Saturday, October 03, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 11

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 11
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO: 0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.com

aaaah ni kirumba polisi ukifika nijulishe nije sawa ,sawa .Adam alimaliza maongezi yake na Irene bila kutambua kwamba ndiye yule yule Irene aliyemkimbia kijijini haraka haraka Adam alijiandaa aende kumfuata mwanae kwa Irene kabla hajatoka simu yake iliita ghafla kupokea tu haloo Mr Mack mimi ni Mr Budodi meneja wa TBL njoo haraka ofisini kuna dharura imetokea haraka.Adam hakuwa na jinsi ilibidi akatishe safari yake ya kwenda kumfuata mwanae na kwenda kazini hivyo akaenda Dayness. Hata hivyo Adam hakufuta namba ya simu ya Irene.
 Miaka sita baadae baada ya kila mtu kuishi maisha yake na maisha yaliyokua mema
kwa familia ya Adam na familia ya Irene watoto wao tayari walikua wamekua wakubwa Martha sasa alikua binti mzuri aliyenawiri mweupe wa rangi na shepu yake sasa aisee utampenda hakuna mwanaume aliyepita karibu yake bila kumshangaa kwa uzuri wake mithiri ya binti wa kinyarwanda anang'aa mwenyewe sasa hiki kilikua ni kizazi kipya na teknologia ilishakuwa simu sasa ni za mkononi na ndogo si kama makubwa ya zamani. Martha alifaulu shule ya msingi kwa alama za juu sana na hivyo kuchaguliwa shule ya vipaji maalumu ila hakuipenda sana na sasa baba yake kwa kuwa alikua na pesa aliamua kumpeleka mwanae st.Marrys sekondari tawi la Dar- es- salaam kwani Mwanza walikua bado hawajafungua tawi lao. Martha alikwenda shule na kuanza haraka miaka ile na kwa sasa alikua kidato cha tatu. Si yeye tu aliyekua akisoma Dar bali na Vatican pia alikua akisoma UDSM Dar akiwa mwaka wa pili. Katika mishe mishe zake mjini kama vijana wa kisasa wanavyoita akiwa posta Vatican na haraka haraka zake za kugombania daladala si akajikuta kapigana kikumbo na mrembo wanagombania siti moja Martha kang'ang'ania hata ataki kuachia siti Vatican naye ndio alikua kawahi siti ila kwa kuwa tembo hashindwi na mkonga wake na udhaifu wa mwanaume ni mwanamke kisauti nyororo kilichotoka kwenye koo la mtoto mzuri ikesema kaka naomba nikae kilimnyanyua pole pole Vatican kama simba aliyekosa mawindo huyoo akasimama na kumwachia siti Martha akae huku yeye kashikilia bomba Hahahaha dhaifu kweli sijui ni umbo lililovutia rangi ya mtume na sauti ya kumtoa simba msituni vilimfanya Vatican aanze kuwaza yale maneno ya uongo ya usiku silali nakuwaza wewe tu , nikinywa togwa nakuona kwenye kata na mengine mengi. Ila Vatican yeye alikua mjanja si kama alivyokua baba yake Adam zamani hajui kutongoza hiki kilikua kizazi kipya cha mitandao woga hakuna , akiwa amesimama karibu naye Vatican akaanza swaga za watoto wa chuo wanavyofanya
Vatican:Mhmhmhmhmhmhmh niaje
Martha: safii mambo
Vatican: daah poa naona umetupia dress code white location wapi leo.
Martha: hapana mi nimependa
kuvaa hivi
Vatican ( huku akichanganya lugha yani kiswanglishi ili kuonyesha swaga za chuo ): oooh looking good in that dress umeibuy wapi zizou fashion nini
Martha: nooh nilichukua kwa Hussein pamba kali ndipo zipo nzuri za hivi kama unapenda nenda
hapo kuna kila aina ya nguo kama zako
Vatican hapo bonge la tozi chini kavaa raba ya converse nyeusi hapa ana ka t - shirt ka habari ndio hiyo kekundu saa ya puma nyeusi nzuri jeans yake nyeusi yani alikua ameng'aa kiukweli , vijana wa sasa wangemuita sharo kwa mng'ao wake sasa mabinti kama unaenda vibaya vibaya daah na kukutana na mtanashati huyo Vatican kulikua hakuna haja ya kubisha ni kumpenda tu maongezi yakaendelea sorry sikujitambulisha naitwa Vatican Shaban nasoma UDSM  mwaka wa pili je wewe ,

                                

0 comments:

Post a Comment