Thursday, October 15, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 24

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
SEHEMU YA 24

Martha mi sitakufanya chochote ila naomba uniambie ukweli wote , iiiiii huku akilia Martha alisema Baba naomba unisamehe sana kweli mi nina ujauzito wa miezi miwili , vipi baba wa mtoto unamjua , ndio namjua baba, sasa naomba tufanye hivi naomba umwite baba wa mtoto tuje tuonane naye ili tumuulize kama atakubali kuwa mtoto wake maana vijana wa siku hizi tabia zao kukataa ujauzito, haya baba nitamtafuta na kumwambia. Kweli Martha alimpigia simu Vatican na kumwambia haloo , halo mpenzi Martha mambo , poa za kwako , ni nzuri tu vipi tena mpenzi wangu unataka tutoke out kesho au, hapana sio hivyo , sasa ni vipi , Vatican naomba unisikilize kwa makini sana hiki ninachotaka kukwambia , kipi tena Martha mbona unataka kunishitua au umefaulu mtihani wa form four , hapana sio hivyo bali hiki ni kitu muhimu sana kwa kweli nilishindwa kukwambia ila naona ni muda muafaka kusema ukweli tu , ukweli upi tena mbona unazidi kunichanganya sana mpenzi wangu , sio nakuchanganya ukweli ni kwamba mimi nina ujauzito tena wa miezi miwili, aaaaah wa kwangu au , ndio wa kwako , weweeeeeee weweeeeeee natamani hata ningekua karibu hapo nikakukumbatie balaa aisee Martha ahsante ahsante sana sana sana siamini kama naenda kuwa baba ahsante , we mbona umeshangilia hivyo , nimefurahi sana mpenzi wangu kuniletea mtoto , we unaona raha eeh je mimi ninavyoumia , aaah basi pole pole mpenzi wangu najua ujauzito unaumiza ila jikaze nipo pamoja nawe, ahsante halafu kuna kitu nataka kukwambia tena lipi tena hilo mimba imetoka au , bora hata lingekua hilo , bora , ndio hivyo bora sababu hili ndio baya yani baba anahitaji kukuona , nini , hujasikia baba anataka kukuona , baba yako Martha acha utani wewe , utani ndio ukweli wenyewe , sasa nakwendaje na lini , hahahaha ulishaogopa kukutana na baba mkwe ndio utakoma sijui utaongea nini , duu hayo hayo nitakayoongea , hahahahahaha hapo kiroho kimeshakudunda , mmh kweli , sasa kesho uje nyumbani najua hupajui hivyo nitakuelekeza ufike sawa , sawa. Basi Vatican hakusita kuonyesha furaha yake kwa kumwambia ukweli mama yake ila kama unavyojua wakinamama hua hawakubali hivi hivi Irene alikasirika kidogo kisha kwa kuwa mtoto mwenyewe mmoja hakuwa na cha kupingana naye lakini aliamua kumwambia mwanae Vatican waende wote ili naye akamuone mkwe wake na wazazi wenzake kweli siku ilipofika Vatican na mama yake walielekezwa na Martha na kufika kwao Martha.Hodi humu hodi mpaka ndani karibu karibuni sana ndivyo Vatican na Mama yake walivyokaribishwa na Martha huku ndani mzee Adam alikua kapumzika chumbani kwake kisha kauli ya Martha ndio ilimshitusha Vatican , jamani karibuni sana waaao mwalimu Irene siamini kama ni wewe shikamoo , marahaba eehee za wapi tena siku hizi , za hapa hapa mwanza mi ndio nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na sasa nipo nyumbani nasubiri majibu , Irene huku akimkejeli Martha na kumshika tumboni akasema majibu yenyewe ndio haya ya kutanguliza tumbo mbele , eeeh ndio hayo au , aaah hili tumbo ni majibu ya huyo kijana uliyekuja nae vipi mnafahamiana, kufahamiana! huyu mtoto wangu wa kuzaa tufahamiane vipi tena , kumbe mwanao sikujua kama mwalimu Irene mwanao ndio atakuja kuwa na mimi , ndio utegemee sasa , basi tuachane na hayo karibuni sana sijui mtapendelea kinywaji kipi kuna maji ,soda, soda kubwa au maziwa, chochote mimi natumia kasoro hiyo soda kubwa labda huyo baba mtoto wako ndio umuulize , aaaah huyu najua , Vatican akadakia , nakunywa nini , siri yangu we subiri haya ngoja niwaletee nikamwamshe na baba alikua kapumzika kidogo ndani si unajua leo weekend haendi kazini hivyo nipo naye nyumbani tu . Martha aliondoka na kuwafuatia vinywaji huku Irene na Vatican wakawa wanaongea we huyu binti umempata wapi , aaah mama tulikutana naye Dar , anhaaa ndio uliyokwenda kusoma Dar hayo ya kuwapa mimba watoto wa watu , aaaah mama nawe mambo gani tena hayo mimi si nilienda chuo kabisa , sasa si ndio mliyofundishwa haya kumbe ndio maana mtoto shida zilikua haziishi mara oooh mama nataka laki tatu ya dom mara kuna mchango wa mlango mara aisee kumbe huyu ndio alikua amekuteka akili na kwa taarifa yako huyu unakaa naye kwako mwenyewe na mimba unalea mwenyewe sio kwangu mi sitoi misaada , mama mbona umefika mbali hivyo nimeshakwambia ni bahati mbaya tu hiyo wala hata yeye alikua hajui kama ana ujauzito hadi alipoenda hospitali sasa kama we unanitenga sa hivi mi nifanyeje basi acha mi niondoe usumbufu kwa kujiua tu sasa sina jinsi mi nitamleaje huyo hata kwangu tu sina, aaaa basi basi mwanangu nawe hutaniwi usihofu mi nipo nawe pamoja ngoja tuwasubiri tuone wataamua nini eehehee tena hawa hapo wanakuja. Ni Martha alileta vinywaji na mzee Adam alifika na kuketi ,Vatican alimsalimia kwa uoga sana ila alishangazwa na mapokeo ya mama yake kwa mzee Adam ghafla Irene alishituka badala ya kumpa salamu Adam alimshangaa kisha akamuita mara tatu Adam , Adam , Adam , naye akaitikia naaam , huyu ni binti yako , ndio ni binti yangu mtoto pekee aliyeachwa na marehemu mke wangu Dayness Mungu ailaze pema roho yake , Irene aliongea kwa sauti kubwa na ya mshangao Mungu wangu , Adam akajibu nini ? Tumekwisha tumekwisha tumekwisha Adam , tumekwisha , kuhusu nini Irene mbona sikuelewi , Adam haya yote uliyataka wewe usingenitelekeza peke yangu na ujauzito wako kijijini ona sasa umewaoanisha kaka na dada bila kujua laana laana hizo Adam huyu hapa (huku akimshika Vatican) ni mwanangu Vatican ambaye pia ni mwanao ulienitelekeza nikiwa na mimba yake kijijini nimemlea mwenyewe hadi akakua hamjui baba yake kisha wewe unanichanganya kwa kuniambia eti Martha ni mtoto wako kumaanisha na Vatican ni mwanao pia hivyo Martha ni dada yake na Vatican mbona kasheshe hili jamani. Aliposema hayo kila mtu Martha na Vatican wakaanza kulia huku wakiwa na wazazi wao wakiwangangania wawathibitishie kuwa hilo jambo lilikua si la ukweli bali ni mbinu za kuwatenganisha, alianza Martha akimtikisa baba na kusema baba baba tell me what she is saying is not true please niambie baba kama mmepanga njama ya kututenganisha please baba please niambie Adam hakusema kitu chochote kwa mwanae Martha bali kimya ndio kilitawala. Vatican naye akamuuliza mama yake , mama huyu ndio baba yangu uliyekua unaniambia au , ndio mwenyewe baba yako kabisa mzazi mzee Adam kwani we kipindi unakutana na mpenzi wako sorry dada yako hukutaka kujua kwao wala wazazi wake nyie vijana wa siku hizi bwana mkikutana tu huko mnakokutania mkatongozana basi ndio imetoka hutaki hata kujua kwao na wazazi wake , aaah mama sio hivyo hata kama ningewajua wazazi wake ningejuaje kama baba yake ni baba yangu kama hukuniambia , basi ndio hivyo imeshatokea na huyu ni dada yako, mama mimi siamini kabisa Vaticani alitoka na kwenda nje huko akaanza kujisemea Yani siamini kama Martha dada na ndio namkosa hivi hivi na hiyo mimba huyo mtoto ataniita nani
baba au mjomba haya maneno alijiuliza Vatican nje ya nyumbani kwao Martha huku machozi yakimtiririka huko ndani napo kila mtu kimya kilitawala Martha ndio kabisa alishindwa kuvumilia na kwenda kujifungia chumbani. Huko chumbani Martha alichukua shuka lake la kujifunika na kulifunga kwenye feni iliyokua juu ya chumba chake kisha akajifunga shingoni na taratibu akajinyonga hadi kufa mzee Adam alipoona kimya alikwenda kwenye chumba cha Martha na alipofungua mlango akakuta umefungwa Adam aliuvunja na kuingia kisha hakuamini alichokiona Martha akiwa amenin'ginia kwenye feni kwa juu kajinyonga kwa shuka Adam alipiga kelele za kilio cha uchungu hadi Irene na Vatican wakakimbia kwenda huko mama yangu Vatican alipo uona mwili wa Martha akiwa amekufa alilia sana na kutoka nje Adam aliishiwa nguvu na kwa mshituko alidondoka chini na kupoteza maisha Vatican na mama yake Irene walibaki peke yao wakiwa na majonzi ya kupoteza wapendwa wao bila kujua hatima yao ya maisha.

KWELI SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
KIJANA POPOTE ULIPO PINDI UNAPOMPA MIMBA BINTI YOYOTE HATA KAMA UNAHISI SIO YA KWAKO TAFADHALI USIIKATAE WALA KUMTELEKEZA MAMA MJAMZITO NA KUANZA MAISHA YAKO BINAFSI BALI MJALI NA KUBALI KILA KITU KWANI HUWEZI KUJUA UKIFANYA HIVYO BAADAE MATATIZO KAMA HAYA YA KWENYE TAMTHILIA HII YANAWEZA KUKUPATA NA CHUNGA SANA KWANI SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.

Tuesday, October 13, 2015

SIRI HUFICHILIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 23

Siri hufichuliwa na mjasiri woga ikikithiri
sehemu 23

Dayness alichukua sumu ya unga ya panya na kuchanganya na juisi aliyokua nayo kisha akainywa haikuchukua muda kufanya kazi Dayness aligaagaa huku na kule akihangaika chini kwa muda kisha akatoa povu jeupe mdomoni na kukata roho maskini Dayness alijiua. Ilikua huzuni majonzi na vilio kwa familia ya Mzee Adam ndugu jamaa na marafiki wa karibu taratibu zote za mazishi zilifuatwa Dayness alizikwa . Irene alipata taarifa za msiba ila hakuhudhuria kwani alijua kuwa maneno na ukweli aliomwambia Dayness ndio ulimfanya ajiue kwa kujiona kuwa yeye Irene alikua ni chanzo cha kifo Dayness hivyo ilibidi Irene aseme ukweli wote kuhusiana na maisha yake na alianza na mwanae Vatican na alimwambia hivi , mwanangu kuna kitu nataka kukwambia na naomba ukishike sana kwa kuwa ni muhimu sana na unisamehe pale nitakapokuumiza hisia zako , mama ni nini tena hicho naomba uniambie , ni kuhusu maisha yako na ukweli kuhusu baba yako ukweli ni kwamba Marehemu mzee Shaban alale pema alikua mtu mwema na alikupenda sana ila hakuwa baba yako mzazi , sasa mama mbona unanichanganya baba yangu mzazi ni nani , huko ndipo ninapoelekea mnamo miaka 25 iliyopita baba yako mzazi alinitelekeza na ujauzito wako kisha akakimbilia mjini mimi nilitengwa na jamii nzima pamoja na wazazi wangu ila mzee Shabani pekee ndio aliniona na kunisaidia kwa kunioa na kuwa mke wake wa tatu hapo ndipo maisha yangu yalinyooka na kumsahau kabisa baba yako ila yupo na tupo naye hapa Mwanza anaitwa mzee Adam ni muhasibu wa TBL ila sasa ana matatizo kidogo akiwa sawa nitakupeleka ukamuone samahani sana mwanangu kwa kukuficha ukweli , hapana mama pole kwa yaliyokukuta sikuyajua ila ukipata muda utanipeleka nikamuone, haya sawa baba. Huku kwa mzee Adam mazishi yaliisha na kifo cha Dayness kilikua kama mwanzo mpya katika maisha ya Adam kwani Adam sasa alimpenda mwanae alirudi kazini na alijirekebisha tabia kwa kuacha pombe alijua kama mke wake angekuwepo angependa mume wake awe na tabia nzuri za hivyo sasa ulikua ni upweke katika familia nzima ya Mzee Adam ila kwa kuwa waliungana wawili yeye na mwanae waliishi kwa amani upendo . Kisha Irene alichukua hatua kubwa zaidi ya kwenda kumwambia Humphrey ukweli wote kuhusu maisha yake na mahusiano yake ya zamani na Adam huu ulikua ni ujasiri wa hali ya juu hapo alikutana na Humphrey na kuanza kumwambia hivi , habari yako Humphrey , nzuri tu mpenzi wangu habari ya kwako (huku akiweka mkono begani kwa Irene) Irene aliutoa mkono na kisha kumwambia Humphrey , nina kitu muhimu sana nahitaji kukuambia , kipi tena hicho au unataka tuoane sa hivi, hapana sio hivyo ila ni kitu muhimu sana katika maisha yangu mimi kabla ya kuwa nawe niliwahi kuwa na mpenzi na nilizaa naye mtoto mmoja ambaye ninaye kama hufahamu hilo na baba wa mtoto huyo nininini ni rafiki yako kipenzi Adam ndio alikua mpenzi wangu wa zamani na hadi sasa alikua bado ananipenda ila mi nilimkatalia na kukukubalia wewe ilikua ni sababu ili nimuumize tu Adam na kulipiza kisasi ila ki ukweli naomba msamaha kwa kuwa mimi sikukupenda kwa dhati , Irene siamini kama unanitenda hivi kweli yani mi niliamini nimepata mke wa kumuoa kumbe aisee kwa hiyo ndio tumeachana au yani Irene ukiniacha unanikumbusha maumivu ya marehemu mke wangu , Humphrey mimi kuwa na wewe haiwezekani kwa kweli yani ni kama kulazimisha pikipiki kuwa gari naomba samahani sana , Irene alimuacha Humphrey na kuondoka zake dah Humphrey aliumia sana ila ndio hivyo hakuwa na jinsi ya kufanya alijikaza kiume tu , huku kwa Martha zilitokea dalili ambazo zilimshitua sana alianza kutapika na kujisikia vibaya hivyo akaamua kwenda hospitali kujua nini kilimsumbua kiafya ndipo alipopata jibu lililomshitua sio tu kiakili bali ilikua ni mabadiliko ya kimwili " umia ujae " ndiyo kilichomtokea Martha alikua na ujauzito kama wa wiki zipatazo mbili hivi aaaaaah aliona hata aibu kumwambia ukweli baba yake na baba mtoto wake Vatican ilikua ni kipindi kigumu sana kwake ila bahati mbaya tumbo hua halifichiki ndipo mzee Adam akaanza kuona dalili kisha akaamua kumuuliza , Martha mama njoo maramoja kuna kitu nataka kukuuliza , shikamoo baba , marahaba habari yako , nzuri tu baba , ila mimi naona sio kama nzuri sana , kwa nini unasema hivyo baba , mama naona mabadiliko sana katika mwili wako wala sio unene huo hayo ni mabadiliko makubwa Martha mi sitakufanya chochote ila naomba uniambie ukweli wote

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 22

Siri hufichuliwa na mjasiri woga ukikithiri
Sehemu ya 22

basi Dayness alikwenda na wazo la kuiokoa ndoa yake aliwaza aende kukutana na Irene na kuongea naye kwani alihisi kuwa Irene alikua chanzo cha mume wake kuwa hivyo . Kweli Dayness alifika nyumbani kwa Irene na alikaribishwa na Vatican , hakujua kwamba Vatican alikua mpenzi wa mtoto wake Martha kweli Dayness alikaribishwa ndani na kumkuta Irene , Vatican aliwapisha waongee , Dayness akaanza ,dada huyo ni kijana wako , ndio kijana wangu wa kwanza anaitwa Vatican kamaliza chuo mwaka huu bado yupo nyumbani hajapata kazi si unajua ajira kwa vijana siku hizi ngumu , kweli kabisa dada , aisee samahani dada nimeshasahau utatumia kinywaji gani , hapana samahani wala usihofu nipo sawa kabisa, usione aibu hapa ni nyumbani , hamna tabu sema tu kuna jambo nataka kukuuliza dada , upo huru sema tu dada , nilikua nasema hivi naomba uwe mkweli dada sababu hili swala ni kubwa sana na na linahitaji ukweli kwa kweli mume wangu siku hizi amechanganyikiwa kabisa tokea Humphrey atangaze kukuoa mume wangu Adam kabadilika sana kitabia yani kama taarifa za ndoa yako zilimuwehusha kabisa na mi kwa muda mrefu nilihisi mabadiliko kutoka kwa mume wangu hakunipenda kama alivyonipenda zamani haki ya ndoa ilikosekana hata na salamu pia baya zaidi ni pale alipojiunga na unywaji wa pombe ndio akawa anarudi saa nane yani ndoa yangu iliteteleka sana sana dada nimeumia sana hadi sasa hivi kazi kaacha dada kama unahusika kwa lolote tafadhali naomba umuachie mume wangu niachie mume wangu nampenda sana dada tafadhali Dayness aliongea hayo huku machozi yakimbubujika katika paji lake jeupe la uso kama mtu angeweza kukinga kikombe basi machozi yale yalikua mengi yangeweza kujaza jagi kabisa kisha baada ya kukaa muda mfupi akiwa kimya Irene alimjibu, dada  pole na samahani sana kwa hilo ki ukweli mimi naomba nikueleze hivi huyo kijana unayemuona hapo ni mtoto halali wa Adam anaitwa Vatican mimi na Adam tulikua wapenzi tulipokua watoto kijijini tulipozaliwa Igombe kisha tukiwa bado tunasoma Adam alinipa ujauzito na kisha akaniacha na kukimbilia mjini mimi huko kijijini shule niliacha wazazi wangu na jamii ilinitenga nikaishi peke yangu na tumbo langu ( huku akilia)kwa kweli dada niliteseka nan niliumia sijapata kuona hadi pale alipotokea msamaria mwema mzee Shaban aliyeahidi kunioa na kurudisha heshima yangu hapo ndipo nilianza mwanzo mpya wa maisha yenye furaha mimi na mwanangu kisha nilijiapia sitomtafuta wala kumwambia chochote Adam kuhusu taarifa zangu na mtoto na yeye tangu akimbilie mjini hakuwahi kurudi mimi nilipohamia mjini baada ya mume wangu kufariki na kuniachia urithi ulioniwezesha kuanza maisha mapya huku mjini na ndio hadi sasa nipo hapa mara ya kwanza nakutana na Adam alinishangaa na kisha kadri siku zilivyozidi kwenda aliniomba msamaha na kunitamkia kuwa alikua bado ananipenda ila mi nilimkatalia na kumwambia kuwa anaweza kuwa rafiki tu basi kwa ufupi ndio hivyo ,dada kumbe Adam ana mtoto mkubwa hivi na hakuwahi kuniambia , pole sana dada hayo yalikua ya zamani , ila madhara yake yanaonekana sasa hivi dada kumbe mimi ndio niliharibu mapenzi yenu kwa kuingilia kati , hapana dada hapana , usifiche ni ukweli mtupu isingekua mimi kuolewa na Adam angekua tayari ameshakutafuta na mngerudiana , hapana dada achana na mawazo hayo we jaribu kumjenga mume wako kisaikolojia anisahau mimi , sasa nitafanyeje, mimi nitakusaidia kwa kuhama mji huu ili mume wako asiwe ananiona , basi dada ni hayo tu mi naomba niondoke , jamani karibu tunapika , ahsante kwaheri, haya kwaheri. Dayness alipofika nyumbani akili yake ilimtuma kuwa yeye ndio alikua chanzo cha yote hayo yani isingekua yeye Adam na Irene wangekua hawana matatizo wala mapenzi yake yeye na Adam yasingekuepo na asingeumia hivyo alijilaumu sana na kisha akachukua maamuzi magumu , chumbani alipokuwapo alimuita Martha na kumuhusia mambo yote kuhusu mapenzi na mahusiano kwamba hata siku moja asijaribu kuchukua mpenzi wa mtu mapenzi yanaua kisha alimtuma Martha Juisi ya matunda na Martha alipoleta Dayness alimkumbatia Martha kwa nguvu yapata dakika nzima huku akitokwa machozi Martha aliuliza kama kuna tatizo na mama yake alisema hapana kisha Dayness alimtuma Martha sokoni amfuatie matunda Martha alipotoka tu ndani na kuondoka Dayness alichukua sumu ya unga ya panya na kuchanganya na juisi aliyokua nayo kisha akainywa haikuchukua muda kufanya kazi Dayness aligaagaa huku na kule akihangaika chini kwa muda kisha akatoa povu jeupe mdomoni na kukata roho maskini Dayness alijiua

Sunday, October 11, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 21

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
SEHEMU YA 21

Dayness kwa Irene kwamba ndio mke wake na Dayness hakusita kumuomba msamaha Irene kwa kitendo alichomfanyia , Dada samahani sana naomba radhi jana kwa mambo niliyokufanyia , usihofu dada hakuna tatizo, wote wakakaa na kujumuika pamoja kwa chakula cha jioni hapo walipiga stori na kubadilishana mawazo kila mtu akiwa na mwanamke wake ila kumbe ule ulikua ni mpango wa Adam kumweka sawa mke wake Dayness na aache wivu wake Ila pia taarifa mbaya kwa Adam zilikua ni hizi siku hiyo ni pale Humphrey alipopiga magoti chini na kutoa kiboksi kilichokua na pete ndani yake akiwa amemshika mkono Irene na kuelekeza kabisa pete ile karibu na kidole cha Irene huku akisema maneno haya , Irene will you marry me , Irene alikaa kimya kidogo kumuangalia Adam alikua ameinamisha kichwa chini huku kamshika mkono mke wake kisha baada ya kufikili kidogo Irene alikisogeza kidole chake hadi kikatosha kabisa kwenye ile pete na akajibu ndiyo huku akimnyanyua na kukumbatiana na Humphrey, kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu aisee Adam aliumia sijapata kuona hadi mke wake akashitukia kidogo, kisha wakiwa na furaha huku wakiwa wamekumbatiana na kushikana mikono Humphrey na Irene walishitushwa na kauli ya rafiki yao Adam alipoaga na kuomba eti awaache wafurahie siku yao hahahaha kweli mpenzi yanaumiza Adam aliumia sana kuendelea kukaa pale hivyo aliona bora aondoke asiendelee kuumia pia kitu hicho kilikua nje ya mpango wao na Humphrey hivyo aliona Humphrey kama amemsaliti kwenye mpango waliopanga na njia pekee ilikua kuondoka na kuumia mwenyewe nyumbani kweli alimchukua mke wake wakaaga na kuondoka , Humphrey yeye kwake furaha tupu na kisha akaagana na Irene wakaachana.Irene alipokua peke yake aliwaza na kujua kuwa alikua anachezea tu hisia za Humphrey ili kumuumiza Adam kweli dunia hii unaweza hata ukamuoa mwanamke na kuishi naye na mkazaa naye kumbe hakupendi alifanya hivyo tu kumuumiza mtu mwingine ambaye aidha ni mtu wa karibu yako sana na anawaona na anaumia sana ndivyo mzunguko wa maisha ulivyo na watu baadhi hupitia huko. Adam aligeuka na kuwa kama chizi sasa nadhani alifunga ndoa na baa kabisa kwani Adam alikua mlevi wa kupindukia alirudi usiku wa manane upendo tena kwa mke wake uliisha kabisa hata mtoto wake tu Martha hakumjali yani alichanganyikiwa hata sijui mfano wake nisemeja kazini aliacha kwenda na siku moja Humphrey alimtembelea kumpa kadi ya harusi yake nadhani hapo ndipo Adam alipotaka kufa kabisa Dayness aligundua kuwa mume wake hakuwa sawa na mwanamke mwenye mapenzi mema na mume wake hutafuta chanzo cha tatizo na kuiokoa ndoa yake hata kwenye biblia imeandikwa mwanamke mwerevu huiokoa ndoa yake bali mpumbavu huiangamiza , basi Dayness alikwenda na wazo la kuiokoa ndoa yake aliwaza aende kukutana na Irene na kuongea naye kwani alihisi kuwa Irene alikua chanzo cha mume wake kuwa hivyo . Kweli Dayness alifika nyumbani kwa Irene na alikaribishwa na Vatican , hakujua kwamba Vatican alikua mpenzi wa mtoto wake Martha. 

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIR WOGA UKIKITHIRI 20

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
SEHEMU YA 20

Dayness aliyekua anamfuatilia mume wake kuwa wapi hua anakwenda ili ajue ni nani anayemuharibia mume wake hadi mapenzi yao yanapungua alifika , alipofika tu hakuamini alichokiona machoni kwake Dayness hakuweza kuizuia hasira yake na kumpalamia Irene kwa vibao na magumi Adam alijitahidi kumzuia sana Dayness asimfikie wala kumuumiza Irene ila alichoharibu zaidi ni pale Adam alipomshikilia Irene badala ya mke wake Dayness hapo ndipo Dayness alipatwa na hasira zaidi na kuondoka katika maeneo hayo Adam alimuomba Irene radhi na kumkimbilia Dayness. Dayness alikimbia kwa haraka kwenye gari lake na kuondoka Adam naye hakusita kumfuatilia mke wake hadi nyumbani .Dayness aliendesha gari ovyo sana wakati akienda nyumbani nusura amgonge mtoto wa shule kwa mwendo kasi aliokua nao ila akamkwepa na yeye kwenda kugonga nguzo ya umeme iliyokua kandokando ya barabara , kama uliwahi kusikia mapenzi yanaua na ukajiuliza maswali mengi sana ni kivipi mapenzi yanaua basi hii ndio njia mojawapo ya mapenzi yanavyoua. Mungu saidia Dayness akatoka mzima wa afya haraka alikimbia na kulitelekeza gari lile na kupanda daladala alipofika nyumbani kila kitu kilichokua mbele yake alikitupa na kuharibu haribu kisha akaenda chumbani na kuweka nguo zake zote akiwa aliye dhamilia kuondoa ila akiwa anaendelea Adam akafika , Mke wangu mke wangu Dayness sikiliza basi mke wangu eeeh nisikilize basi usije ukajutia baadae maamuzi unayoyafanya na kumuumiza mtoto wetu Martha hebu nisikie basi , Dayness aligeuka huku akilia na amsikilize Adam anasema nini na Adam akaendelea , ulichokiona mama Martha sio unavyofikilia huyo ni Irene mwalimu wa Martha wa kitangiri pia ni mpenzi wake Humphrey yule rafiki yangu kipenzi sasa hapo alikua ananielezea kuhusu ugomvi wao na Humprey sasa nikawa nampa pole ndio wewe ukaja hebu fikiri ni miaka ishirini na kadhaa tupo pamoja sasa sijawahi kukudanganya wala kukuumiza iweje leo unifikilie vibaya au hatuaminiani mke wangu siku hizi , Dayness huku akifuta machozi alikua kama aliyeridhika na jibu la mume wake na kwa upole akajibu, basi sawa mi nilijua labda ndio umeniacha sababu siku hizi sikuelewi kabisa haki yangu ya ndoa hunipi salamu imekua tabu au tuna ugomvi, hapana hapana mke wangu ni matatizo madogo madogo yalinipata kazini ndio maana nilikua hivyo , sasa mimi si ni mke wako unashindwa nini kuniambia matatizo yako tukasaidiana, eeeeeeeh basi basi mke wangu usihofu hayo matatizo madogo sema sasa au twende sa hivi eeeh mke wangu , mmmh kukwambia tu tayari ulishataka, si umeomba mwenyewe , we naye huzeeki , aaah wapi ng'ombe hazeeki maini wewe sema kama upo tayari , haya basi sawa njoo. Ugomvi huo ulisha hivyo na Adam akafanikiwa kuiokoa ndoa yake kwa muda kisha kesho yake alimwelezea rafiki yake Humphrey yaliyomkuta kisha Humphrey aliwaalika Adam na Dayness kwenye chakula cha jioni huku yeye akiwa amemualika Irene wote walikutana kwenye meza moja na kusalimiana kwa pamoja kabla hawajaendelea Adam alichukua nafasi hiyo kumtambulisha Dayness kwa Irene kwamba ndio mke wake na Dayness hakusita kumuomba msamaha Irene kwa kitendo alichomfanyia.

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 19

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
SEHEMU YA 19

wewe kama mtu mzima ulishajua nini kilichoendelea hahahahaha jiongeze mkubwa hayo ndio yaliyoendelea huko. Vatican naye nyumba yake ilianza kuteteleka sijui ni sababu ya Irene baada ya kumuona yani mapenzi yake kwa Dayness yalianza kupungua muda mwingine hata kusalimiana ilikua tabu na haki ya ndoa ilipungua na kukosekana kabisa siku nyingine ilikua sio kama zamani alivyokua na mapenzi kwa mke wake maskini Dayness alihisi kuachwa kabisa ila kama kawaida ya wanawake hua hawaachi kufuatilia chanzo ni nini siku moja akamfuatilia mume wake anakwenda wapi siku moja Adam alimuomba Irene wakutane kuna kitu anataka kumwambia kweli kwa kuwa Adam alikua mzazi mwenzie Irene hakukataa kuonana naye na alijua ni kitu cha kawaida sana basi muda ulipofika kweli walikutana pale pale kwenye hoteli yao walipokua wanakutania Irene alikuja kwa muda muafaka waliopangiana wakutane kila mtu akaagiza huduma yake aliyoiitaji na kuanza maongezi Adam hakusita kuanza na salamu , za saizi , salama, habari za kazi , mmmmh ni nzuri, pole na kazi , ahsante , naomba radhi kwa kukupotezea muda wako , hapana wala haina shida kabisa kumbuka nilikuhakikishia kuwa utakua rafiki yangu hivyo sioni tabu au shida kuongea nawe, aaa basi sawa ila naomba hili jambo ninalotaka kukwambia ulichukulie umuhimu sana na unijibu ipasavyo , jambo lipi, kiukweli mimi nilikua napenda uniambie kama mwanangu ulijifungua au alikufa niwe na uhakika kabisa , Irene alikaa kimya kwa muda kisha akaguna kama aliyekua anavuta pumzi kusema kitu huku Adam akiwa amemkazia macho kujua Irene angesema nini na Irene akaanza kusema kwa sauti ya chini na kumwambia uliponiacha kijijini na ujauzito sio tu familia yangu kila mtu alinitenga na nikaishi mwenyewe sikuwa na wakunisaidia hivyo nilijifungua kwa shida na kwa bahati mbaya mtoto alifariki, pole sana , Irene alidiliki kudanganya huku akilia Adam kwa mapenzi mema alinyanyuka na kumsogelea Irene na kumkumbatia kama kumnyamazisha alipokua analia wakati Irene alifahamu kuwa anadanganya ila alijifanya mwenye majonzi huku akijiliza liza , Adam alimkumbatia Irene na kumbe Dayness aliyekua anamfuatilia mume wake kuwa wapi hua anakwenda ili ajue ni nani anayemuharibia mume wake hadi mapenzi yao yanapungua alifika , alipofika tu hakuamini alichokiona machoni kwake 

SIR HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 18

SIRI HUFICHULIWA NA UJASIR WOGA UKIKITHIRI 18
SEHEMU YA 18

Irene alisita kidogo na alipoangalia watu wote katika hoteli hiyo waliduwaa wakiwaangalia wao kwa kuepusha aibu Irene ilibidi aeleweke tu na kusema haya nimekusamehe simama sasa , ahsante alijibu Adam ambaye aliposimama hakusimamam hivi hivi bali alijifanya kajisahau na kumkumbatia Irene ambaye naye kwa kuwa ni mbele ya watu aliweka mikono yake mgongoni mwa Adam na kumkumbatia huku Adam kakamatilia kiuno daaah huyu jamaa kweli ngombe hazeeki maini yani tabia zake zilikua zile zile kwa vijana wa sasa wangemuita kicheche , kisha wakakaa tena kwenye meza yao na Adam akaanza maongezi yake tena kwa Irene na kumwambia , ahsante kwa kunisamehe kisha naweza kujua mwanangu sa hivi yuko wapi na anaitwa nani , kwa hilo siwezi kukwambia kwa sasa ila naomba please please usidhani eti kukusamehe ndio mambo yako sawa hapana kwanza hapa una bahati sana na shukuru Mungu leo sijui nimeamkia wapi tu haya mi naomba niende sasa , aaah si nikupe lifti hadi kwako hata nipajue , hapana sitaki sitaki siku nikitaka upajue utapajua kwa sasa nitakachoweza kukuhakikishia ni urafiki tu mengine yote hapana, aaah masharti magumu hayo sawa mama nimekuelewa alisema Adam nakuagana kila mmoja akaenda kwake , Kesho ya muda wa mchana Adam alishangaa kumuona Irene katika viunga vya kampuni ya TBL mawazo yake yote yalimtuma anakuja kumtafuta yeye kumbe Irene alikuja kumuumiza zaidi Adam aliyefikiri kasamehewa hivi hivi tu kirahisi rahisi , Irene alikuja kumuona Humphrey , Adam si akatoka anajiamini kwamba Irene anakuja kwake kwa mbwembwe huku akitabasamu tabasamu kabla hajafika Irene alipokua Irene si akanyoosha mikono kama mtu aliyekua akihitaji kumkumbatia mtu fulani Adam si akazani ni yeye naye akanyoosha mikono kama anataka kumkumbatia Irene mara ghafla akatokea mtu nyuma yake Adam na kwenda kukumbatiana na Irene alikua ni Humphrey daaah Adam ilimuuma sana hii ilikua ni michezo ya kitoto ikichezwa na watu wazima hahahahahaha hayo ndio mapenzi bwana hayakui yani michezo ya kitoto mtu mzima anamfanyia mtu mzima mwenzake , huku napo sio pa kusahau kwani siku hii ndio haswa ile siku mjenzi alikua anakabidhiwa vifaa vyake vya kazi aanze kazi ilikua ni kazi ya kukimbiza mwenge yani namaanisha ilikua siku ya kuvunja ahadi ya siku nyingi waliowekeana ni hawa vijana wa kizazi kipya Vatican na Martha ndio hasa walikutana tena baada ya kutoonana kwa muda mrefu sasa nao waliona ulikua ni muda bora wa kupinga amri za Mungu kwa kuvunja mojawapo ya amri zake ambayo ilikua ni amri ya sita. Hawaanzagi hivi hivi bali ndani ya jiji la miamba miamba la Mwanza vijana hawa wawili walikutana katika hoteli ya Golden crest kupata maraha ya dunia yani duu yani daah Vatican kishamchomoa mama yake kama laki mbili hivi za kutumia siku hiyo mtoto mwenyewe mmoja huyo chochote atakacholilia anapewa haikua shida kupewa laki mbili na mama haya tuendelee, baada ya vinywaji na chakula hotelini hapo sasa ulikua ni muda wa kupumzika . Katika chumba walichokua Martha alienda kwanza kuoga humo humo bafuni na Vatican kwa haraka haraka zake alikua tayari ameshajiaandaa yani kabaki na nguo kama tatu mwilini mwake ambazo zilikua ni kaptula fupi na nguo ya ndani kisha na kaushi wakati akiwa anasubiria kwa hamu kumwaga marhamu harufu marashi ya utamu sogea wote tule humu Vatican aliweka kwenye redio wimbo wa Whitney Houston I will always love you Martha alitoka nao taratibu bafuni akiimba wimbo huo bila ajizi akaumwaga mchuzi mbele ya walowezi ni kile ki taulo alichokua amekivaa alikiachia kikaanguka hadi chini pwaaa mambo hadharani karibu mwandani tuonyeshane vya ndani mimba hiyo ajali kazini hebu karibia tusafishe nyota kila siku niwe ninakuota ilikua ni katika chumba kimoja kitanda kimoja watu wawili wakiwa na wazo moja na wakifanya tendo moja kwa pamoja huku hawajui kama ni wa baba mmoja aisee hatutapoteza sana muda huko wewe kama mtu mzima ulishajua nini kilichoendelea hahahahaha jiongeze mkubwa hayo ndio yaliyoendelea huko

Friday, October 09, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 17

                     SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
                                                 SEHEMU YA 17

haikuchukua muda akafika Irene mamamamama pwaaaa moyo wa Adam ulishituka alikua ni Irene yule yule mzuri vile vile kama zamani alipokua na miaka 17 mwenye sura ya kupendeza mwili ambao kama ulitengenezwa vile yani kama alikua bado binti kumbe mama wa miaka arobaini na kadhaa hivi Adam alibaki ameduwaa kama aliyeshangaa mwonekano mzuri wa Irene ghafla alishituliwa na sauti ya Humprey akimkaribisha Irene karibu mwalimu Irene , ahsante habari zenu, oooh salama salama Adam ,Adam unasalimiwa , Adam alishituliwa na Humprey kwani alikua bado ameduwaa huku akicheka hahaha salama tu mawazo haya, Humprey bila kuchelewesha muda akaanza utambulisho Adam huyu hapa anaitwa Mwalimu Irene ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi kitangiri , ooooh nashukuru kumfahamu huku akimpa Irene mkono , Irene naye akasita kidogo kisha akampa mkono Adam na Adam naye akatambulishwa kwa Irene , Irene huyu ni rafiki yangu kipenzi anaitwa Adam ni muhasibu mkuu wa TBL , oooh nashukuru kwa kumfahamu alisema Irene. Kisha Irene aliagiza chakula alichohitaji na kukaa Adam hakuacha kumtupia jicho Irene kwa chini chini mwishowe kama ka mchezo wakawa wanatupiana macho kwa kuibia mithili ya kutegeana yani huyu anamwangalia mwenzie kisha anapindisha macho na mwenzake pia anamuangalia mwishowe hadi Humprey akataka kuwashitukia na akauliza vp mnafahamiana au naona wote kwa pamoja wakaitikia aaaa hapana wala hatufahamiani , aaah sawa nilidhani mnafahamiana. Adam alianza kukumbuka zamani na kujiuliza kama Irene alikua mwalimu wa kitangiri basi ndio yule aliyewasiliana naye kitambo kipindi mwanae alipopotea shule pia akaanza kufungua simu yake na kutafuta namba ya Irene aliyoiifadhi miaka iliyopita kwenye simu yake Mungu saidia akaipata bwana hapo hapo akaanza uchokozi ulikua ni uchokozi wa kubip zaidi ya mara tatu akamudu kukatisha mazungumzo ya Irene na Humprey ila Irene kwa kukomesha akazima kabisa simu hapo akamkomesha kabisa kisha mazungumzo yao yakafana na kua vyema na sasa Humprey akapanga kutupa nanga za kiutu uzima na hapa akaanza pole pole ki hivi sasa mwalimu unalifikiriaje lile swala langu nililokugusia kipindi kirefu , jamani huniachi hata nifikirie kidogo jibu lako nitakupa tu , haya ngoja nisubiri, Adam kwa chini chini si akakaza macho kwa Irene hapo ndipo Irene alipochukua maamuzi magumu ni ya kusogea karibu na Humprey kisha akamwekea mkono juu ya mabega yake na kumwambia unajua nini Humprey unaonekana mwenye nia sana na mimi sasa naona wacha nikupe nafasi japo nijaribu nione kwa sababu nyinyi wanaume hua hamtabiriki mwanzoni mnaonyesha kama mna upendo kisha baadae mkipata mnachokihitaji hukimbia na kutuacha wapweke (Irene alimaanisha hivyo kama kumuumiza Adam kwa mafumbo) , aaah hayo mi siwezi kufanya mi bwana najua kutunza wanawake wala sitokuumiza na utu uzima wangu kweli huu nifanye mambo ya vijana hayo siwezi ,alisema Humprey , Huku Adam aliumia roho zaidi yale mapenzi ya zamani kwa Irene alikua bado anayo na aliumia kuona Irene anakwenda kwa Humphrey kiulaini kumbe Irene naye alifanya hivyo kumuumiza Adam asikie maumivu aliyoyapata yeye miaka kadhaa iliyopita na kweli Adam aliumia kabisa sema alijikaza kwa kuwa ilikua mbele ya rafiki yake. Kisha makutano hayo yaliisha na kila mmoja alimuaga mwenzake na kuondoka ilikua ni furaha kwa Humphrey na kilio kwa Adam na sasa Adam aliona acha ajaribu nafasi yake kwa kumpigia simu Irene , huku Irene akiwa na furaha kwamba kamkomesha Adam mara simu ikaita akapokea haloo nanana ( Adam alipata kigugumizi ) naongea na mwalimu Irene tafadhali , ndio mimi nikusaidie nini ,(Adam akakaza sauti kwa kukalipia) nimesema sitaki ujinga nataka unionyeshe mwanangu na unileze ni kwa nini miaka yote hiyo hupo hapa hukuwahi kunitafuta , wewe baba una wazimu kwanza naongea na nani we unapiga simu tu na kuanza kufoka unamfokea nani hebu kama umekosea namba bora ukate au useme we nani , (Adam kwa upole) aaaah samahani sana mi naitwa Mr Adam ni menejaaa, wala hata usimalizie ehe shida yako nini ? Una wazimu hivi ulidhani kuwa sitoishi uliponiacha na mimba yangu sasa umekosea njia mtoto wako hutamjua wala hana jina lako niache na maisha yangu niishi kwa raha kwanza nitamwambia rafiki yako kwamba unanisumbua , aaaaah basi basi yaishe Irene tukutane basi tuongee yaishe mi naomba msamaha najua nilikuumiza ila nina sababu zangu njoo tuongee nitakwambia ukweli wote , tafadhala tafadhali sana sitaki unipotezee muda wako na uongo wako wa tangu zamani , hapana naapa kweli sitatumia muda mwingi kukueleza naomba tafadhali , haya sawa wapi na saa ngapi, mmmh ni pale lenana hotel saa kumi jioni nadhani utakua umeshamaliza kazi zako, hayo hayakuhusu haya nitakuja, haya kwa he haloo haloo, kabla hajamaliza simu ilikua tayari ilishakata , kesho yake muda ulipofika kweli baada ya kazi Irene alikwenda Lenana Hotel pasiansi na kukutana na Adam, kwa mbwembwe kabla Irene hajakaa Adam akamvutia kiti na kumruhusu akae kisha akamuuliza Irene angetumia kinywaji gani na kuagiza, maongezi yakaanzishwa na Adam mwenyewe aisee siamini japo miaka imekwenda Irene we bado ni mzuri vile vile na mrembo wa kuvutia kwa kweli sichoki kukuangalia nikikumbuka zamani nilivyokupenda hadi moyo unaniuma , eeeeeh wewe baba sikuja kwa hayo hebu eleza shida zako haraka mi niondoke naona kama unanichelewesha , aaah samahani kwa hilo unajua tangu tuachane kijijini sijaacha kukufikilia wewe yani upendo wangu kwako bado upo ule ule , (Irene huku akitaka kunyanyuka) wewe hebu usiniletee mambo ya kizamani historia ambayo ilishafutika kichwani mwangu kama huna la kuniambia mimi naondoka , aaaa basi basi najua unanichukia sana kwa mambo niliyokutendea ila naomba samahani sana naomba msamaha kwa hilo Irene kuna sababu nyingi zilizonifanya kukuacha kijijini , kama zipi , nyingi tu, hazina majina au kumbe nia yako ilikua kunichezea na kukimbilia mjini , hapana hapana , ila , ila matatizo madogo tu , aaaah sawa hayo matatizo madogo ndio yananifanya na mimi nikuache sa hivi , usifanye hivyo usi , tayari Irene alinyanyuka na kutaka kuondoka Adam haraka alimdaka Irene miguu na kuing'ang'ania kwa kuikumbatia huku akiwa kapiga magoti na kichwa chake kipo usawa wa tumbo la Irene na akiwa kakiegemesha hapo akisema naomba msamaha nisamehe tafadhali Irene , mwili wa Irene ulisisimka na hisia zake zikamjia na kumrudisha mbali kumbuka ni miaka mingi hakuwahi kukutana na mwanaume yoyote kimwili sasa mkono wa Adam uliopita kiunoni mwake uliamsha hisia zake na kumkumbusha zamani sana kwa moyo wa hurumu Irene huku akiwa amemshika Adam kichwani akasema unaniaibisha bwana tafadhali simama simama , Adam akajibu siwezi kusimama hapa hadi uniambie kama umenisamehe au , Irene alisita kidogo na alipoangalia watu wote katika hoteli hiyo waliduwaa wakiwaangalia wao kwa kuepusha aibu Irene ilibidi aeleweke tu na kusema haya nimekusamehe simama sasa 

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 16

                  SIRI  HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
                                              SEHEMU YA 16

ahsante kwa chocolate dedication massari real love i love you . Hayo ndiyo ya moyoni ya Martha aliyoyatoa kwa Vatican. Vatican alipoipokea tu barua kutoka kwa Angel na kuisoma nusu alie alipiga makelele hayo kama mwanafunzi wa form four aliyepata matokeo kuwa kafaulu wakati asilia 80 wamefeli utani tu ila ki ukweli Vatican alikua mwenye furaha sana pia furaha hiyo iliongezeka zaidi pale Vatican alipofaulu kwenda mwaka wa tatu kwa ufaulu mkubwa wa GPA ya nne na hakusita kumshirikisha mama yake katika furaha yake ilikua kama kuokota dhahabu mchangani huku wengine wanahangaika kuchimba migodini . Shikamoo mama , marahaba hali yako ,nzuri , za masomo , nazo nzuri , vipi unataka shilingi ngapi sababu nishazoea ukinipigia tu wewe unaomba hela , haaaa mama sio hivyo leo nitabadilisha ratiba kidogo nina jambo jema nataka kukwambia mama yangu nimefaulu kwenda mwaka wa tatu tena kwa GPA kubwa mi ndio nimeongoza chuo kizima ,haya hongera zako , halafu pia kuna suprise nataka nikupe mama yangu , ipi hiyo ,ni siri utaona baadae , haya, halafu mama , mmh nini tena , nina shida ya kiasi kadhaa cha fedha , nilijua tu wewe uache kuomba hela mtoto wewe kama ulizaliwa benki vile haya shilingi ngapi , kama laki tatu hivi , haya kesho, haya mama siku njema ,nawe pia masomo mema baba, haya kwaheri ,haya. Kwa mtoto wa mwalimu mkuu ilikua sio kazi kupewa laki tatu ni kama kuomba maji mtoni yani ilikua rahisi kweli kweli . Masomo yaliendelea na Martha alikua kidato cha nne wakati fulani akafunga shule na likizo hakwenda Mwanza kwani ilikua likizo ya muda mfupi kama wiki moja tu hapo alipata nafasi rasmi sasa ya kukutana na Vatican tena aisee Martha maharage ya shule yalimkubali alikua kanona ile mbaya alinenepa kwa kiasi kama ni ngombe basi hata wasingengojea sikukuu tayari angekua ameshachinjwa umbo lake mithili ya namba nane na alivyonawiri mweupeee Vatican alikosa cha kuongea ila cha kushangaza zaidi walipoonana hakuna aliyemsemesha mwenzake hapa ilitumika lugha ya matendo yani walicheka kila mmoja akitabasamu na kucheka kumvutia mwenzie ilikua kama sumaku vile huo mvutano yani ghafla kila mmoja alijikuta kwenye ndimi ya mwenzake wakaanza kubadilishana bacteria mwaaa mwaaa ndio sauti zilizosikika. Kubadilishana mate tu watu kidogo wajigonge wengine nao hadi wakaacha shughuli zao wakishangaa watu wanang'atana midomo bila kuumia Vatican hapo kakamatilia kiuno taratibu anashusha shusha mkono hadi kwenye makalio hahahahahaha ndivyo mambo ya vijana yalivyo ila sasa hili lilikua fumanizi ni Mary alitoka nje na kukuta Vatican na Martha wakifanya yao aisee ilimuuma sana na Mary hua akopeshi hapo hapo aliwafuata na kuanza kuongea mhhh haya wapendanao sasa mtauza sana sura mwaka huu sijui nawe umempendea nini gunia kama hili (huku akimwekea kidole usoni Martha) Martha kidogo atake kupigana ila Vatican akamzuia hawakuishia hapo kula raha bali walirudi tena JB Belmont kukumbushia raha za siku ile ya zamani huko kama kawaida yao hawakuacha kunywa na kula vya kutosha ila sasa Vatican alidhamiria kuvunja amri ya sita siku hiyo kwani alikazana sana kumshika shika Martha mapaja mara kumbusu sana kama aliyehitaji Mambo fulani hivi kutoka kwa Martha kwa kuwa ilikua ni the promise ilibidi Vatican awe mpole na kusubiri hadi siku ya ahadi itakapofika siku hiyo Martha alikua makini sana hakunywa pombe wala hakutaka kukaa sana kwenye starehe siku hiyo hivyo alirudi mapemaa nyumbani kisha wakaagana na kuachana kila mmoja alilala kwa furaha huku akimfikiria mwenzake ilikua ni kama ndoto na siku hiyo hakuna aliyelala kwa raha walizoponda siku hiyo kama mwenye njaa kutupwa katika msitu wa matunda. Likizo iliisha na Martha akarudi shule siku nazo hazigandi kama maziwa mtindi kujenga historia zaidi ya mwanamalundi sasa Martha alimaliza kidato cha nne sio yeye tu pia na Vatican naye alimaliza mwaka wa tatu chuo hivyo kama muda wa kutimiza ule usemi wa ahadi ni deni ulitakiwa utimizwe yani ni kuwasumbua wachawi kwa sauti za kuwafanya wasiloge usiku na kuwasikiliza nyie hahahahaha najua ulishatambua kama una nia ya kujua ni zile mechi muhimu zenye matokeo matatu tu kushinda kushindwa au kutoa sare tena zipo za uwanja wa nyumbani na zile za ugenini ila kubwa zaidi ni zile za kimataifa hapo uwanja wa taifa kuna heshima yake hapo we acha yani unalichezea taifa lako , tuachane na mbwembwe hizo tuje kwenye mahafali iliyofana sana ilikua ni mahafali ya Martha kumaliza kidato cha nne aisee haya mahafali yalikua ya kifahali watu walikula hadi wakawa wanaitwa warudie tena , mzee Adam alikuepo mama Martha Dayness na Mary kuchukua taarifa za umbea .Martha alipewa laptop kama zawadi kutoka kwa baba na saa ya dhahabu kutoka kwa mama , Vatican naye hakusita kupita japo kwa mbali japo alione ua la moyo wake kheri subuhana na radhi zake upendo huu uishe kwake aisee yani mvutano zaidi ya marhamu tamu inavyonukia huku Martha akinuia japo amuone hata kwa mbali Vatican naye alisubiri apate majibu ya asali asije umia kwa uchungu wa shubiri wakakutana wawili kama hadithi vile kidogo mambo yafanyike yakumtafuta mrithi ila aaah Vatican akajisemea sizitaki mbichi hizi " ishara ya upendo kuonyesha uvumilivu na skendo hatoi maulana uzuri wako bado msichana nakupenda tena nakupenda sana pindi uniachapo mi nitakazana niombe radhi kwako usije nihama atakayesema chokochoko ruhusa kumtukana" haka ni ka nyimbo ka msanii Joseph ambako Vatican alikua anakaimba huku kabeba  maua yake mawili kama ishara ya upendo na Martha kifuani mwake waliachiana na Martha akamuaga kwa busu hatari sijapata ona hadi watu walisikia kisha akarudi haraka kwa wazazi wake sherehe ikafana na ikawa kama historia mzee Adam hakutaka aaache kitu Martha alikua anaondoka naye kurudi nyumbani Mwanza huko atasubiri matokeo Martha alibisha kwanza kidogo baadae ikabidi akubaliane na baba yake na kurudi Mwanza Vatican naye hua ashindwi kitu si akarudi pia nyumbani kwao Mwanza sa hapo bila bila mzee Adam na Vatican . Milima haikutani ila binadamu hukutana, kwenye hoteli moja maarufu Mwanza ambayo wafanyakazi , mabosi na watu maarufu hukutana hapo kupata chai na chakula cha mchana hapo ndipo Irene kwa miaka zaidi ya mitano hivi anamwona tena Adam ila Adam ni baada ya miaka 25 anakutana tena na Irene aisee ilikua siku ya kazi jumatano Irene amekwenda kupata kifungua kinywa kama kawaida yake katika hoteli ile ila Adam yeye siku hiyo alipelekwa hapo na rafiki yake wa karibu sana na meneja masoko Humprey katika kampuni aliyokua anafanya kazi Adam ,lengo la Humprey ilikua ni kumkutanisha Adam na rafiki yake wa karibu wa Humprey ambaye katika tetesi Humprey alimwambia Adam kuwa angependa amuoe ila alikua bado akisubiri majibu kutoka kwa mama huyo. Kweli walitangulia wao kufika na kuagiza kile walichotaka Adam kwa shauku si akaanza , Humprey huyo mrembo mbona hafiki au umepigwa changa la macho hahahahaha na wazee unajua hua hatutaniani sasa kama ulitaniwa au leo siku ya wajinga nini ?, Aaaa Adam sipendi utani bwana haraka haraka haina baraka subiri atakuja uje umuone we mwenyewe utamkubali mama wa watu alivyoumbika. Kama unakumbuka zamani Adam naye alikua mtu wa wanawake hivyo sifa tu alizoambiwa na Humprey ye mwenyewe mate yakaanza anza , haikuchukua muda akafika 

Wednesday, October 07, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 15

                     SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
                                SEHEMU YA 15

Mary hakuwa na uwezo wa kutunza siri aliwapigia simu wazazi wake na Martha na kuwaeleza ukweli wote mzee Adam alikasirishwa sana na Kufunga safari kwenda Dar akiwa na mke wake Dayness walipofika wakakutana na mtoto wao kitu cha kwanza kabla ya salamu Martha alipokea kibao kutoka kwa baba yake mzee Adam , mama yake alijaribu kumtetea na kisha akaenda naye chumbani na kumwacha mzee Adam na Mary wakiwa nje mzee Adam alimpongeza Mary kwa kazi nzuri ya kutoa taarifa huko ndani napo mama yake Martha alimwamuru Martha avue nguo zote na kuanza kumkagua kwa kuwa yeye alikua mzoefu alijua kila kitu na akajua kuwa Martha alikua hajafanyiwa chochote na kumwambia mwanae , Martha pole sana mama kwa kibao kutoka kwa baba usichana wako bado unao usihofu mama ukufanywa chochote , kweli mama , kweli usihofu acha nikaongee na baba we kaa hapa sawa , sawa, alipotoka akamwita mzee Adam na kumwambia baba Martha Martha bado , umejuaje, mi nimeenda nikamkagua bado ipo , usije ukawa unamtetea mwanao , haa twende mwenyewe ukaone kawa unadhani nakutania , basi acha nakuamini sana mke wangu sa sijui nitamwambiaje wivu kweli na kile kibao ila lazima nimpeleke akasome boarding siku nyingine watamfanya kweli hebu niitie Martha alikuja huku akiogopa ogopa kisha mzee Adam akamwita na kumwambia Sikia Mama pole kwa kukuumiza ila hiki nitakachokwambia kitakuumiza zaidi nataka nikuamishe kabisa hapa na ukasome shuleni boarding, baba jamani mbona unanionea hivyo mi sipendi boarding maisha ya huko magumu sana , sasa nataka ujue maisha magumu yalivyo kuanzia leo utahamia bodying. Kweli uamuzi ukitolewa na mzazi tena baba huwezi kupinga ndio ilivyotokea kwa Martha alikubali na kupelekwa shule boarding hapo hapo shuleni kwao ila baada ya siku kadhaa hivi Vatican alikwenda alipokua anaishi Martha na ndugu yake Mary kufika pale jamaa alienda kajiandaa ile mbaya maua, chocolate. Kadi ya sorry vyote alibeba kama ishara ya upendo na kuja kuomba msamaha alipofika akakutana na Mary akamkaribisha ndani kisha alipomuulizia Martha, Mary alikaa kimya kidogo na kumwambia Martha hayupo kahamishiwa boarding shuleni , (kama akishituka hivi) boarding kwa nini, we si ulimfanyia vibaya heheheee halafu kumbe hakuna kitu , Mary Kumbe naye alikua anamtamani tamani Vatican akaanza kumwambia huku akaja kukaa karibu naye na kuanza kuvuta vuta sketi yake fupi , hivi we Vatican huoni wanawake wa kupenda yani unahangaika na Martha mtoto huyo analialia na kukusumbua hivi hutuoni (huku akinyanyuka na kujigeuza mbele nyuma kama anamuonesha Vatican umbo lake) umeona mambo hayo cheki mtoto ninavyolipa eleweka wewe utaendelea hadi lini kulala na chakula halafu una njaa unaacha kula kisa hujui cha nani au unaogopa funguka mtoto wa kiume nipo hapa kwa ajili yako sema sasa (huku akipitisha mkono wake shingoni mwa Vatican), aaah Mary acha kwanza basi tufanye hivi hebu chukua hivi . Akampa maua kadi na ile choclate Mary alifurahi akajua labda Vatican kishanasa kwenye mtego wake kumbe wapi mawazo ya Vatican bado yapo kwa Martha tu kisha Vatican alimuaga Mary na kumpoteza zaidi si akamkumbatia basi Mary kichwa hilo kajua ndege mjanja yupo kwenye tundu bovu kumbe wapi. Vatican alifuatilia hadi akampata mtu aliyekua anasoma st marrys day aliyeitwa Angel. Angel alikua anasoma darasa moja na Martha , Vatican alimtuma Angel akamsalimie tu Martha , Martha alipopata habari hizo moyo ulilipuka ila naye alikua kaanza kumpenda Vatican hata ile hasira aliyekua nayo kwa Vatican ilitoka alipojua kuwa Vatican hakufanya chochote basi mind game ndio ilifanya kazi hivyo Martha alitokea kumpenda sana Vatican kisha alimpa majibu Angel na kumwambia Akamwambie Vatican aandike barua kwa kuwa shule hawakuruhusiwa kuwa na simu kweli Vatican aliandika barua na kumpa Angel na ilisomeka kama hivi " mambo natumaini we ni mzima wa afya pole na samahani kwa niliyokutendea najua nilikuudhi sana ila naomba nikwambie ukweli nilipolala na wewe sikufanya chochote wala sikulala na wewe usiku mzima bali nilikuja tu asubuhi naomba unisamehe kwa kukuchezea akili nakutakia masomo mema love you. Ndani ya barua yake Vatican aliweka chocolate kama ishara ya kumvutia Martha. Martha naye hakusita kujibu barua hiyo na kuandika hivi Kwako kipenzi Vatican najua kuwa nilikua na hasira kwako ila hilo ilikua ni sababu nilihisi umenitendea matendo mabaya ila haikua hivyo nimeamini kuwa we ni muaminifu na unanipenda kweli nachukua nafasi hii kukuambia kuwa nimekubali kuwa mpenzi wako kuanzia leo ila kwa masharti haya matatu kwanza sitopenda tukutane kimwili hadi nimalize kidato cha nne pili sipendi kuumizwa na nitajiua nikigundua una mpenzi mwingine hivyo nataka uwe wangu peke yangu tu hilo muhimu sana kisha sitopenda nifahamike sana kwa rafiki zako kuwa mi ni mpenzi wako naomba kwa sasa iwe siri ahsante kwa chocolate dedication massari real love i love you .

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 14

                       SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 14
                                                  SEHEMU YA 14

ulipofika muda wa muziki wa taratibu ndipo Vatican akatingisha kiberiti ki hivi , hivi Martha unaionaje siku ya leo , ni nzuri ahsante kwa kunitoa out ni my first date ila nime-enjoy , poa hivi ni mwanaume wa aina gani we unapenda uwe nawe , mmmh awe mrefu mwenye umbo handsome anapenda kuongea na sifa nyingine , hivi ukiniangalia mimi sina sifa hizo , unazo we ni mrefu handsome charming , hivyo nafaa kuwa na msichana kama wewe , yaah unafaa ila sio mimi , kwa nini , you are my friend , hivyo tu , yah thats all , kwani upande wa pili mi siwezi kua mpenzi wako , nooo Vatican noo , kwa nini , hapana tu , Martha nisikilize vizuri since the first day nimekuona i fell for you na sina jinsi yote haya nimefanya kwa kuwa nakupenda na si rafiki kama unavyofikilia Martha i love you i love you so much will you be my girl please Martha. Martha hakuwa na jibu na ghafla alimwachia Vatican na kuondoka. Martha alirudi na kukaa pale kwenye kaunta ya juu Vatican naye kwa haraka alimfuata na kwenda kukaa naye Martha alianza kulia na Vatican akaanza kumnyamazisha , Martha please i am sorry sijui kama ungeipokea hivi , please naomba uniache (huku akiendelea kulia) , siwezi kukuacha tumekuja pamoja sikia Martha kunipenda mi sio lazima leo na sina haraka sana sikia utakapokua tayari ndio unaweza kunikubalia mimi nilikua natoa kilichopo moyoni mwangu sikia eeeh sikulazimishi eti sa hivi ndio unipende muda wowote utakapokua tayari na ukakaa ukawaza kwamba unipende au usinipende hayo yatakua mawazo yako hivyo we ndio mwamuzi mi sikulazimishi i am still your friend right (Martha hakujibu kitu) please say it  I am sorry to play with your feelings i am sorry Martha friends (huku akimpa mkono) Martha naye akampa mkono na kuitikia kwa kichwa kama ishara ya kukubali kisha wakanyanyuka na kukumbatiana huku Martha akilia tu Vatican akiwa kamkumbatia akamtuliza huku akimpet pet mgongoni Martha. Sasa walirudi kwenye meza yao na Vatican akaanza kucheza mchezo unaitwa mind game kwanza alimshawishi Martha anywe mvinyo kidogo Martha alikataa na kusema hua anywi pombe Vatican alikunywa kidogo kisha akamwambia Martha kua sio chungu na ajaribu tu kweli Martha akajaribu na kama unavyojua bandu bandu huisha gogo na safari moja huanzisha nyingine ndivyo ilivyokua kwa Martha kosa la kunywa mara moja tu hakuacha kunywa tena mara nyingi aisee alilewa chakali na hapo akaanza tu kuropokaropoka kwa sauti kubwaa mara oooh Vatican ananipenda Vatican ananipenda hahahahahaha. Vatican kwa kuona Martha anamuaibisha haraka alimchukua na kumpeleka kwenye kile chumba alichokua amekilipia kisha akamwacha Martha humo na yeye kutoka nje kwanza aliporudi alikuta Martha tayari kishalala aliwaita wadada waliofanya kazi hapo na kuwaacha wakimbadilisha Martha nguo Kisha wakamuacha wamemfunga taulo tu na kumlaza kitandani kwa kuwa alikua amelewa sana Martha hakuweza hata kutambua yupo wapi kisha Vatican akacheza tena mchezo wa mind game hapa alilala sebuleni na Martha akalala kitandani kisha asubuhi sana kabla hakujakucha Vatican haraka alikwenda kitandani alipolala Martha na kulala pale na kujifunika shuka kama alikuwepo pale usiku mzima. Hakufanya chochote ila ilikua ni mind game tu kwa Martha . Martha alipoamka akashituka kufunua shuka tu akajikuta kalala na Vatican wee kwanza alipojikuta tu ana taulo Martha akajua tayari kitu cha kwanza ilikua ni kujishika na kuhakikisha kama kweli Vatican hakuharibu chochote ila akawa hajiamini bado ana hofu kitu cha kwanza ilibidi amwamushe Vatican . Wewe wewe Vatican , Vatican , mhh mhh , amka , oooh Martha mambo , sitaki mambo yako pumbavu ( huku akimpiga kibao Vatican na Martha akaanza kulia) umefanya nini ,nini mbona sikuelewi , Vatican i trust you kama rafiki yangu then hiki nini umenifanyia did you do that Vatican please niambie , Vatican hakusema kitu Martha kwa kuwa hakuwahi kufanya mapenzi hata siku moja hakujua maskini hivyo mawazo yake yote yalimtuma tayari Vatican alivunja kikombe tena na hivi Vatican hakumjibu kitu Martha alijua kwamba ni kweli akaanza kulia na kumlaumu Vatican akisema Vatican umenibaka umenibaka Vatican najuta kukuamini kwa nini kwa nini nilikuamini, Martha alichukua nguo zake na kuondoka huku akilia na kukimbia hapo ndipo Vatican kama alishituka na kuanza kumkimbiza Martha huku akimuita Martha alikimbia na kuondoka alipofika nyumbani alipokua anaishi alianza kulia ndugu yake Mary aligundua na kumuuliza Martha alimwambia kila kitu sasa kwa kuwa Mary hakuwa na uwezo wa kutunza siri aliwapigia simu wazazi wake na Martha na kuwaeleza ukweli wote

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 13

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
                                           SEHEMU YA 13

Siku ilifika kweli na Vatican alijipanga kukutana na mrembo Martha kwanza akanunua chocolate ya arpella na maua ya waridi mazuri kisha akavaa nguo zake mpyaa alizichukua hussein pamba kali ili kumfurahisha Martha , Vatican alivalia shati ya mikoni mirefu nyeusi jeans yake ya bluu saa nyeusi na kiatu cha clipper nyeusi Martha alinawiri vibaya mno kwa kuvaa gauni la pink lililombana kwenye hips na lilikua fupi likiishia mapajani na mkoba wa pink pia walikutana JB belmont hotel aisee Vatican alijitoa heri amalize hela yake yote kuliko kumkosa Martha. Alipofika tu Vatican kwa mkwala mara akatoa Ua kwanza na kumkumbatia huku akimvutia kiti akae kisha alipokaa tu akampatia arpella ooh arpella I like it thank you alisema Martha , Vatican naye hakusita kumsifia Martha kwa vazi lake alilokua amevaa ooh umependeza kweli kweli zaidi hata ya malkia wa uingereza ( huku akitia nakshi nakshi maneno yake) , ahsante , mnmmnmnh sijui utatumia nini leo soda, bia , maji ama nini , we mi bia situmii bado mtoto, mhhh kwani hua mnasema ukweli huku (akimuita muhudumu) , nipatie Malta na huyu mrembo sijui hebu muulize , mi naomba alvaro apple ,  wakaagiza kila walichokihitaji hadi chakula kisha Vatican ndio akaanza kuongea. Jamaa Vatican alikua kajipanga aisee msosi ulikua wa maana sana hapa chips, huku kuku, pale sandwich meza imechafuka vibaya kwa vinywaji nadhani waliagiza ili wasirudie kabisa kwa kuwa ilikua ni vinywaji kama kumi kwa kila mmoja Vatican naye sijui alijua mambo yote yataisha siku hiyo hiyo kwani alikua tayari ameshalipia na chumba kwenye hotel hiyo haya sasa ulikua ni muda wa kumwaga mchele kwa kuku kuona kama atakula ili kumkamata kirahisi na kumchinjia mgeni.mambo yakaanza hivi kwa vatican , unakionaje chakula , ooooh kiko poa kabisa , unajua hii hotel mi naiaminia hapa mjini ndio inaongoza kwa msosi na huduma nzuri , hee kweli kabisa yani msosi wao hadi nime enjoy kweli, kweli , vp we hua unapendelea nini , mhhhh mimi napendelea kusoma kutoka out na marafiki kuchart na mhhh nadhani ndio hayo , kulala je ,hahahahaha (akacheka) that is a part of life , ahaaaa yah its true kweli ni part of life , je vitu gani hupendelei ( huku akimuita muhudumu na kuagiza mvinyo wa zabibu au red wine) , haaaaa wine ya nini tena ? , we subiri , kwani we unakunywa wine , nitajaribu , mbona hapa ulikunywa marta au we mlevi unanificha , hapana subiri nataka nijaribu leo , mhhhh mi simo wala sitatumia , ok turudi tulipokua nimekuuliza hupendelei , sipendi majungu uongo usaliti nadhani hayo yanatosha , na kuhusu rangi whats your favourity colour , pupple , waaaaao puple nice , vipi una mpenzi , mmmmmmmmmh probably no mi bado mtoto bwana , kwa hiyo bado, yah sure, kwani huna mpango wa kuwa naye ,labda baadae nikikua kwani mama aliniambia sitakiwi kuwa na mchumba hadi nimalize shule kwani aliniambia mapenzi yanaua na mimi sitaki kufa sasa hivi. Hayo yalikua ni majibu ya kitoto ya Martha kwani hakujua chochote kuhusu mapenzi na alilelewa familia yenye maadili mema Siku ilifika kweli na Vatican alijipanga kukutana na mrembo Martha kwanza akanunua chocolate ya arpella na maua ya waridi mazuri kisha akavaa nguo zake mpyaa alizichukua hussein pamba kali ili kumfurahisha Martha , Vatican alivalia shati ya mikoni mirefu nyeusi jeans yake ya bluu saa nyeusi na kiatu cha clipper nyeusi Martha alinawiri vibaya mno kwa kuvaa gauni la pink lililombana kwenye hips na lilikua fupi likiishia mapajani na mkoba wa pink pia walikutana JB belmont hotel aisee Vatican alijitoa heri amalize hela yake yote kuliko kumkosa Martha. Alipofika tu Vatican kwa mkwala mara akatoa Ua kwanza na kumkumbatia huku akimvutia kiti akae kisha alipokaa tu akampatia arpella ooh arpella I like it thank you alisema Martha , Vatican naye hakusita kumsifia Martha kwa vazi lake alilokua amevaa ooh umependeza kweli kweli zaidi hata ya malkia wa uingereza ( huku akitia nakshi nakshi maneno yake) , ahsante , mnmmnmnh sijui utatumia nini leo soda, bia , maji ama nini , we mi bia situmii bado mtoto, mhhh kwani hua mnasema ukweli huku (akimuita muhudumu) , nipatie Malta na huyu mrembo sijui hebu muulize , mi naomba alvaro apple ,  wakaagiza kila walichokihitaji hadi chakula kisha Vatican ndio akaanza kuongea. Jamaa Vatican alikua kajipanga aisee msosi ulikua wa maana sana hapa chips, huku kuku, pale sandwich meza imechafuka vibaya kwa vinywaji nadhani waliagiza ili wasirudie kabisa kwa kuwa ilikua ni vinywaji kama kumi kwa kila mmoja Vatican naye sijui alijua mambo yote yataisha siku hiyo hiyo kwani alikua tayari ameshalipia na chumba kwenye hotel hiyo haya sasa ulikua ni muda wa kumwaga mchele kwa kuku kuona kama atakula ili kumkamata kirahisi na kumchinjia mgeni.mambo yakaanza hivi kwa vatican , unakionaje chakula , ooooh kiko poa kabisa , unajua hii hotel mi naiaminia hapa mjini ndio inaongoza kwa msosi na huduma nzuri , hee kweli kabisa yani msosi wao hadi nime enjoy kweli, kweli , vp we hua unapendelea nini , mhhhh mimi napendelea kusoma kutoka out na marafiki kuchart na mhhh nadhani ndio hayo , kulala je ,hahahahaha (akacheka) that is a part of life , ahaaaa yah its true kweli ni part of life , je vitu gani hupendelei ( huku akimuita muhudumu na kuagiza mvinyo wa zabibu au red wine) , haaaaa wine ya nini tena ? , we subiri , kwani we unakunywa wine , nitajaribu , mbona hapa ulikunywa marta au we mlevi unanificha , hapana subiri nataka nijaribu leo , mhhhh mi simo wala sitatumia , ok turudi tulipokua nimekuuliza hupendelei , sipendi majungu uongo usaliti nadhani hayo yanatosha , na kuhusu rangi whats your favourity colour , pupple , waaaaao puple nice , vipi una mpenzi , mmmmmmmmmh probably no mi bado mtoto bwana , kwa hiyo bado, yah sure, kwani huna mpango wa kuwa naye ,labda baadae nikikua kwani mama aliniambia sitakiwi kuwa na mchumba hadi nimalize shule kwani aliniambia mapenzi yanaua na mimi sitaki kufa sasa hivi. Hayo yalikua ni majibu ya kitoto ya Martha kwani hakujua chochote kuhusu mapenzi na alilelewa familia yenye maadili mema ya kikristo na hakuwahi kujifunza chochote kwani kwao alikua geti kali yani kutoka nje ilikua ni kwenda shule au kanisani tu na kurudi hivyo hakuwa na mazoea na watu zaidi ya wazazi wake. Vatican alikua bado hajasema hasa nia yake kuu ila sasa aliamua kuonyesha upendo kwa njia nyingine katika hotel hiyo siku hiyo kulikua na onyesho la wazi la wasanii wa kizazi kipya, Vatican na Martha walikula na kunywa vinywaji vyao haraka haraka na vinywaji vingine wakaacha si unajua kizungu zaidi hakuna kumaliza ili wahudhulie onyesho hilo lililokua ndani ya ukumbi wa hoteli hiyo, kabla hawajaenda waliingia kwanza kwenye chumba cha michezo huko Vatican hakuacha kuonyesha ufundi wake huku akiwa amemkamatilia kiuno Martha. Vatican alimfundisha Martha kucheza pool table, wakaenda kucheza mchezo wa magari ya kuteleza kurusha vitufe (bowling) kulenga shabaa na michezo mingine mingi. Katika safari zote zile Vatican alibeba DOMPO yake au wine aliyoagiza muda ule sijui nia yake ilikua nini hadi kutembea nayo. Masaa yalikatika na ilikua inaelekea usiku hapo wakaingia ndani ya club iliyokuwepo kwenye hotel hiyo ambapo ndio kulikua na shoo wao walienda na kukaa peke yao kaunta ya juu kwenye makochi na kuanza kuongea Vatican kwa uchokozi huku kamshika paja Martha kisha akaingia msanii kuimba watu wakaanza kucheza Vatican alipomwambia Martha waende kucheza Martha alikataa na kudai hajui kucheza hapo ndipo Vatican alipochukua jukumu la kufungua kitoa aibu chake yani wine na kuinywa kidogo kisha akaingia dancing floor kucheza Martha alicheka kwa staili alizokua anacheza Vatican yani ilikua ni vituko hadi Martha akaona aibu na kuamua kwenda kucheza naye ayayayayaya Vatican kama alifunguliwa upya na hivi mishipa ya aibu ishakata daaah alimbamba Martha kiukweli kweli ulipofika muda wa muziki wa taratibu ndipo Vatican akatingisha kiberiti ki hivi
 ya kikristo na hakuwahi kujifunza chochote kwani kwao alikua geti kali yani kutoka nje ilikua ni kwenda shule au kanisani tu na kurudi hivyo hakuwa na mazoea na watu zaidi ya wazazi wake. Vatican alikua bado hajasema hasa nia yake kuu ila sasa aliamua kuonyesha upendo kwa njia nyingine katika hotel hiyo siku hiyo kulikua na onyesho la wazi la wasanii wa kizazi kipya, Vatican na Martha walikula na kunywa vinywaji vyao haraka haraka na vinywaji vingine wakaacha si unajua kizungu zaidi hakuna kumaliza ili wahudhulie onyesho hilo lililokua ndani ya ukumbi wa hoteli hiyo, kabla hawajaenda waliingia kwanza kwenye chumba cha michezo huko Vatican hakuacha kuonyesha ufundi wake huku akiwa amemkamatilia kiuno Martha. Vatican alimfundisha Martha kucheza pool table, wakaenda kucheza mchezo wa magari ya kuteleza kurusha vitufe (bowling) kulenga shabaa na michezo mingine mingi. Katika safari zote zile Vatican alibeba DOMPO yake au wine aliyoagiza muda ule sijui nia yake ilikua nini hadi kutembea nayo. Masaa yalikatika na ilikua inaelekea usiku hapo wakaingia ndani ya club iliyokuwepo kwenye hotel hiyo ambapo ndio kulikua na shoo wao walienda na kukaa peke yao kaunta ya juu kwenye makochi na kuanza kuongea Vatican kwa uchokozi huku kamshika paja Martha kisha akaingia msanii kuimba watu wakaanza kucheza Vatican alipomwambia Martha waende kucheza Martha alikataa na kudai hajui kucheza hapo ndipo Vatican alipochukua jukumu la kufungua kitoa aibu chake yani wine na kuinywa kidogo kisha akaingia dancing floor kucheza Martha alicheka kwa staili alizokua anacheza Vatican yani ilikua ni vituko hadi Martha akaona aibu na kuamua kwenda kucheza naye ayayayayaya Vatican kama alifunguliwa upya na hivi mishipa ya aibu ishakata daaah alimbamba Martha kiukweli kweli ulipofika muda wa muziki wa taratibu ndipo Vatican akatingisha kiberiti ki hivi 

Sunday, October 04, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 12

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 12.
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

naitwa Vatican Shaban nasoma UDSM  mwaka wa pili je wewe , mi naitwa Martha Adam nipo marrys kidato cha tatu , du mbona unaonekana mkubwa sana( Vatican akiuliza kwa mshangao) , yaaah ndivyo nilivyo that's my shape ndio mwili wangu ila I am still young as you can see I am only 17 now ,aisee nice looking you are so gorgeous , waaaaaho thanks a lot you too looking handsomite ,Hahaha not that much daaah yani hapa ilikua ni maongezi kwa kizungu tu kwa sisi tuliosoma shule za asante mkapa hapo walikua wametuuza kabisa hata wale wenzangu na mimi walikua kwenye daladala hawakuelewa kitu waliishia kushangaa tu nakujiuliza au hawa watoto wa Obama nini? Nashuka next stand hapo alisema Martha kama akimuaga Vatican, poa ila wait may I have your phone number, sure save yours here it is (huku akimpa simu yake aliyokua kaishika mkononi)  Vatican fasta bila kupoteza nafasi aliandika namba yake na kujibeep hapo hapo na kumrudishia simu Martha na Martha akafika akiwa anataka kushuka akamuaga Vatican kwa kumkumbatia si unajua swaga za watoto wa marrys kama wazungu vile ok bye handsome huku akitoa fumbatio Vatican aliona rahaaaa hata alikua hataki kuachia I will call you later Vatican alipayuka kwa sauti na gari likaondoka. Daah kijana wa watu Vatican akafurahi kweli kukumbatiwa na binti Hahahaha alipofika nyumbani tu Vatican fasta akapiga simu ya Martha sauti ikasikika nyororo Vatican kidogo ashindwe kuongea haloo haloo haloo Martha aliita mara tatu si Vatican alikua bado ameduwaa na sauti ila akashituka haloo hehehehehe samahani ni mimi Vatican mambo vipi , Poa vipi , safii , mzima wewe , mzima za muda , aaah nzuri tu , unaishi wapi , ukifika kile kituo niliposhuka naweza kukuelekeza mi sipajui vizuri huku , kwa hiyo kwenu wapi , mi natokea Mwanza , ooooh ndipo na mimi natokea kumbe tunatoka mkoa mmoja we unaishi wapi Mwanza , aaah mi kwetu ni capri point , ooh sawa na hapa unaishi na nani , nipo nimepanga naishi na ndugu yangu , basi sawa ila nikuulize kitu , uliza tu , utakubali kweli , kama ni jambo jema nitakubali na kama ni baya hapana, kweli , kweli , ok hivi naweza kuwa rafiki yako , mhhh yah hakuna tatizo haya poa nikipata muda nitakuja kukutembelea, poa , haya rafiki siku njema , haya kwako pia siku njema. Daah ka moyo kalimdunda vibaya Vatican yani kukubaliwa urafiki na mtoto wa kike duuuh siku hiyo alilala vizuri sana siku kadhaa zikapita na Vatican akapanga safari ya kwenda kumuona Martha kweli akapiga simu na mrembo Martha akaja kumpokea daah nguo zake sasa ndio zilikua zikimchanganya Vatican kwani Martha alijua kupangilia mvao wa nguo zake ili zimpendeze hapa alikua kavaa kaptula fupi inaitwa kipedo na blauzi ya rangi ya zambarau kiukweli ilimtoa na Vatican hakusita kuonyesha kufurahia kumwona Martha kwa kumkumbatia kwa nguvu aisee wala hakutaka hata kumuachia Martha kwa kumkatisha akajitoa haraka na kumpa mkono na kumkaribisha walienda hadi kwenye nyumba aliyokua akiishi yeye na mtoto wa mama yake mkubwa aliyeitwa Mary aisee chumba kilikua kizuri hicho sijapata kuona si unajua watoto wa kitajiri chumba kilijaa vitu vingi hapa tv hapa hiki mara hiki aisee. Vatican akabaki anashangaa tu akaletewa kinywaji maongezi yakaendelea siku ikawa imeisha hivyo kisha Vatican akamuomba Martha watoke out kidogo nje ya mahali anapoishi sijui malengo yake yalikua nini ila katika mawazo ya Vatican aliwaza kuanza kutupa karata yake kwa Martha ili aone kama atakubaliwa . Siku ilifika kweli na Vatican alijipanga kukutana na mrembo Martha kwanza 

Saturday, October 03, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 11

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 11
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

aaaah ni kirumba polisi ukifika nijulishe nije sawa ,sawa .Adam alimaliza maongezi yake na Irene bila kutambua kwamba ndiye yule yule Irene aliyemkimbia kijijini haraka haraka Adam alijiandaa aende kumfuata mwanae kwa Irene kabla hajatoka simu yake iliita ghafla kupokea tu haloo Mr Mack mimi ni Mr Budodi meneja wa TBL njoo haraka ofisini kuna dharura imetokea haraka.Adam hakuwa na jinsi ilibidi akatishe safari yake ya kwenda kumfuata mwanae na kwenda kazini hivyo akaenda Dayness. Hata hivyo Adam hakufuta namba ya simu ya Irene.
 Miaka sita baadae baada ya kila mtu kuishi maisha yake na maisha yaliyokua mema
kwa familia ya Adam na familia ya Irene watoto wao tayari walikua wamekua wakubwa Martha sasa alikua binti mzuri aliyenawiri mweupe wa rangi na shepu yake sasa aisee utampenda hakuna mwanaume aliyepita karibu yake bila kumshangaa kwa uzuri wake mithiri ya binti wa kinyarwanda anang'aa mwenyewe sasa hiki kilikua ni kizazi kipya na teknologia ilishakuwa simu sasa ni za mkononi na ndogo si kama makubwa ya zamani. Martha alifaulu shule ya msingi kwa alama za juu sana na hivyo kuchaguliwa shule ya vipaji maalumu ila hakuipenda sana na sasa baba yake kwa kuwa alikua na pesa aliamua kumpeleka mwanae st.Marrys sekondari tawi la Dar- es- salaam kwani Mwanza walikua bado hawajafungua tawi lao. Martha alikwenda shule na kuanza haraka miaka ile na kwa sasa alikua kidato cha tatu. Si yeye tu aliyekua akisoma Dar bali na Vatican pia alikua akisoma UDSM Dar akiwa mwaka wa pili. Katika mishe mishe zake mjini kama vijana wa kisasa wanavyoita akiwa posta Vatican na haraka haraka zake za kugombania daladala si akajikuta kapigana kikumbo na mrembo wanagombania siti moja Martha kang'ang'ania hata ataki kuachia siti Vatican naye ndio alikua kawahi siti ila kwa kuwa tembo hashindwi na mkonga wake na udhaifu wa mwanaume ni mwanamke kisauti nyororo kilichotoka kwenye koo la mtoto mzuri ikesema kaka naomba nikae kilimnyanyua pole pole Vatican kama simba aliyekosa mawindo huyoo akasimama na kumwachia siti Martha akae huku yeye kashikilia bomba Hahahaha dhaifu kweli sijui ni umbo lililovutia rangi ya mtume na sauti ya kumtoa simba msituni vilimfanya Vatican aanze kuwaza yale maneno ya uongo ya usiku silali nakuwaza wewe tu , nikinywa togwa nakuona kwenye kata na mengine mengi. Ila Vatican yeye alikua mjanja si kama alivyokua baba yake Adam zamani hajui kutongoza hiki kilikua kizazi kipya cha mitandao woga hakuna , akiwa amesimama karibu naye Vatican akaanza swaga za watoto wa chuo wanavyofanya
Vatican:Mhmhmhmhmhmhmh niaje
Martha: safii mambo
Vatican: daah poa naona umetupia dress code white location wapi leo.
Martha: hapana mi nimependa
kuvaa hivi
Vatican ( huku akichanganya lugha yani kiswanglishi ili kuonyesha swaga za chuo ): oooh looking good in that dress umeibuy wapi zizou fashion nini
Martha: nooh nilichukua kwa Hussein pamba kali ndipo zipo nzuri za hivi kama unapenda nenda
hapo kuna kila aina ya nguo kama zako
Vatican hapo bonge la tozi chini kavaa raba ya converse nyeusi hapa ana ka t - shirt ka habari ndio hiyo kekundu saa ya puma nyeusi nzuri jeans yake nyeusi yani alikua ameng'aa kiukweli , vijana wa sasa wangemuita sharo kwa mng'ao wake sasa mabinti kama unaenda vibaya vibaya daah na kukutana na mtanashati huyo Vatican kulikua hakuna haja ya kubisha ni kumpenda tu maongezi yakaendelea sorry sikujitambulisha naitwa Vatican Shaban nasoma UDSM  mwaka wa pili je wewe ,

                                

Friday, October 02, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 10



SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 10
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

Baaadae Adam aliporudi hospitali kutoka nyumbani alipokwenda ghafla alikuta tayari Vatican alishatoka na hayupo mazingira yale basi akaona kama ndio kaepushiwa kesi naa kuondoka. Wala haikuchukua muda Vatican kupata nafuu na kurudi shule, Miaka hua haichelewi bwana Martha tayari alikua kakua na kaanza darasa la kwanza katika shule ya msingi kitangiri ambayo mwalimu wake mkuu alikua ni Irene daaaaah hapo sasa. Vatican pia alishinda la saba na sasa ailkua kidato cha kwanza pamba sekondari . Masomo ni mazuri kwa Vatican na kwa Martha pia wakati Dayness alipokuja kumuijia Martha shule ghafla akajikuta kajigonga kikumbo na Irene
Dayness: ooooooooh pole dada samahani sana
Irene: bila samahani dada pole kwako wewe vipi hujaumia
Dayness: hapana nipo salama kabisa wala usihofu
Irene : haya sawa sawa karibu sana shuleni kuna chochote ungependa nikusaidie
Dayness: kwani we ni mhusika hapa
Irene: naitwa mwalimu Irene ni mwalimu mkuu wa shule hii
Dayness: mi naitwa Dayness Haule ni mzazi nina mtoto wangu hapa yupo la kwanza anaitwa Martha tena huyo hapo ( huku akimkumbatia)
Irene : jamani kumbe ndio huyu mtoto mzuri sana inaonekana na baba yake atakua mzuri sana sababu mtoto ajafanana sana nawe hivyo atakua kafanana na baba yake.
Dayness: kweli kabisa mwalimu bab yake ukimuona ni mtu mmoja mstaarabu
Irene: kweli nami naona basi nakutakia siku njema na kwaher
Dayness: kwaheli mwalimu (huku akiondoka na mwanae) baasi maisha ndivyo yalivyosonga hivyo pole pole kila mtu akifanya mambo yake siku moja akiwa shuleni Irene alishangaa kumwona Martha peke yake huku wanafunzi wengine wakiwa tayari wamekwisha kuondoka ni mama yake alichelewa kumuijia kama mkuu wa shule Irene alichukua jukumu la kwenda naye Martha nyumbani kwake kwa usalama zaidi ila aliacha taarifa kwa mlinzi wa shule kuwa endapo Dayness angekuja ampe namba yake ya simu wawasiliane. mama Martha hakuwa na simu hivyo namba ile alimpa mume wake Adam aipige na aongee na mwalimu mkuu. Griiiiiiiiiiiiiim griiiiiiiiiiiiim ring ring ianita ngoja tusubiri apokee Adam alimwambia mke wake mara halooo Haloo naitwa Mr Mack A (Adam alijitambulisha kwa jina lake la ofisini ) ni baba wa Martha samahani naongea na mwalimu mkuu wa kitangiri , hee ndio mimi mtoto mlichelewa kumuijia nikaenda naye nyumbani nipo naye hapa yupo salama kabisa mnaweza kumuijia , basi ahsante sana nitakuja mimi kumchukua nielekeze kwako ni wapi , aaaah ni kirumba polisi ukifika nijulishe nije sawa ,sawa