Sunday, September 27, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 5

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 5
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Ndivyo alivyofanya mzee Shabani na akamuoa Irene kama mke wake wa tatu. Kuolewa kwa Irene kulimrudishia heshima yake sana kijijini hapo watu walianza kumuheshimu na kumuona mama mwenye ndoa yake hata baba yake pia alirudisha mapenzi yake kwa mwanae na kumpa onyo kwamba hata siku moja asije akajaribu kurudiana tena na Adam hata kama akirudi kijijini hapo.Maisha yalimwendea vizuri sana Irene na alipendwa sana na jamii nzima nzima iliyomzunguka miezi tisa ya furaha Irene alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume jina lakeVatican kwa kuwa siku anajifungua alipata uchungu karibu na kanisani na ma sister wamissionari ndio waliomsaidia kujifungua hivyo wakampa jina Vatican yani mtakatifu aliyezaliwa kanisani.Adam masomo kwake yalikua kama mtelezo alijijengea uaminifu kwa Paschal kwamba kweli hatorudia kosa kama la kijijini kumbe wapi alificha makucha tayari alikua naye ameshampenda Dayness aliekua anajipendekeza kwake.Sema tu Adam kwenye kuongea yeye alikua mwoga kazi yake yeye alikua mtu wa matendo kama alivyofanya kwa Irene . Masomo kwa Adam aliyapa umuhimu sana kipindi hiki labda ni kwa sababu sasa alikua mtu mzima kwani tayari Adam alikua na umri wa miaka 19. Umri huo ulimtosha kupambanua mengi na kuelewa mengi zaidi, kijijini napo nderemo na vifijo vya hongera vilitawala pale Vatican alipoiona dunia kuzaliwa kwake kulileta mabadiliko mapya katika maisha ya Irene sasa Irene alikua mpya mwenye furaha na huru kwani sasa hakufungwa na mimba tena kama zamani hivyo alidhani angepata muda wa kusoma baadae kwa kuwa alipenda sana shule na alijua umuhimu wa shule katika maisha yake kwani alishaona jamii jinsi ilivyomtenga mwanzoni hivyo msaada wake pekee ulikua elimu .Irene alijaribu kumshawishi mume wake wa sasa mzee Shaban kuhusu masomo ilikua hivi siku hiyo mzee Shaban alikwenda kumtembelea Irene kwenye chumba chake kwa kuwa yeye alikua na wake watatu hivyo kila mwanamke alikua na zamu yake kulala kwake katika wiki siku mbili na siku hiyo ilikua zamu ya mzee Shaban kulala kwa Irene wakati wakiwa kitandani Irene akaanza
Irene:mmhhmhhhhmhhh (akijikoholesha) unajua baba Vatican unaonaje mi nikirudia shule nisome kidogo
Mzee Shaban: hapana hapana kabisa kwa hilo wala hata sitaki kulisikia unataka urudishe mambo kama yaliyokupata mwanzo huko shule hakuna faida sipendi kabisa urudi tena shule yani ukapewe mimba nyingine mi nije nileee heeee ndo unataka hivyo au sababu mi nimezeeka ndio unanidharau.
Irene: sio hivyo baba Adam jamani mi nakuheshimu sana hayo yametokea wapi tena mi niliomba tu kama ingewezekana nikarudi shule na wala siwezi kurudia makosa ya zamani naapa kwa Mungu huo ulikua utoto tu kwanza we nani kasema mzee ng'ombe tangu lini azeeke maini .
Mzee Shaban: si ndio hapo nilitaka kushangaa mke wangu tena mambo gani hayo ananiletea sasa
Irene: mhhhhhhhhhhhh
mzee Shaban : we mwenyewe umelitambua hilo kwamba ng'ombe hazeeki maini sogea basi karibu tuwaumize wachawi.
irene: mhhhhhhhh we mzee nawe nilijua tu shida yako nini yani umezunguka kumbe shida yako ndogo tu wazee bwana waoga kweli kusema ila jamani hata sijapona vizuri.
Mzee Shaban: haaaa hivyo hivyo kwanza si kidogo tu utaponea huko huko bwana hebu njoo(huku akijifunika shuka) .                                                                                       Kilichoendelea humo mi na we hatukifahamu labda hiki kilichokua kinataka kuendelea kwa Adam

0 comments:

Post a Comment