SIRI HUFICHULIWA NA
MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 9
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO:
0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.comMafanikio kwa Irene kama mama mpambanaji yalianza kujitokeza kwani Irene alitangazwa rasmi kuwa mwalimu mkuu wa kitangiri shule ya msingi aisee ilikua ni hatua kubwa sana kwa Irene ambae alikua bado binti sana kupata nafasi hiyo ila ndio bahati yake hiyo.Siku moja akiwa benki ya posta anachukua mishahara ya walimu sababu wakati ule walimu walilipwa pesa mkononi na mwalimu mkuu ndiye aliyekua anazifuata pesa benki na kisha kuja kugawa kwa walimu .Alipofika benki katika foleni kumbe siku hiyo Adam alikuja kumsalimia Paschal na kumshukuru kwa yote Irene alibahatika kumuona kwanza Adam baada ya miaka zaidi ya minane ya kutoonana ila maamuzi aliyochukua yalikua magumu sana aliondoka haraka pale benki ghafla tu alipomwona Adam alikua mwenye haraka tena kwa mwendo wa kukumbia nusura aanguke ila akajikwaa tu alikimbia hadi sehemu palipokua hakuna watu na kuanza kulia maskini ni machungu yote aliyoyakumbuka na shida zote alizopitia ila kwa kuwa alikua jasiri alijikaza sana na kuapa hata itokee nini kamwe asingeweza kumsamehe Adam na kusahau mateso aliyoyapata wala hatojaribu kumuonyesha mtoto wake aliyehangaika kumlea mwenyewe bila baba . Katika mizunguko ya hapa na pale Adam akiwa anatoka kazini aliwasha gari yake na kwenda nyumbani ghafla mbele yake mtoto wa shule aliyevuka haraka sana bila kuangalia vizuri barabarani alijikuta tayari amejaa kwenye kioo chake puuuuuuuuuuh mamaaaaaaaaaaaaaa! ndio sauti ya kilio cha msaada ilisikika alikua ni Vatican aliyesukumwa ghafla na rafiki yake Kelvin avuke barabara ayayayayayaya aisee ilikua kama ni ziwa la damu pale chini alipoanguka Vatican kwa haraka haraka Adam aliomba msaada na kumuwahisha haraka Vatican hospitali huko Adam akutulia mara asimame mara ajingate kucha ajipige mwenyewe ilimradi kutoa hofu tu ya kwamba mtoto yule akupoteza maisha kweli hali ya vatican ilikua nzuri sema alichanika kwenye mkono ndio maana alitoa damu nyingi sana ila alifanyiwa matibabu na akawa sawa sasa juhudi za kuwasiliana na mzazi wa Vatican zilifanyika. Irene haraka alipopata taarifa alikwenda hospitali, Dokta vp anaendeleaje, ahaaaa afadhali kidogo hakupata maumivu sana zaidi ni jeraha la mkononi tena halitachukua muda kupona ni dogo sana sasa hivi tumemuacha apumzike kidogo na baadae tutampima tena na kumruhusu kwenda kupumzika nyumbani, basi mi natoka kidogo kwenda kupiga simu kuwajulisha familia yangu kuwa nipo hospitali , sawa. Hayo yalikua ni mazungumzo ya Adam na na daktari wa hospitali ya sekoutoure .Adam alitoka kuwasiliana na Dayness kumjulisha yaliyomkuta vuuuuu akavuta antena ya simu yake kubwa mfano wa mche wa sabuni ya kipande cha mia tano na ukubwa kama sabuni za kigoma hahahahahaha ilikua ni phillips moja kubwa sana mara akapiga griiiim griiiiim ring ring
Adam: haloo haloo haloo
Dayness: halooo naongea na nani hapa ni nyumbani kw Adam.
Adam : haloo Dayness ni mimi Adam baba Martha habari ya hapo nyumbani.
Dayness: baba Martha afadhali umepiga simu nimekusubiri sana nyumbani ila hukuja ni Martha ameshanisumbua tangu asubuhi analia tu sasa sijui tatizo ni nini
Adam (huku akiondoka) : haya nakuja sasa hivi. Adam alisahau hata kumuaga Vatican na aliondoka akiwa na haraka sana kwenda kuona yaliyojiri nyumbani kwake.Sasa mwalimu Irene ndio alikua anafika haraka baada ya kupata taarifa kuwa mwanae alipata ajali ila kwa bahati mbaya Adam alikua tayari amekwisha kuondoka hivyo alichofanya Irene ni kumchukua mwanae baada ya kuruhusiwa kutoka.Baaadae Adam aliporudi hospitali kutoka nyumbani alipokwenda ghafla alikuta tayari Vatican alishatoka na hayupo mazingira yale basi akaona kama ndio kaepushiwa kesi naa kuondoka.
0 comments:
Post a Comment