Wednesday, October 07, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 14

                       SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 14
                                                  SEHEMU YA 14

ulipofika muda wa muziki wa taratibu ndipo Vatican akatingisha kiberiti ki hivi , hivi Martha unaionaje siku ya leo , ni nzuri ahsante kwa kunitoa out ni my first date ila nime-enjoy , poa hivi ni mwanaume wa aina gani we unapenda uwe nawe , mmmh awe mrefu mwenye umbo handsome anapenda kuongea na sifa nyingine , hivi ukiniangalia mimi sina sifa hizo , unazo we ni mrefu handsome charming , hivyo nafaa kuwa na msichana kama wewe , yaah unafaa ila sio mimi , kwa nini , you are my friend , hivyo tu , yah thats all , kwani upande wa pili mi siwezi kua mpenzi wako , nooo Vatican noo , kwa nini , hapana tu , Martha nisikilize vizuri since the first day nimekuona i fell for you na sina jinsi yote haya nimefanya kwa kuwa nakupenda na si rafiki kama unavyofikilia Martha i love you i love you so much will you be my girl please Martha. Martha hakuwa na jibu na ghafla alimwachia Vatican na kuondoka. Martha alirudi na kukaa pale kwenye kaunta ya juu Vatican naye kwa haraka alimfuata na kwenda kukaa naye Martha alianza kulia na Vatican akaanza kumnyamazisha , Martha please i am sorry sijui kama ungeipokea hivi , please naomba uniache (huku akiendelea kulia) , siwezi kukuacha tumekuja pamoja sikia Martha kunipenda mi sio lazima leo na sina haraka sana sikia utakapokua tayari ndio unaweza kunikubalia mimi nilikua natoa kilichopo moyoni mwangu sikia eeeh sikulazimishi eti sa hivi ndio unipende muda wowote utakapokua tayari na ukakaa ukawaza kwamba unipende au usinipende hayo yatakua mawazo yako hivyo we ndio mwamuzi mi sikulazimishi i am still your friend right (Martha hakujibu kitu) please say it  I am sorry to play with your feelings i am sorry Martha friends (huku akimpa mkono) Martha naye akampa mkono na kuitikia kwa kichwa kama ishara ya kukubali kisha wakanyanyuka na kukumbatiana huku Martha akilia tu Vatican akiwa kamkumbatia akamtuliza huku akimpet pet mgongoni Martha. Sasa walirudi kwenye meza yao na Vatican akaanza kucheza mchezo unaitwa mind game kwanza alimshawishi Martha anywe mvinyo kidogo Martha alikataa na kusema hua anywi pombe Vatican alikunywa kidogo kisha akamwambia Martha kua sio chungu na ajaribu tu kweli Martha akajaribu na kama unavyojua bandu bandu huisha gogo na safari moja huanzisha nyingine ndivyo ilivyokua kwa Martha kosa la kunywa mara moja tu hakuacha kunywa tena mara nyingi aisee alilewa chakali na hapo akaanza tu kuropokaropoka kwa sauti kubwaa mara oooh Vatican ananipenda Vatican ananipenda hahahahahaha. Vatican kwa kuona Martha anamuaibisha haraka alimchukua na kumpeleka kwenye kile chumba alichokua amekilipia kisha akamwacha Martha humo na yeye kutoka nje kwanza aliporudi alikuta Martha tayari kishalala aliwaita wadada waliofanya kazi hapo na kuwaacha wakimbadilisha Martha nguo Kisha wakamuacha wamemfunga taulo tu na kumlaza kitandani kwa kuwa alikua amelewa sana Martha hakuweza hata kutambua yupo wapi kisha Vatican akacheza tena mchezo wa mind game hapa alilala sebuleni na Martha akalala kitandani kisha asubuhi sana kabla hakujakucha Vatican haraka alikwenda kitandani alipolala Martha na kulala pale na kujifunika shuka kama alikuwepo pale usiku mzima. Hakufanya chochote ila ilikua ni mind game tu kwa Martha . Martha alipoamka akashituka kufunua shuka tu akajikuta kalala na Vatican wee kwanza alipojikuta tu ana taulo Martha akajua tayari kitu cha kwanza ilikua ni kujishika na kuhakikisha kama kweli Vatican hakuharibu chochote ila akawa hajiamini bado ana hofu kitu cha kwanza ilibidi amwamushe Vatican . Wewe wewe Vatican , Vatican , mhh mhh , amka , oooh Martha mambo , sitaki mambo yako pumbavu ( huku akimpiga kibao Vatican na Martha akaanza kulia) umefanya nini ,nini mbona sikuelewi , Vatican i trust you kama rafiki yangu then hiki nini umenifanyia did you do that Vatican please niambie , Vatican hakusema kitu Martha kwa kuwa hakuwahi kufanya mapenzi hata siku moja hakujua maskini hivyo mawazo yake yote yalimtuma tayari Vatican alivunja kikombe tena na hivi Vatican hakumjibu kitu Martha alijua kwamba ni kweli akaanza kulia na kumlaumu Vatican akisema Vatican umenibaka umenibaka Vatican najuta kukuamini kwa nini kwa nini nilikuamini, Martha alichukua nguo zake na kuondoka huku akilia na kukimbia hapo ndipo Vatican kama alishituka na kuanza kumkimbiza Martha huku akimuita Martha alikimbia na kuondoka alipofika nyumbani alipokua anaishi alianza kulia ndugu yake Mary aligundua na kumuuliza Martha alimwambia kila kitu sasa kwa kuwa Mary hakuwa na uwezo wa kutunza siri aliwapigia simu wazazi wake na Martha na kuwaeleza ukweli wote

0 comments:

Post a Comment