SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
SEHEMU YA 16
ahsante kwa chocolate dedication massari real
love i love you . Hayo ndiyo ya moyoni ya Martha aliyoyatoa kwa Vatican.
Vatican alipoipokea tu barua kutoka kwa Angel na kuisoma nusu alie alipiga
makelele hayo kama mwanafunzi wa form four aliyepata matokeo kuwa kafaulu
wakati asilia 80 wamefeli utani tu ila ki ukweli Vatican alikua mwenye furaha
sana pia furaha hiyo iliongezeka zaidi pale Vatican alipofaulu kwenda mwaka wa
tatu kwa ufaulu mkubwa wa GPA ya nne na hakusita kumshirikisha mama yake katika
furaha yake ilikua kama kuokota dhahabu mchangani huku wengine wanahangaika
kuchimba migodini . Shikamoo mama , marahaba hali yako ,nzuri , za masomo ,
nazo nzuri , vipi unataka shilingi ngapi sababu nishazoea ukinipigia tu wewe
unaomba hela , haaaa mama sio hivyo leo nitabadilisha ratiba kidogo nina jambo
jema nataka kukwambia mama yangu nimefaulu kwenda mwaka wa tatu tena kwa GPA
kubwa mi ndio nimeongoza chuo kizima ,haya hongera zako , halafu pia kuna
suprise nataka nikupe mama yangu , ipi hiyo ,ni siri utaona baadae , haya,
halafu mama , mmh nini tena , nina shida ya kiasi kadhaa cha fedha , nilijua tu
wewe uache kuomba hela mtoto wewe kama ulizaliwa benki vile haya shilingi ngapi
, kama laki tatu hivi , haya kesho, haya mama siku njema ,nawe pia masomo mema
baba, haya kwaheri ,haya. Kwa mtoto wa mwalimu mkuu ilikua sio kazi kupewa laki
tatu ni kama kuomba maji mtoni yani ilikua rahisi kweli kweli . Masomo
yaliendelea na Martha alikua kidato cha nne wakati fulani akafunga shule na
likizo hakwenda Mwanza kwani ilikua likizo ya muda mfupi kama wiki moja tu hapo
alipata nafasi rasmi sasa ya kukutana na Vatican tena aisee Martha maharage ya
shule yalimkubali alikua kanona ile mbaya alinenepa kwa kiasi kama ni ngombe
basi hata wasingengojea sikukuu tayari angekua ameshachinjwa umbo lake mithili
ya namba nane na alivyonawiri mweupeee Vatican alikosa cha kuongea ila cha
kushangaza zaidi walipoonana hakuna aliyemsemesha mwenzake hapa ilitumika lugha
ya matendo yani walicheka kila mmoja akitabasamu na kucheka kumvutia mwenzie
ilikua kama sumaku vile huo mvutano yani ghafla kila mmoja alijikuta kwenye
ndimi ya mwenzake wakaanza kubadilishana bacteria mwaaa mwaaa ndio sauti
zilizosikika. Kubadilishana mate tu watu kidogo wajigonge
wengine nao hadi wakaacha shughuli zao wakishangaa watu wanang'atana midomo
bila kuumia Vatican hapo kakamatilia kiuno taratibu anashusha shusha mkono hadi
kwenye makalio hahahahahaha ndivyo mambo ya vijana yalivyo ila sasa hili
lilikua fumanizi ni Mary alitoka nje na kukuta Vatican na Martha wakifanya yao aisee ilimuuma sana na Mary hua
akopeshi hapo hapo aliwafuata na kuanza kuongea mhhh haya wapendanao sasa
mtauza sana sura mwaka huu sijui nawe umempendea nini gunia kama hili (huku
akimwekea kidole usoni Martha) Martha kidogo atake kupigana ila Vatican
akamzuia hawakuishia hapo kula raha bali walirudi tena JB Belmont kukumbushia
raha za siku ile ya zamani huko kama kawaida yao hawakuacha kunywa na kula vya
kutosha ila sasa Vatican alidhamiria kuvunja amri ya sita siku hiyo kwani
alikazana sana kumshika shika Martha mapaja mara kumbusu sana kama aliyehitaji
Mambo fulani hivi kutoka kwa Martha kwa kuwa ilikua ni the promise ilibidi
Vatican awe mpole na kusubiri hadi siku ya ahadi itakapofika siku hiyo Martha
alikua makini sana hakunywa pombe wala hakutaka kukaa sana kwenye starehe siku
hiyo hivyo alirudi mapemaa nyumbani kisha wakaagana na kuachana kila mmoja
alilala kwa furaha huku akimfikiria mwenzake ilikua ni kama ndoto na siku hiyo
hakuna aliyelala kwa raha walizoponda siku hiyo kama mwenye njaa kutupwa katika
msitu wa matunda. Likizo iliisha na Martha akarudi shule siku nazo hazigandi
kama maziwa mtindi kujenga historia zaidi ya mwanamalundi sasa Martha alimaliza
kidato cha nne sio yeye tu pia na Vatican naye alimaliza mwaka wa tatu chuo
hivyo kama muda wa kutimiza ule usemi wa ahadi ni deni ulitakiwa utimizwe yani
ni kuwasumbua wachawi kwa sauti za kuwafanya wasiloge usiku na kuwasikiliza
nyie hahahahaha najua ulishatambua kama una nia ya kujua ni zile mechi muhimu
zenye matokeo matatu tu kushinda kushindwa au kutoa sare tena zipo za uwanja wa
nyumbani na zile za ugenini ila kubwa zaidi ni zile za kimataifa hapo uwanja wa
taifa kuna heshima yake hapo we acha yani unalichezea taifa lako , tuachane na
mbwembwe hizo tuje kwenye mahafali iliyofana sana ilikua ni mahafali ya Martha
kumaliza kidato cha nne aisee haya mahafali yalikua ya kifahali watu walikula
hadi wakawa wanaitwa warudie tena , mzee Adam alikuepo mama Martha Dayness na
Mary kuchukua taarifa za umbea .Martha alipewa laptop kama zawadi kutoka kwa
baba na saa ya dhahabu kutoka kwa mama , Vatican naye hakusita kupita japo kwa
mbali japo alione ua la moyo wake kheri subuhana na radhi zake upendo huu uishe
kwake aisee yani mvutano zaidi ya marhamu tamu inavyonukia huku Martha akinuia
japo amuone hata kwa mbali Vatican naye alisubiri apate majibu ya asali asije
umia kwa uchungu wa shubiri wakakutana wawili kama hadithi vile kidogo mambo yafanyike yakumtafuta mrithi ila aaah Vatican
akajisemea sizitaki mbichi hizi " ishara ya upendo kuonyesha uvumilivu na
skendo hatoi maulana uzuri wako bado msichana nakupenda tena nakupenda sana
pindi uniachapo mi nitakazana niombe radhi kwako usije nihama atakayesema
chokochoko ruhusa kumtukana" haka ni ka nyimbo ka msanii Joseph ambako Vatican alikua
anakaimba huku kabeba maua yake mawili
kama ishara ya upendo na Martha kifuani mwake waliachiana na Martha akamuaga
kwa busu hatari sijapata ona hadi watu walisikia kisha akarudi haraka kwa
wazazi wake sherehe ikafana na ikawa kama historia mzee Adam hakutaka aaache
kitu Martha alikua anaondoka naye kurudi nyumbani Mwanza huko atasubiri matokeo
Martha alibisha kwanza kidogo baadae ikabidi akubaliane na baba yake na kurudi
Mwanza Vatican naye hua ashindwi kitu si akarudi pia nyumbani kwao Mwanza sa
hapo bila bila mzee Adam na Vatican . Milima haikutani ila binadamu hukutana,
kwenye hoteli moja maarufu Mwanza ambayo wafanyakazi , mabosi na watu maarufu
hukutana hapo kupata chai na chakula cha mchana hapo ndipo Irene kwa miaka
zaidi ya mitano hivi anamwona tena Adam ila Adam ni baada ya miaka 25 anakutana
tena na Irene aisee ilikua siku ya kazi jumatano Irene amekwenda kupata
kifungua kinywa kama kawaida yake katika hoteli ile ila Adam yeye siku hiyo
alipelekwa hapo na rafiki yake wa karibu sana na meneja masoko Humprey katika
kampuni aliyokua anafanya kazi Adam ,lengo la Humprey ilikua ni kumkutanisha
Adam na rafiki yake wa karibu wa Humprey ambaye katika tetesi Humprey
alimwambia Adam kuwa angependa amuoe ila alikua bado akisubiri majibu kutoka
kwa mama huyo. Kweli walitangulia wao kufika na kuagiza kile walichotaka Adam
kwa shauku si akaanza , Humprey huyo mrembo mbona hafiki au umepigwa changa la
macho hahahahaha na wazee unajua hua hatutaniani sasa kama ulitaniwa au leo
siku ya wajinga nini ?, Aaaa Adam sipendi utani bwana haraka haraka haina
baraka subiri atakuja uje umuone we mwenyewe utamkubali mama wa watu
alivyoumbika. Kama unakumbuka zamani Adam naye alikua mtu wa wanawake hivyo
sifa tu alizoambiwa na Humprey ye mwenyewe mate yakaanza anza , haikuchukua
muda akafika
Friday, October 09, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment