Wednesday, October 07, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 15

                     SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
                                SEHEMU YA 15

Mary hakuwa na uwezo wa kutunza siri aliwapigia simu wazazi wake na Martha na kuwaeleza ukweli wote mzee Adam alikasirishwa sana na Kufunga safari kwenda Dar akiwa na mke wake Dayness walipofika wakakutana na mtoto wao kitu cha kwanza kabla ya salamu Martha alipokea kibao kutoka kwa baba yake mzee Adam , mama yake alijaribu kumtetea na kisha akaenda naye chumbani na kumwacha mzee Adam na Mary wakiwa nje mzee Adam alimpongeza Mary kwa kazi nzuri ya kutoa taarifa huko ndani napo mama yake Martha alimwamuru Martha avue nguo zote na kuanza kumkagua kwa kuwa yeye alikua mzoefu alijua kila kitu na akajua kuwa Martha alikua hajafanyiwa chochote na kumwambia mwanae , Martha pole sana mama kwa kibao kutoka kwa baba usichana wako bado unao usihofu mama ukufanywa chochote , kweli mama , kweli usihofu acha nikaongee na baba we kaa hapa sawa , sawa, alipotoka akamwita mzee Adam na kumwambia baba Martha Martha bado , umejuaje, mi nimeenda nikamkagua bado ipo , usije ukawa unamtetea mwanao , haa twende mwenyewe ukaone kawa unadhani nakutania , basi acha nakuamini sana mke wangu sa sijui nitamwambiaje wivu kweli na kile kibao ila lazima nimpeleke akasome boarding siku nyingine watamfanya kweli hebu niitie Martha alikuja huku akiogopa ogopa kisha mzee Adam akamwita na kumwambia Sikia Mama pole kwa kukuumiza ila hiki nitakachokwambia kitakuumiza zaidi nataka nikuamishe kabisa hapa na ukasome shuleni boarding, baba jamani mbona unanionea hivyo mi sipendi boarding maisha ya huko magumu sana , sasa nataka ujue maisha magumu yalivyo kuanzia leo utahamia bodying. Kweli uamuzi ukitolewa na mzazi tena baba huwezi kupinga ndio ilivyotokea kwa Martha alikubali na kupelekwa shule boarding hapo hapo shuleni kwao ila baada ya siku kadhaa hivi Vatican alikwenda alipokua anaishi Martha na ndugu yake Mary kufika pale jamaa alienda kajiandaa ile mbaya maua, chocolate. Kadi ya sorry vyote alibeba kama ishara ya upendo na kuja kuomba msamaha alipofika akakutana na Mary akamkaribisha ndani kisha alipomuulizia Martha, Mary alikaa kimya kidogo na kumwambia Martha hayupo kahamishiwa boarding shuleni , (kama akishituka hivi) boarding kwa nini, we si ulimfanyia vibaya heheheee halafu kumbe hakuna kitu , Mary Kumbe naye alikua anamtamani tamani Vatican akaanza kumwambia huku akaja kukaa karibu naye na kuanza kuvuta vuta sketi yake fupi , hivi we Vatican huoni wanawake wa kupenda yani unahangaika na Martha mtoto huyo analialia na kukusumbua hivi hutuoni (huku akinyanyuka na kujigeuza mbele nyuma kama anamuonesha Vatican umbo lake) umeona mambo hayo cheki mtoto ninavyolipa eleweka wewe utaendelea hadi lini kulala na chakula halafu una njaa unaacha kula kisa hujui cha nani au unaogopa funguka mtoto wa kiume nipo hapa kwa ajili yako sema sasa (huku akipitisha mkono wake shingoni mwa Vatican), aaah Mary acha kwanza basi tufanye hivi hebu chukua hivi . Akampa maua kadi na ile choclate Mary alifurahi akajua labda Vatican kishanasa kwenye mtego wake kumbe wapi mawazo ya Vatican bado yapo kwa Martha tu kisha Vatican alimuaga Mary na kumpoteza zaidi si akamkumbatia basi Mary kichwa hilo kajua ndege mjanja yupo kwenye tundu bovu kumbe wapi. Vatican alifuatilia hadi akampata mtu aliyekua anasoma st marrys day aliyeitwa Angel. Angel alikua anasoma darasa moja na Martha , Vatican alimtuma Angel akamsalimie tu Martha , Martha alipopata habari hizo moyo ulilipuka ila naye alikua kaanza kumpenda Vatican hata ile hasira aliyekua nayo kwa Vatican ilitoka alipojua kuwa Vatican hakufanya chochote basi mind game ndio ilifanya kazi hivyo Martha alitokea kumpenda sana Vatican kisha alimpa majibu Angel na kumwambia Akamwambie Vatican aandike barua kwa kuwa shule hawakuruhusiwa kuwa na simu kweli Vatican aliandika barua na kumpa Angel na ilisomeka kama hivi " mambo natumaini we ni mzima wa afya pole na samahani kwa niliyokutendea najua nilikuudhi sana ila naomba nikwambie ukweli nilipolala na wewe sikufanya chochote wala sikulala na wewe usiku mzima bali nilikuja tu asubuhi naomba unisamehe kwa kukuchezea akili nakutakia masomo mema love you. Ndani ya barua yake Vatican aliweka chocolate kama ishara ya kumvutia Martha. Martha naye hakusita kujibu barua hiyo na kuandika hivi Kwako kipenzi Vatican najua kuwa nilikua na hasira kwako ila hilo ilikua ni sababu nilihisi umenitendea matendo mabaya ila haikua hivyo nimeamini kuwa we ni muaminifu na unanipenda kweli nachukua nafasi hii kukuambia kuwa nimekubali kuwa mpenzi wako kuanzia leo ila kwa masharti haya matatu kwanza sitopenda tukutane kimwili hadi nimalize kidato cha nne pili sipendi kuumizwa na nitajiua nikigundua una mpenzi mwingine hivyo nataka uwe wangu peke yangu tu hilo muhimu sana kisha sitopenda nifahamike sana kwa rafiki zako kuwa mi ni mpenzi wako naomba kwa sasa iwe siri ahsante kwa chocolate dedication massari real love i love you .

0 comments:

Post a Comment