SEHEMU YA 21
Dayness kwa Irene kwamba ndio mke wake na
Dayness hakusita kumuomba msamaha Irene kwa kitendo alichomfanyia , Dada
samahani sana naomba radhi jana kwa mambo niliyokufanyia , usihofu dada hakuna
tatizo, wote wakakaa na kujumuika pamoja kwa chakula cha jioni hapo walipiga
stori na kubadilishana mawazo kila mtu akiwa na mwanamke wake ila kumbe ule
ulikua ni mpango wa Adam kumweka sawa mke wake Dayness na aache wivu wake Ila pia taarifa mbaya kwa Adam zilikua ni hizi siku hiyo ni pale
Humphrey alipopiga magoti chini na kutoa kiboksi kilichokua na pete ndani yake
akiwa amemshika mkono Irene na kuelekeza kabisa pete ile karibu na kidole cha
Irene huku akisema maneno haya , Irene will you marry me , Irene alikaa kimya
kidogo kumuangalia Adam alikua ameinamisha kichwa chini huku kamshika mkono mke wake
kisha baada ya kufikili kidogo Irene alikisogeza kidole chake hadi kikatosha
kabisa kwenye ile pete na akajibu ndiyo huku akimnyanyua na kukumbatiana na
Humphrey, kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu aisee Adam aliumia
sijapata kuona hadi mke wake akashitukia kidogo, kisha wakiwa na furaha huku
wakiwa wamekumbatiana na kushikana mikono Humphrey na Irene walishitushwa na
kauli ya rafiki yao Adam alipoaga na kuomba eti awaache wafurahie siku yao
hahahaha kweli mpenzi yanaumiza Adam aliumia sana kuendelea kukaa pale hivyo
aliona bora aondoke asiendelee kuumia pia kitu hicho kilikua nje ya mpango wao
na Humphrey hivyo aliona Humphrey kama amemsaliti kwenye mpango waliopanga na
njia pekee ilikua kuondoka na kuumia mwenyewe nyumbani kweli alimchukua mke
wake wakaaga na kuondoka , Humphrey yeye kwake furaha tupu na kisha akaagana na
Irene wakaachana.Irene alipokua peke yake aliwaza na kujua kuwa alikua
anachezea tu hisia za Humphrey ili kumuumiza Adam kweli dunia hii unaweza hata
ukamuoa mwanamke na kuishi naye na mkazaa naye kumbe hakupendi alifanya hivyo
tu kumuumiza mtu mwingine ambaye aidha ni mtu wa karibu yako sana na anawaona
na anaumia sana ndivyo mzunguko wa maisha ulivyo na watu baadhi hupitia huko.
Adam aligeuka na kuwa kama chizi sasa nadhani alifunga ndoa na baa kabisa kwani
Adam alikua mlevi wa kupindukia alirudi usiku wa manane upendo tena kwa mke
wake uliisha kabisa hata mtoto wake tu Martha hakumjali yani alichanganyikiwa
hata sijui mfano wake nisemeja kazini aliacha kwenda na siku moja Humphrey
alimtembelea kumpa kadi ya harusi yake nadhani hapo ndipo Adam alipotaka kufa
kabisa Dayness aligundua kuwa mume wake hakuwa sawa na mwanamke mwenye mapenzi
mema na mume wake hutafuta chanzo cha tatizo na kuiokoa ndoa yake hata kwenye
biblia imeandikwa mwanamke mwerevu huiokoa ndoa yake bali mpumbavu huiangamiza
, basi Dayness alikwenda na wazo la kuiokoa ndoa yake aliwaza aende kukutana na
Irene na kuongea naye kwani alihisi kuwa Irene alikua chanzo cha mume wake kuwa
hivyo . Kweli Dayness alifika nyumbani kwa Irene na alikaribishwa na Vatican ,
hakujua kwamba Vatican alikua mpenzi wa mtoto wake Martha.
0 comments:
Post a Comment