SEHEMU YA 19
wewe kama mtu mzima ulishajua nini kilichoendelea hahahahaha jiongeze mkubwa hayo ndio
yaliyoendelea huko. Vatican naye nyumba yake ilianza kuteteleka sijui ni sababu
ya Irene baada ya kumuona yani mapenzi yake kwa Dayness yalianza kupungua muda
mwingine hata kusalimiana ilikua tabu na haki ya ndoa ilipungua na kukosekana
kabisa siku nyingine ilikua sio kama zamani alivyokua na mapenzi kwa mke wake
maskini Dayness alihisi kuachwa kabisa ila kama kawaida ya wanawake hua
hawaachi kufuatilia chanzo ni nini siku moja akamfuatilia mume wake anakwenda
wapi siku moja Adam alimuomba Irene wakutane kuna kitu anataka kumwambia kweli
kwa kuwa Adam alikua mzazi mwenzie Irene hakukataa kuonana naye na alijua ni
kitu cha kawaida sana basi muda ulipofika kweli walikutana pale pale kwenye
hoteli yao walipokua wanakutania Irene alikuja kwa muda muafaka waliopangiana
wakutane kila mtu akaagiza huduma yake aliyoiitaji na kuanza maongezi Adam
hakusita kuanza na salamu , za saizi , salama, habari za kazi , mmmmh ni nzuri,
pole na kazi , ahsante , naomba radhi kwa kukupotezea muda wako , hapana wala
haina shida kabisa kumbuka nilikuhakikishia kuwa utakua rafiki yangu hivyo
sioni tabu au shida kuongea nawe, aaa basi sawa ila naomba hili jambo
ninalotaka kukwambia ulichukulie umuhimu sana na unijibu ipasavyo , jambo lipi,
kiukweli mimi nilikua napenda uniambie kama mwanangu ulijifungua au alikufa
niwe na uhakika kabisa , Irene alikaa kimya kwa muda kisha akaguna kama
aliyekua anavuta pumzi kusema kitu huku Adam akiwa amemkazia macho kujua Irene
angesema nini na Irene akaanza kusema kwa sauti ya chini na kumwambia
uliponiacha kijijini na ujauzito sio tu familia yangu kila mtu alinitenga na
nikaishi mwenyewe sikuwa na wakunisaidia hivyo nilijifungua kwa shida na kwa
bahati mbaya mtoto alifariki, pole sana , Irene alidiliki kudanganya huku
akilia Adam kwa mapenzi mema alinyanyuka na kumsogelea Irene na kumkumbatia
kama kumnyamazisha alipokua analia wakati Irene alifahamu kuwa anadanganya ila
alijifanya mwenye majonzi huku akijiliza liza , Adam alimkumbatia Irene na
kumbe Dayness aliyekua anamfuatilia mume wake kuwa wapi hua anakwenda ili ajue
ni nani anayemuharibia mume wake hadi mapenzi yao yanapungua alifika ,
alipofika tu hakuamini alichokiona machoni kwake
0 comments:
Post a Comment