SEHEMU YA 20
Dayness aliyekua anamfuatilia mume wake kuwa
wapi hua anakwenda ili ajue ni nani anayemuharibia mume wake hadi mapenzi yao
yanapungua alifika , alipofika tu hakuamini alichokiona machoni kwake Dayness
hakuweza kuizuia hasira yake na kumpalamia Irene kwa vibao na magumi Adam
alijitahidi kumzuia sana Dayness asimfikie wala kumuumiza Irene ila
alichoharibu zaidi ni pale Adam alipomshikilia Irene badala ya mke wake Dayness
hapo ndipo Dayness alipatwa na hasira zaidi na kuondoka katika maeneo hayo Adam
alimuomba Irene radhi na kumkimbilia Dayness. Dayness alikimbia kwa haraka kwenye gari lake na kuondoka Adam naye hakusita
kumfuatilia mke wake hadi nyumbani .Dayness aliendesha gari ovyo sana wakati
akienda nyumbani nusura amgonge mtoto wa shule kwa mwendo kasi aliokua nao ila
akamkwepa na yeye kwenda kugonga nguzo ya umeme iliyokua kandokando ya barabara
, kama uliwahi kusikia mapenzi yanaua na
ukajiuliza maswali mengi sana ni kivipi mapenzi yanaua basi hii ndio njia
mojawapo ya mapenzi yanavyoua. Mungu saidia Dayness akatoka mzima wa afya
haraka alikimbia na kulitelekeza gari lile na kupanda daladala alipofika
nyumbani kila kitu kilichokua mbele yake alikitupa na kuharibu haribu kisha
akaenda chumbani na kuweka nguo zake zote akiwa aliye dhamilia kuondoa ila
akiwa anaendelea Adam akafika , Mke wangu mke wangu Dayness sikiliza basi mke
wangu eeeh nisikilize basi usije ukajutia baadae maamuzi unayoyafanya na
kumuumiza mtoto wetu Martha hebu nisikie basi , Dayness aligeuka huku akilia na
amsikilize Adam anasema nini na Adam akaendelea , ulichokiona mama Martha sio
unavyofikilia huyo ni Irene mwalimu wa Martha wa kitangiri pia ni mpenzi wake
Humphrey yule rafiki yangu kipenzi sasa hapo alikua ananielezea kuhusu ugomvi
wao na Humprey sasa nikawa nampa pole ndio wewe ukaja hebu fikiri ni miaka
ishirini na kadhaa tupo pamoja sasa sijawahi kukudanganya wala kukuumiza iweje
leo unifikilie vibaya au hatuaminiani mke wangu siku hizi , Dayness huku
akifuta machozi alikua kama aliyeridhika na jibu la mume wake na kwa upole
akajibu, basi sawa mi nilijua labda ndio umeniacha sababu siku hizi sikuelewi
kabisa haki yangu ya ndoa hunipi salamu imekua tabu au tuna ugomvi, hapana
hapana mke wangu ni matatizo madogo madogo yalinipata kazini ndio maana nilikua
hivyo , sasa mimi si ni mke wako unashindwa nini kuniambia matatizo yako
tukasaidiana, eeeeeeeh basi basi mke wangu usihofu hayo matatizo madogo sema
sasa au twende sa hivi eeeh mke wangu , mmmh kukwambia tu tayari ulishataka, si
umeomba mwenyewe , we naye huzeeki , aaah wapi ng'ombe hazeeki maini wewe sema
kama upo tayari , haya basi sawa njoo. Ugomvi huo ulisha hivyo na Adam
akafanikiwa kuiokoa ndoa yake kwa muda kisha kesho yake alimwelezea rafiki yake
Humphrey yaliyomkuta kisha Humphrey aliwaalika Adam na Dayness kwenye chakula
cha jioni huku yeye akiwa amemualika Irene wote walikutana kwenye meza moja na
kusalimiana kwa pamoja kabla hawajaendelea Adam alichukua nafasi hiyo
kumtambulisha Dayness kwa Irene kwamba ndio mke wake na Dayness hakusita
kumuomba msamaha Irene kwa kitendo alichomfanyia.
0 comments:
Post a Comment