derick numekupitia twende shule
Adam: Leo mbona mapema hivi au tuna zamu (akimfungulia Derick mlango)
Derick: mi nimeona bora tuwahi si unajua wiki hii zamu ya mwalimu mnoko anachapa kweli yule bora tumuwahi
Adam:sawa basi ngoja ninawe miguu na uso twende
Derick(akiwa amekaa kitandani ghafla) we Adam nini sasa hiki umefanya aisee mbona mlinzi ameenda mnara kiasi hicho.
Adam: Acha zako we hujui kama sasa hivi ni asubuhi ndio muda wake kwenda mnara.
Derick: ahahahaa ila sio kwa kiasi hicho au umeota ndoto pevu nini (huku akiangalia shuka lipo wapi) si akaliona uvunguni wacha amcheke akamwambia
Derick: Adam rafiki yangu umri wako unakwenda tafuta kipozeo angalia utakufa nacho.
Adam:Hahahaha hebu acha utani achana na hilo shuka nitafua baadae hebu toka mi ninawe.
Enzi hizo nyumba za tope sakafu mchanga kwa hiyo walikua wanaogea humo humo ndani. Adam alikwenda shule na saa ya kutoka haraka akawahi kumpitia Irene wakasome. Irene alimwambia Adam atangulie. Huko ghetto Adam amekaa anapanga mipango ya kuua ndege siku hiyo Irene si akafika Adam kachangamka anaona ng'ombe kaja mwenyewe machinjioni kumbe hakujua kama Irene alikuja na celine mtoto wa mwalimu mkuu wa shule anayosoma Adam .Na Celine kwa unoko hajambo mipango yote ya Adam ikafa sasa akafundisha ili mradi liende tu .Celine yeye alisingizia hajui hesabu kumbe anataka kujua Adam na Irene kama wana uhusiano na alifaulu kumdanganya Irene hadi wakaenda wote .Hiyo siku ikapita na Adam akafeli mipango yake mara ya pili sasa hapo akanuia kabisa kwamba lazima aue ndege siku hiyo mipango yake kidogo ifanikiwe alianza kwa kumshika paja Irene anamkazia kama alielewa alichofundishwa Irene mtoto wa kinyaturu Mungu alimzawadia weupe nyuma sasa kama palitengenezwa vile alikua na mizunguko kama tikiti maji kubwa limekatwa katikati,kifua sasa Adam ndio alidata zaidi ghafla si akamshika kiunoni haaa Irene akajiachia kabisa kuonyesha ishara ya kumpa uhuru Adam ashike popote haraka bila kupoteza muda fundi akuchezea spana Adam akapandisha sketi ndefu ya Irene hadi mapajani kwake kisha si akashika ile nguo ya mwisho kuvuliwa kabla hajaivuta mshituko ghafla haaaa

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com
                               
                                        SEHEMU YA KWANZA.
Yani siamini kama Martha dada na ndio namkosa hivi hivi na hiyo mimba huyo mtoto ataniita nani baba au mjomba.Haya maneno alijiuliza Vatican nje ya nyumbani kwao Martha huku machozi yakimtiririka huko ndani napo kila mtu kimya kilitawala Martha ndio kabisa alishindwa kuvumilia na kwenda kujifungia chumbani. Ilikua kama ndoto baada ya miaka 27 mzee Adam anakutana na bi Irene story inaanza hivi miaka 30 iliyopita ni furaha iliyoje kufika darasa la 5 baada ya kufanya mtihani wa darasa la 4 Adam amefaulu kwa maisha ya kijijini ukifika darasa la saba wewe unaheshimika sana na Adam alivyokua na akili we acha aliheshimika sana hadi kuletewa watoto awafundishe. Siku moja akiwa nyumbani mara hodi vuu haraka akanyanyuka Alikua akifuma mkeka wa makuti Shikamoo baba Irene alisalimia huku akisema baba na mama hawapo mzee Deogratius huku akicheka Hahaha sina shida nao mi nina shida na wewe huku akikaza mkono wake aliomshika Irene,
Adam: sasa mzee Deo kama hauna shida nao mi nikusaidie nini sasa kama kuoa mi bado mwanafunzi na Irene mwenyewe mtoto kwangu.
Mzee Deo: si hilo kwanza we bado hujawa mwanaume kamili vp kwani unaweza kusimamisha ndege acha utani Adam mi ninachotaka kusema ni kwamba dada yako huyu anafeli sana shuleni sasa wewe kwa kuwa una yaweza hebu mfundishe naye jamani nishachoka kumlipia ada ya darasa la nne wewe unafaulu ye anarudia mwaka wa pili sasa.
Adam:ha! kumbe hicho tu mzee hapa kafika we niachie hilo suala.
kwa kipindi hicho watu walisoma wakiwa na umri mkubwa Adam alikua na miaka 18 Irene naye ndio alikua anaibukia miaka 16. Sasa fisi kakabidhiwa bucha Adam kufundisha si ndio ikawa kufundishana Adam alitokea kumpenda Irene ila kumwambia ndio ilikua shughuli siku moja nyumbani akiwa anamfundisha Irene Adam akaanza
Adam:unajua Irene hizi hesabu za Kuzidisha ngumu sana( huku akimshika paja)
Irene: kweli ni ngumu ila hazifiki kwenye mapaja ya watu (Huku akiutoa mkono wa Adam mapajani kwake ) mi naona hesabu za leo zimenichanganya sana wacha niende kisimani na baadae nitakwenda mlimani kuchukua kuni nadhani leo jioni hatutasoma kazi nyingi sana nyumbani.
Adam(huku akinyanyuka) : we acha kujitesa mi nitakusindikiza nikusaidie ili umalize haraka au unasemaje
Irene:mhhhhh sawa basi nitakukuta hapa.
Kweli wakaenda hadi kisimani na Adam alijituma balaa kubeba maji na kupeleka kwao Irene mara tatu alipomaliza Irene alimuahidi watakutana jioni mlimani akamsaidie kukata kuni. Adam kumbe kakazana kuchota maji kwa ajili ya Irene kasahau kwao daah alichapwa fimbo sana na mama yake kisha babake naye alipo ambiwa tu na mama Adam zoezi la fimbo likaanza upya. Adam akapewa kazi mara mbili achote maji na kukata kuni. Huku akigumia maumivu akapita kwao Irene wakaenda mlimani kukata kuni. sasa huko Adam si akaanza kuongea
Adam : unajua Irene huu mlima unatisha usiwe unakuja huku peke yako hadi uwe na mwanaume wa kukusindikiza kama mimi sawa.
Irene : sawa
Adam: halafu unajua kuna kitu nataka kukwambia je utakubali
Irene:we sema tu
Adam : we sema kwanza utakubali
Irene: bwana we kama hutaki kusema basi (huku akijitwisha mzigo wa kuni)
Adam: ahaaaa subiri sasa niseme unajua Irene yani mimi Nilikua noana hivi tutafute sehemu nzuri ya kusomea pale nyumbani mama ananisumbua sana mara anitume kisimani wala hata sikufundishi vizuri
Irene: kweli kabisa unajua hadi leo hesabu za kuzidisha sijazielewa tafuta sehemu nzuri tuwe tunasomea.
Adam: basi sawa nitatafuta vp umemaliza twende.
Irene: mi nakungoja wewe tu. Adam alipofika nyumbani haraka akaenda kwa kaka yake aitwaye Jimmy aliyekua na chumba au gheto akamwomba awe anasomea hapo kweli akakubaliwa usiku wake Adam kalala mara akaanza kuota ndoto Yupo na Irene mlimani wamekaa wakila maembe na wakipeana maneno ya mahaba Irene hakukaa sana akaaga anawahi kupika na kisha akamkumbatia Adam daaah Adam mwili ulimsisimka ghafla akasikia anaitwa Adam we Adam amka twende shule sauti ya Derick ilimtoa Adam ndotoni ghafla kuangalia kwenye shuka alishachafua na mlinzi naye kishapandisha mnara.Derick akaita tena Adam                     Adam:mhhh nani tena mapema yote hii (huku akificha shuka uvunguni)