SIRI HUFICHULIWA NA
MJASIRI WOGA UKIKITHIRI.
SEHEMU YA 10
MTUNZI: JOSEPH SAMWEL.
MAWASILIANO:
0764217244.
EMAIL: josephsamwel484@gmail.comBaaadae Adam aliporudi hospitali kutoka nyumbani alipokwenda ghafla alikuta tayari Vatican alishatoka na hayupo mazingira yale basi akaona kama ndio kaepushiwa kesi naa kuondoka. Wala haikuchukua muda Vatican kupata nafuu na kurudi shule, Miaka hua haichelewi bwana Martha tayari alikua kakua na kaanza darasa la kwanza katika shule ya msingi kitangiri ambayo mwalimu wake mkuu alikua ni Irene daaaaah hapo sasa. Vatican pia alishinda la saba na sasa ailkua kidato cha kwanza pamba sekondari . Masomo ni mazuri kwa Vatican na kwa Martha pia wakati Dayness alipokuja kumuijia Martha shule ghafla akajikuta kajigonga kikumbo na Irene
Dayness: ooooooooh pole dada samahani sana
Irene: bila samahani dada pole kwako wewe vipi hujaumia
Dayness: hapana nipo salama kabisa wala usihofu
Irene : haya sawa sawa karibu sana shuleni kuna chochote ungependa nikusaidie
Dayness: kwani we ni mhusika hapa
Irene: naitwa mwalimu Irene ni mwalimu mkuu wa shule hii
Dayness: mi naitwa Dayness Haule ni mzazi nina mtoto wangu hapa yupo la kwanza anaitwa Martha tena huyo hapo ( huku akimkumbatia)
Irene : jamani kumbe ndio huyu mtoto mzuri sana inaonekana na baba yake atakua mzuri sana sababu mtoto ajafanana sana nawe hivyo atakua kafanana na baba yake.
Dayness: kweli kabisa mwalimu bab yake ukimuona ni mtu mmoja mstaarabu
Irene: kweli nami naona basi nakutakia siku njema na kwaher
Dayness: kwaheli mwalimu (huku akiondoka na mwanae) baasi maisha ndivyo yalivyosonga hivyo pole pole kila mtu akifanya mambo yake siku moja akiwa shuleni Irene alishangaa kumwona Martha peke yake huku wanafunzi wengine wakiwa tayari wamekwisha kuondoka ni mama yake alichelewa kumuijia kama mkuu wa shule Irene alichukua jukumu la kwenda naye Martha nyumbani kwake kwa usalama zaidi ila aliacha taarifa kwa mlinzi wa shule kuwa endapo Dayness angekuja ampe namba yake ya simu wawasiliane. mama Martha hakuwa na simu hivyo namba ile alimpa mume wake Adam aipige na aongee na mwalimu mkuu. Griiiiiiiiiiiiiim griiiiiiiiiiiiim ring ring ianita ngoja tusubiri apokee Adam alimwambia mke wake mara halooo Haloo naitwa Mr Mack A (Adam alijitambulisha kwa jina lake la ofisini ) ni baba wa Martha samahani naongea na mwalimu mkuu wa kitangiri , hee ndio mimi mtoto mlichelewa kumuijia nikaenda naye nyumbani nipo naye hapa yupo salama kabisa mnaweza kumuijia , basi ahsante sana nitakuja mimi kumchukua nielekeze kwako ni wapi , aaaah ni kirumba polisi ukifika nijulishe nije sawa ,sawa
0 comments:
Post a Comment