Tuesday, October 13, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 22

Siri hufichuliwa na mjasiri woga ukikithiri
Sehemu ya 22

basi Dayness alikwenda na wazo la kuiokoa ndoa yake aliwaza aende kukutana na Irene na kuongea naye kwani alihisi kuwa Irene alikua chanzo cha mume wake kuwa hivyo . Kweli Dayness alifika nyumbani kwa Irene na alikaribishwa na Vatican , hakujua kwamba Vatican alikua mpenzi wa mtoto wake Martha kweli Dayness alikaribishwa ndani na kumkuta Irene , Vatican aliwapisha waongee , Dayness akaanza ,dada huyo ni kijana wako , ndio kijana wangu wa kwanza anaitwa Vatican kamaliza chuo mwaka huu bado yupo nyumbani hajapata kazi si unajua ajira kwa vijana siku hizi ngumu , kweli kabisa dada , aisee samahani dada nimeshasahau utatumia kinywaji gani , hapana samahani wala usihofu nipo sawa kabisa, usione aibu hapa ni nyumbani , hamna tabu sema tu kuna jambo nataka kukuuliza dada , upo huru sema tu dada , nilikua nasema hivi naomba uwe mkweli dada sababu hili swala ni kubwa sana na na linahitaji ukweli kwa kweli mume wangu siku hizi amechanganyikiwa kabisa tokea Humphrey atangaze kukuoa mume wangu Adam kabadilika sana kitabia yani kama taarifa za ndoa yako zilimuwehusha kabisa na mi kwa muda mrefu nilihisi mabadiliko kutoka kwa mume wangu hakunipenda kama alivyonipenda zamani haki ya ndoa ilikosekana hata na salamu pia baya zaidi ni pale alipojiunga na unywaji wa pombe ndio akawa anarudi saa nane yani ndoa yangu iliteteleka sana sana dada nimeumia sana hadi sasa hivi kazi kaacha dada kama unahusika kwa lolote tafadhali naomba umuachie mume wangu niachie mume wangu nampenda sana dada tafadhali Dayness aliongea hayo huku machozi yakimbubujika katika paji lake jeupe la uso kama mtu angeweza kukinga kikombe basi machozi yale yalikua mengi yangeweza kujaza jagi kabisa kisha baada ya kukaa muda mfupi akiwa kimya Irene alimjibu, dada  pole na samahani sana kwa hilo ki ukweli mimi naomba nikueleze hivi huyo kijana unayemuona hapo ni mtoto halali wa Adam anaitwa Vatican mimi na Adam tulikua wapenzi tulipokua watoto kijijini tulipozaliwa Igombe kisha tukiwa bado tunasoma Adam alinipa ujauzito na kisha akaniacha na kukimbilia mjini mimi huko kijijini shule niliacha wazazi wangu na jamii ilinitenga nikaishi peke yangu na tumbo langu ( huku akilia)kwa kweli dada niliteseka nan niliumia sijapata kuona hadi pale alipotokea msamaria mwema mzee Shaban aliyeahidi kunioa na kurudisha heshima yangu hapo ndipo nilianza mwanzo mpya wa maisha yenye furaha mimi na mwanangu kisha nilijiapia sitomtafuta wala kumwambia chochote Adam kuhusu taarifa zangu na mtoto na yeye tangu akimbilie mjini hakuwahi kurudi mimi nilipohamia mjini baada ya mume wangu kufariki na kuniachia urithi ulioniwezesha kuanza maisha mapya huku mjini na ndio hadi sasa nipo hapa mara ya kwanza nakutana na Adam alinishangaa na kisha kadri siku zilivyozidi kwenda aliniomba msamaha na kunitamkia kuwa alikua bado ananipenda ila mi nilimkatalia na kumwambia kuwa anaweza kuwa rafiki tu basi kwa ufupi ndio hivyo ,dada kumbe Adam ana mtoto mkubwa hivi na hakuwahi kuniambia , pole sana dada hayo yalikua ya zamani , ila madhara yake yanaonekana sasa hivi dada kumbe mimi ndio niliharibu mapenzi yenu kwa kuingilia kati , hapana dada hapana , usifiche ni ukweli mtupu isingekua mimi kuolewa na Adam angekua tayari ameshakutafuta na mngerudiana , hapana dada achana na mawazo hayo we jaribu kumjenga mume wako kisaikolojia anisahau mimi , sasa nitafanyeje, mimi nitakusaidia kwa kuhama mji huu ili mume wako asiwe ananiona , basi dada ni hayo tu mi naomba niondoke , jamani karibu tunapika , ahsante kwaheri, haya kwaheri. Dayness alipofika nyumbani akili yake ilimtuma kuwa yeye ndio alikua chanzo cha yote hayo yani isingekua yeye Adam na Irene wangekua hawana matatizo wala mapenzi yake yeye na Adam yasingekuepo na asingeumia hivyo alijilaumu sana na kisha akachukua maamuzi magumu , chumbani alipokuwapo alimuita Martha na kumuhusia mambo yote kuhusu mapenzi na mahusiano kwamba hata siku moja asijaribu kuchukua mpenzi wa mtu mapenzi yanaua kisha alimtuma Martha Juisi ya matunda na Martha alipoleta Dayness alimkumbatia Martha kwa nguvu yapata dakika nzima huku akitokwa machozi Martha aliuliza kama kuna tatizo na mama yake alisema hapana kisha Dayness alimtuma Martha sokoni amfuatie matunda Martha alipotoka tu ndani na kuondoka Dayness alichukua sumu ya unga ya panya na kuchanganya na juisi aliyokua nayo kisha akainywa haikuchukua muda kufanya kazi Dayness aligaagaa huku na kule akihangaika chini kwa muda kisha akatoa povu jeupe mdomoni na kukata roho maskini Dayness alijiua

0 comments:

Post a Comment