SIRI HUFICHULIWA NA
MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 6
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO:
0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.comKilichoendelea humo mi na we hatukifahamu labda hiki kilichokua kinataka kuendelea kwa Adam , siku hiyo bwana Adam kipindi anatoka shule Dayness aling'ang'ania kwamba ampeleke Adam akapaone kwao Adam naye akasitasita mara aliposhikwa mkono tu na Dayness kwani alisema chochote huyoooo akawa mlaini wakaenda wote. Dah kwao Irene kwa kitajiri sana ona mazingira ya nje na ndani yalivyokua mazuri alijisemea Adam akiwa amekaa sebuleni anashangaa TV ya Sony black & white yani isiyo na rangi mara Dayness si huyo kapita mara kaenda jikoni mara chooni mara bafuni mwishowe ikawa kero sasa kumbe yeye yupo kwenye show kumteka akili Adam ili amtamani mara akamletea soda ya fanta kipindi kile zipo kwenye chupa kubwa sana kama ya kupimia mafuta ya kura fanta sa hivi duuuu Adam akashangaa kweli kweli , sawa maisha haya alishaanza kuyazoea alipokua kwa Paschal ila leo kwa Dayness daaaaaaah Adam alishangaaa sana na kwa bahati nzuri au mbaya siku hiyo wazazi wa Dayness hawakuwepo nyumbani walikwenda kwenye harusi hivyo wangerudi usiku sana sasa lindo halina mlinzi nafasi kwa wezi kuchukua vya wazi. Kabla hata hajamaliza soda tayari Dayness mara kakaa juu ya kiti mara kapanda juu ya meza na sketi yake fupi ya shule Adam alikua anaona kabati wazi wazi mamaaaaaaaa sasa hili jaribio la mwisho ndio lilikua kali zaidi baada ya Adam kuepuka majaribio yote haya Dayness si akaaga kama anakwenda kuoga ghafla kajimwagia maji tu haraka haraka akatoka mamamamamamama kanga ilivyokua imemshika kisha akapita sebuleni hapo hapo alipokua Adam na ghafla Kama jadi ya Adam hua aachii nafasi wazi kama hizo pole pole akamvuta Dayness hadi karibu na Kochi alipokua amekaa akamsukuma kwa nguvu hadi akalala chali kwenye kochi na kwa vile alikua kavaa kanga moja haikua kazi ngumu kwa Adam kutoa nuksi daaaah mtendwa katendewa tendo lililotendeka katika amri kumi za Mungu moja ikavunjika siku hiyo . Vatican naye ndio huyo anaiona ona dunia malezi mazuri ,ulinzi afya na chakula bora vyote alivipata hivyo alikua mtoto mwenye afya mnene si mchezo. Baada ya Adam kumfukuza mchawi sasa rasmi alitangaza mahusiano sasa hivi ilikua rahiiiiiisi kweli wala hata hakuhangaika na ndio ulikua mara ya kwanza kwa Adam kutongoza na kumtamkia msichana kwamba anampenda na alitamka kwa Dayness. Miaka ikasonga sasa na Adam akafanikiwa kufaulu darasa la saba na kujiunga na kidato cha kwanza shule ya Mwanza sekondari. Kwa bahati mbaya Dayness yeye mambo kwake yalimuendea kombo hakupata nafasi ya kwenda kidato cha kwanza hivyo akawa mama wa nyumbani tu ila mapenzi yao na Adam hayakuisha.Irene naye sasa aliamua kulivalia njuga swala la yeye kurudi shule basi mzee shabani baada ya kuona usumbufu sana alimrudisha Irene shule na alianza darasa la nne, shule kwake ilikua changamoto kwa kuwa tayari alikua ni mama hivyo alikua na majukumu mawili na muda mwingine alipokua shule alikua anamuwaza mwanae nyumbani.Miaka ilisogea Vatican naye akazidi kukua na sasa mama yake alihitimu darasa la saba na kufanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza ila sasa shule aliyochaguliwa ilikua ile ile anayosoma Adam na Adam kwa kipindi hicho alikua tayari kafika kidato cha nne. Kweli taratibu zilifanywa na mzee Shaban kuhakikisha mke wake anakwenda mjini kusoma ila Vatican ndio ivyo alikua anaachwa mpweke bila ya mama ambaye ndio alikua kila kitu kwake ila kwa sasa umri wake ulikaribia aanze shule ya msingi kwani tayari alikua na miaka sita hivyo haikua tatizo sana kwake kuachwa na mama bali upweke kwa kuwa alimzoea sana mama yake kuliko mtu mwingine katika familia ya mzee shaban si mama zake wengine yani wake wa mzee shaban au hata ndugu zake watoto wa mzee shaban.Irene leo ndio ilikua safari yake kwenda kuanza shule mjini Mwanza aliwaaga ndugu jamaa na marafiki na kwenda.Alifika salama na alitakiwa kuripoti shule siku hiyo hiyo ili apewe chumba chake kwa kuwa yeye alitakiwa kulala hapo shule yan boarding.Adam sasa alizidi yani alimgeuza Dayness mke kabisa yani ilikua kazi na dawa hatimaye Dayness akapata ujauzito
0 comments:
Post a Comment