Thursday, October 15, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 24

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
SEHEMU YA 24

Martha mi sitakufanya chochote ila naomba uniambie ukweli wote , iiiiii huku akilia Martha alisema Baba naomba unisamehe sana kweli mi nina ujauzito wa miezi miwili , vipi baba wa mtoto unamjua , ndio namjua baba, sasa naomba tufanye hivi naomba umwite baba wa mtoto tuje tuonane naye ili tumuulize kama atakubali kuwa mtoto wake maana vijana wa siku hizi tabia zao kukataa ujauzito, haya baba nitamtafuta na kumwambia. Kweli Martha alimpigia simu Vatican na kumwambia haloo , halo mpenzi Martha mambo , poa za kwako , ni nzuri tu vipi tena mpenzi wangu unataka tutoke out kesho au, hapana sio hivyo , sasa ni vipi , Vatican naomba unisikilize kwa makini sana hiki ninachotaka kukwambia , kipi tena Martha mbona unataka kunishitua au umefaulu mtihani wa form four , hapana sio hivyo bali hiki ni kitu muhimu sana kwa kweli nilishindwa kukwambia ila naona ni muda muafaka kusema ukweli tu , ukweli upi tena mbona unazidi kunichanganya sana mpenzi wangu , sio nakuchanganya ukweli ni kwamba mimi nina ujauzito tena wa miezi miwili, aaaaah wa kwangu au , ndio wa kwako , weweeeeeee weweeeeeee natamani hata ningekua karibu hapo nikakukumbatie balaa aisee Martha ahsante ahsante sana sana sana siamini kama naenda kuwa baba ahsante , we mbona umeshangilia hivyo , nimefurahi sana mpenzi wangu kuniletea mtoto , we unaona raha eeh je mimi ninavyoumia , aaah basi pole pole mpenzi wangu najua ujauzito unaumiza ila jikaze nipo pamoja nawe, ahsante halafu kuna kitu nataka kukwambia tena lipi tena hilo mimba imetoka au , bora hata lingekua hilo , bora , ndio hivyo bora sababu hili ndio baya yani baba anahitaji kukuona , nini , hujasikia baba anataka kukuona , baba yako Martha acha utani wewe , utani ndio ukweli wenyewe , sasa nakwendaje na lini , hahahaha ulishaogopa kukutana na baba mkwe ndio utakoma sijui utaongea nini , duu hayo hayo nitakayoongea , hahahahahaha hapo kiroho kimeshakudunda , mmh kweli , sasa kesho uje nyumbani najua hupajui hivyo nitakuelekeza ufike sawa , sawa. Basi Vatican hakusita kuonyesha furaha yake kwa kumwambia ukweli mama yake ila kama unavyojua wakinamama hua hawakubali hivi hivi Irene alikasirika kidogo kisha kwa kuwa mtoto mwenyewe mmoja hakuwa na cha kupingana naye lakini aliamua kumwambia mwanae Vatican waende wote ili naye akamuone mkwe wake na wazazi wenzake kweli siku ilipofika Vatican na mama yake walielekezwa na Martha na kufika kwao Martha.Hodi humu hodi mpaka ndani karibu karibuni sana ndivyo Vatican na Mama yake walivyokaribishwa na Martha huku ndani mzee Adam alikua kapumzika chumbani kwake kisha kauli ya Martha ndio ilimshitusha Vatican , jamani karibuni sana waaao mwalimu Irene siamini kama ni wewe shikamoo , marahaba eehee za wapi tena siku hizi , za hapa hapa mwanza mi ndio nimemaliza kidato cha nne mwaka jana na sasa nipo nyumbani nasubiri majibu , Irene huku akimkejeli Martha na kumshika tumboni akasema majibu yenyewe ndio haya ya kutanguliza tumbo mbele , eeeh ndio hayo au , aaah hili tumbo ni majibu ya huyo kijana uliyekuja nae vipi mnafahamiana, kufahamiana! huyu mtoto wangu wa kuzaa tufahamiane vipi tena , kumbe mwanao sikujua kama mwalimu Irene mwanao ndio atakuja kuwa na mimi , ndio utegemee sasa , basi tuachane na hayo karibuni sana sijui mtapendelea kinywaji kipi kuna maji ,soda, soda kubwa au maziwa, chochote mimi natumia kasoro hiyo soda kubwa labda huyo baba mtoto wako ndio umuulize , aaaah huyu najua , Vatican akadakia , nakunywa nini , siri yangu we subiri haya ngoja niwaletee nikamwamshe na baba alikua kapumzika kidogo ndani si unajua leo weekend haendi kazini hivyo nipo naye nyumbani tu . Martha aliondoka na kuwafuatia vinywaji huku Irene na Vatican wakawa wanaongea we huyu binti umempata wapi , aaah mama tulikutana naye Dar , anhaaa ndio uliyokwenda kusoma Dar hayo ya kuwapa mimba watoto wa watu , aaaah mama nawe mambo gani tena hayo mimi si nilienda chuo kabisa , sasa si ndio mliyofundishwa haya kumbe ndio maana mtoto shida zilikua haziishi mara oooh mama nataka laki tatu ya dom mara kuna mchango wa mlango mara aisee kumbe huyu ndio alikua amekuteka akili na kwa taarifa yako huyu unakaa naye kwako mwenyewe na mimba unalea mwenyewe sio kwangu mi sitoi misaada , mama mbona umefika mbali hivyo nimeshakwambia ni bahati mbaya tu hiyo wala hata yeye alikua hajui kama ana ujauzito hadi alipoenda hospitali sasa kama we unanitenga sa hivi mi nifanyeje basi acha mi niondoe usumbufu kwa kujiua tu sasa sina jinsi mi nitamleaje huyo hata kwangu tu sina, aaaa basi basi mwanangu nawe hutaniwi usihofu mi nipo nawe pamoja ngoja tuwasubiri tuone wataamua nini eehehee tena hawa hapo wanakuja. Ni Martha alileta vinywaji na mzee Adam alifika na kuketi ,Vatican alimsalimia kwa uoga sana ila alishangazwa na mapokeo ya mama yake kwa mzee Adam ghafla Irene alishituka badala ya kumpa salamu Adam alimshangaa kisha akamuita mara tatu Adam , Adam , Adam , naye akaitikia naaam , huyu ni binti yako , ndio ni binti yangu mtoto pekee aliyeachwa na marehemu mke wangu Dayness Mungu ailaze pema roho yake , Irene aliongea kwa sauti kubwa na ya mshangao Mungu wangu , Adam akajibu nini ? Tumekwisha tumekwisha tumekwisha Adam , tumekwisha , kuhusu nini Irene mbona sikuelewi , Adam haya yote uliyataka wewe usingenitelekeza peke yangu na ujauzito wako kijijini ona sasa umewaoanisha kaka na dada bila kujua laana laana hizo Adam huyu hapa (huku akimshika Vatican) ni mwanangu Vatican ambaye pia ni mwanao ulienitelekeza nikiwa na mimba yake kijijini nimemlea mwenyewe hadi akakua hamjui baba yake kisha wewe unanichanganya kwa kuniambia eti Martha ni mtoto wako kumaanisha na Vatican ni mwanao pia hivyo Martha ni dada yake na Vatican mbona kasheshe hili jamani. Aliposema hayo kila mtu Martha na Vatican wakaanza kulia huku wakiwa na wazazi wao wakiwangangania wawathibitishie kuwa hilo jambo lilikua si la ukweli bali ni mbinu za kuwatenganisha, alianza Martha akimtikisa baba na kusema baba baba tell me what she is saying is not true please niambie baba kama mmepanga njama ya kututenganisha please baba please niambie Adam hakusema kitu chochote kwa mwanae Martha bali kimya ndio kilitawala. Vatican naye akamuuliza mama yake , mama huyu ndio baba yangu uliyekua unaniambia au , ndio mwenyewe baba yako kabisa mzazi mzee Adam kwani we kipindi unakutana na mpenzi wako sorry dada yako hukutaka kujua kwao wala wazazi wake nyie vijana wa siku hizi bwana mkikutana tu huko mnakokutania mkatongozana basi ndio imetoka hutaki hata kujua kwao na wazazi wake , aaah mama sio hivyo hata kama ningewajua wazazi wake ningejuaje kama baba yake ni baba yangu kama hukuniambia , basi ndio hivyo imeshatokea na huyu ni dada yako, mama mimi siamini kabisa Vaticani alitoka na kwenda nje huko akaanza kujisemea Yani siamini kama Martha dada na ndio namkosa hivi hivi na hiyo mimba huyo mtoto ataniita nani
baba au mjomba haya maneno alijiuliza Vatican nje ya nyumbani kwao Martha huku machozi yakimtiririka huko ndani napo kila mtu kimya kilitawala Martha ndio kabisa alishindwa kuvumilia na kwenda kujifungia chumbani. Huko chumbani Martha alichukua shuka lake la kujifunika na kulifunga kwenye feni iliyokua juu ya chumba chake kisha akajifunga shingoni na taratibu akajinyonga hadi kufa mzee Adam alipoona kimya alikwenda kwenye chumba cha Martha na alipofungua mlango akakuta umefungwa Adam aliuvunja na kuingia kisha hakuamini alichokiona Martha akiwa amenin'ginia kwenye feni kwa juu kajinyonga kwa shuka Adam alipiga kelele za kilio cha uchungu hadi Irene na Vatican wakakimbia kwenda huko mama yangu Vatican alipo uona mwili wa Martha akiwa amekufa alilia sana na kutoka nje Adam aliishiwa nguvu na kwa mshituko alidondoka chini na kupoteza maisha Vatican na mama yake Irene walibaki peke yao wakiwa na majonzi ya kupoteza wapendwa wao bila kujua hatima yao ya maisha.

KWELI SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
KIJANA POPOTE ULIPO PINDI UNAPOMPA MIMBA BINTI YOYOTE HATA KAMA UNAHISI SIO YA KWAKO TAFADHALI USIIKATAE WALA KUMTELEKEZA MAMA MJAMZITO NA KUANZA MAISHA YAKO BINAFSI BALI MJALI NA KUBALI KILA KITU KWANI HUWEZI KUJUA UKIFANYA HIVYO BAADAE MATATIZO KAMA HAYA YA KWENYE TAMTHILIA HII YANAWEZA KUKUPATA NA CHUNGA SANA KWANI SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.

0 comments:

Post a Comment