SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 7
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.comAdam sasa alizidi yani alimgeuza Dayness mke kabisa yani ilikua kazi na dawa hatimaye Dayness akapata ujauzito.Siku ya kwanza shule ndio hii kwa Irene na alipokua kwenye mstari mara ghafla. Wapeni wali wao waulao wale. Hahahaha
sio ulichofikiria bali Irene alimwona mwalimu mnubi aliyemfundisha shule ya msingi na akaenda mjini kusoma sasa alikua ni mwalimu wa sekondari Irene alishangaa kumwona kwani ilikua ni muda tangu waonane hiyo ilimpa furaha kwani alipata mwenyeji mjini na asingesumbuka sana kuizoea shule na kizuri zaidi alikua ndio mwalimu wake wa darasa sasa kibaya kilikua ni hiki mwalimu huyu alikua anampenda Irene tangu zamani shule ya msingi na alishawahi kumshawishi afanye mapenzi naye zamani sasa hiyo ilikua changamoto kwake ila hakusita kuionyesha furaha yake hivi
Irene: mwalimu Mnubi jamani Shikamoo
mwalimu
Mwl.Mnubi (huku akitaka kumpotezea)
marahaba panga mstari vizuri haa nani
Irene marahaba za siku
Irene: nzuri mwalimu za mjini
Mwl.Mnubi: nzuri Karibu mjini Karibu sana
Irene: Ahsante mwalimu
Mwl.Mnubi: sawa upo darasa gani
Irene: form one B
Mwl.Mnubi: haya ntakutafuta (huku akiamlisha mguu pande mguu sawa) Shule haikua tabu sana kwake Irene kwa kuwa alipata kila alichokihitaji na mzee Shaban alihakikisha anampa matumizi Irene kwa muda muafaka ila huwezi amini Irene hakuwahi kukutana kabisa na Adam kwani Mwanza sekondari ilikua shule kubwa sana iliyokua na wanafunzi zaidi ya elfu tatu hivyo wanafunzi waliingia kwa zamu asubuhi na jioni hivyo kidato cha nne wakiingia saa 1 asubuhi basi cha kwanza waliingia mchana saa 6 hivyo ilikua ngumu kwa wawili hao kukutana hadi Adam akamaliza hapo kidato cha nne.Irene yeye aliendelea na masomo yake.Adam aliukubali ujauzito wa Dayness kwani alimpenda kweli na muda wa kujifungua nao ndio huo ulikaribia sasa kituko ni kwamba Dayness alifukuzwa kwao baada ya ujauzito kujulikana na sasa aliishi na Adam pamoja na paschal ila Paschal alichukia basi tu hakutaka kuonyesha hasira zake kwa Adam. Mwalimu mnubi naye aliona ndio muda muafaka wa cheo kutumika vibaya kwa Irene ni pale mwalimu Mnubi alipo muomba penzi Irene tena na sasa alimtishia kumfelisha kama asingekubali jamani jamani yalikua maamuzi magumu kwa Irene kufanya na alipewa siku tatu tu kufanya maamuzi hayo Kweli Irene alifikiria na hiki ndicho alicho mjibu mwalimuMnubi. Maamuzi ya kupanda mnazi hufanywa namkwezi muuza mbaazi kakupa mashuzi.Hayo yalikua magumu maamuzi ila Irene alipofiri na kuona mbali hiki ndicho alifanya
0 comments:
Post a Comment