Friday, September 25, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 4

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 4
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Jimmy ndiye aliyesuka mipango ya kumtorosha Adam usiku wa manane na kumpeleka mjini .walikwenda kwa miguu hadi wakafika pasiansi Mwanza kutoka kwao kijijini Kayenze nyafura.Jimmy alimuaga Adam ili arudi nyumbani na kumwachia shillingi ishirini kama ya kutumia akiwa mjini. Huku kijijini napo kesho yake wanagundua kwamba Adam hayupo ndani ya kijiji kile kwamba alishatoroka baba yake Irene alimgawia Irene urithi wake kwa kumpa kiwanja ,shamba , na mtoto wang'ombe mdogo ili aaanze maisha kisha akamfukuza na kusema hamtambui kama mtoto wake sio yeye tu bali kijiji kizima kilimtenga na ukoo wake pia allionekana kaiaibisha jamii hiyo nzima na pigo kubwa la mwisho Irene alifukuzwa shule alijuta kwa nini alinasa katika mapenzi na Adam aliyemtelekeza. Sasa alikua na kazi mbili moja ni kuhakikisha anapata chakula na pili kutunza ujauzito wake na kupata mahali pa kulala.Siku moja Irene akiwa kisimani mara akasikia vicheko'' hehehehheeee ndege mjanja kanaswa kwenye tundu bovu kumbe ndio wanayosoma shule hayo'' alikua ni Magreth na Rachel kiukweli ilimuuma sana akikumbuka kisha ye mwenyewe akaanza kuwaza moyoni akijisemea ''yani ilikua mara moja tu tena mara ya kwanza hii mimba imetokea wapi'' hakujua jibu lake kwani hakuna na elimu ya uzazi. Adam naye huko mjini alianza maisha mapya ya kuishi mitaani pesa aliyopewa na kaka yake sasa ilikwisha uwezekano wa kula ukapungua hapo ndipo Adam alipoamua kuanza kuosha magari na kufanya vibarua ili apate chochote tumboni. Wote wawili Irene na Adam waliishi maisha ya tabu hadi walikumbuka nyumbani walipopata ugali wa bure kila siku ila walikua walishamwaga ugali na familia zao zikamwaga mboga.Kama bahati nzuri akiwa mjini Adam alipata ahueni ni kama bahati Adam alikutana na Paschal mtoto wa mzee Wamichongo aliyekua jirani yao na Adam huku kijijini.Paschal alikutana ma Adam car wash alipopeleka kuosha gari lake alishangaa kumuona Adam mjini ila kitu cha kwanza ilibidi ampeleke nyumbani kisha baada ya kupata chakula paschal akamuuliza Adam:-
 Paschal: ehehe habari za nyumbani Adam                                                                              Adam: kwa kweli ni salama kwao ila sio kwangu.
Paschal: unamaanisha nini
Adam: mimi kaka nyumbani nilitoroka nilipata matatizo
Paschal: matatizo gani mdogo wangu.
Adam: kaka nilimpa mimba Irene wazazi wakanilazimisha nimuoe na niache shule ili nilime nimtunze na mimi ninapenda sana shule nikaamua kukimbilia mjini huku ili nisome.
Paschal: pole sana mdogo wangu hapa sasa umefika nyumbani hapa utasoma vizuri tu ila nisingependa urudie kosa ulilolifanya kijijini.
Adam: ahsante kaka naahidi sitarudia kosa la kumpa mimba binti yoyote .
Paschal: sawa mdogo wangu pumzika kesho tutaona mpango wa shule.
Adam: ahsante kaka usiku mwema.
Paschal : nawe pia usiku mwema Adam.
Paschal alikua anafanya kazi benki kama bank teller wa benki ya posta hivyo pesa haikua tatizo kwake naye pia alitorokea mjini zamani na kuja mjini kama Adam.Irene aliendelea kupata shida na matatizo kila kukicha alikwenda mbali kuchota maji , kujipikia kukata kuni na kulima na kuitunza mimba yake siku moja alipokwenda kisimani Irene alikua kabeba ndoo nzito ya maji alipofika kwenye mpando ghafla alijikwaa na kuanguka Mungu wangu Irene akutikisa hata kiungo baada ya kuanguka alikua kimya kama bahati mabinti wawili waliokua wakienda kisimani walimuona mama mjamzito akiwa amelala chini kalowana mwili mzima haraka haraka walipiga kelele za kuomba msaada kwa watu waliokua Karibu wanaume kadhaa walijitokeza na kutoa msaada wa kumpeleka kwa mganga aliyekua karibu na kijiji hicho huko alimaliza siku saba bila kuamka ilikua kama kupima kifo au nusu kifo kabisa.Mjini nako Adam alifanyiwa mpango wa shule na paschal na alipelekwa shule ya msingi mwenge ili aanze shule .Pia Paschal alihakikisha Adam anapata mahitaji yote ya shule .Huko kijijini Irene akazinduka baada ya siku nyingi za kuzimia mhhhh Irene naye alizinduka kwa aina yake ilimshangaza mganga ila ndivyo ilivyokuwa Irene alinyanyuka haraka alipokua amelazwa kama anataka kukimbia huku akiita Adam Adam Adam sijui ni Kwa nini ila ni ndoto aliyoiota Irene kabla hajazinduka ndio ilimfanya awe hivyo.Irene aliota yupo na Adam msituni wamekaa pamoja wakicheza na kufurahi kama wapenzi Adam si akaanza kumuimbia nyimbo Irene kwa lugha ya kisukuma daaah kama nachi vile za wahindi sasa katika kucheza mara ghafla Adam alianguka kwenye shimo refu sana Irene aliogopa na kuanza kuita Adam Adam Adam huuuuhuu kumbe ilikua ndoto masikini Irene alishindwa kuvumilia kuonyesha huzuni yake kwa kumwaga chozi ilikua ni kilio kama cha mtoto achomwapo sindano anavyolia Irene alilia akikumbuka mambo aliyofanya na Adam na moyo mpweke alikua nao kwa sasa nani wakutuliza moyo huo mpweke hakuwepo basi ilibaki ni maumivu tu kwa Irene.Siku hiyo hiyo  ndio siku ambayo Irene alipata fahamu na baada ya siku tatu Irene aliruhisiwa na mganga Jedi kwenda nyumbani.Masomo Kwa Adam yalianza vizuri shuleni kama unavyojua bwana kijana mtanashati siku zote hakosi wa kumtaka handsome boy Adam kama alianza shule na bahati hivi kwanza alivyokua ameng'aa kwa sare zake zilizokua mpyaaa kabisa shati lake jeupe lililong'aa mithiri ya shati la tomato sasa hivi na kaptula yake ya kaki ndefu soksi nyeupe fupi na viatu vyeusi vilivyong'aa havikumzuia Adam kuonekana mtanashati na hicho ndicho kilichomfanya Dayness kujipendekeza kwa msafi Adam.Huko kijijini Irene sasa naye alipata bahati. Ni bahati ya kutaka kuolewa ni mzee Shabani aliyekua mfanyabiashara anapeleka mazao mjini alipenda amuoe Irene hii ilikua kama bahati kwa kuwa Irene hakuwa na jinsi sababu mimba hiyo aliwaza angekaa nayo hadi lini bila msaada wowote kweli mzee Shabani alipomwambia Irene hakusita kukubali haraka na kama unavyojua wazee wa zamani walikua hawazunguki kwenye kutongoza kwa kudanganya au kuhangaika sana kama vijana wa siku hizi wao kama mtu kampenda binti fulani anaenda kwao na kujitambulisha kisha atatoa mahali na kufanya taratibu zote we binti utashangaa tu unachukuliwa na kufanyiwa sherehe basi ndio ndoa yako hiyo.Ndivyo alivyofanya mzee Shabani na akamuoa Irene kama mke wake wa tatu.

0 comments:

Post a Comment