Tuesday, October 13, 2015

SIRI HUFICHILIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 23

Siri hufichuliwa na mjasiri woga ikikithiri
sehemu 23

Dayness alichukua sumu ya unga ya panya na kuchanganya na juisi aliyokua nayo kisha akainywa haikuchukua muda kufanya kazi Dayness aligaagaa huku na kule akihangaika chini kwa muda kisha akatoa povu jeupe mdomoni na kukata roho maskini Dayness alijiua. Ilikua huzuni majonzi na vilio kwa familia ya Mzee Adam ndugu jamaa na marafiki wa karibu taratibu zote za mazishi zilifuatwa Dayness alizikwa . Irene alipata taarifa za msiba ila hakuhudhuria kwani alijua kuwa maneno na ukweli aliomwambia Dayness ndio ulimfanya ajiue kwa kujiona kuwa yeye Irene alikua ni chanzo cha kifo Dayness hivyo ilibidi Irene aseme ukweli wote kuhusiana na maisha yake na alianza na mwanae Vatican na alimwambia hivi , mwanangu kuna kitu nataka kukwambia na naomba ukishike sana kwa kuwa ni muhimu sana na unisamehe pale nitakapokuumiza hisia zako , mama ni nini tena hicho naomba uniambie , ni kuhusu maisha yako na ukweli kuhusu baba yako ukweli ni kwamba Marehemu mzee Shaban alale pema alikua mtu mwema na alikupenda sana ila hakuwa baba yako mzazi , sasa mama mbona unanichanganya baba yangu mzazi ni nani , huko ndipo ninapoelekea mnamo miaka 25 iliyopita baba yako mzazi alinitelekeza na ujauzito wako kisha akakimbilia mjini mimi nilitengwa na jamii nzima pamoja na wazazi wangu ila mzee Shabani pekee ndio aliniona na kunisaidia kwa kunioa na kuwa mke wake wa tatu hapo ndipo maisha yangu yalinyooka na kumsahau kabisa baba yako ila yupo na tupo naye hapa Mwanza anaitwa mzee Adam ni muhasibu wa TBL ila sasa ana matatizo kidogo akiwa sawa nitakupeleka ukamuone samahani sana mwanangu kwa kukuficha ukweli , hapana mama pole kwa yaliyokukuta sikuyajua ila ukipata muda utanipeleka nikamuone, haya sawa baba. Huku kwa mzee Adam mazishi yaliisha na kifo cha Dayness kilikua kama mwanzo mpya katika maisha ya Adam kwani Adam sasa alimpenda mwanae alirudi kazini na alijirekebisha tabia kwa kuacha pombe alijua kama mke wake angekuwepo angependa mume wake awe na tabia nzuri za hivyo sasa ulikua ni upweke katika familia nzima ya Mzee Adam ila kwa kuwa waliungana wawili yeye na mwanae waliishi kwa amani upendo . Kisha Irene alichukua hatua kubwa zaidi ya kwenda kumwambia Humphrey ukweli wote kuhusu maisha yake na mahusiano yake ya zamani na Adam huu ulikua ni ujasiri wa hali ya juu hapo alikutana na Humphrey na kuanza kumwambia hivi , habari yako Humphrey , nzuri tu mpenzi wangu habari ya kwako (huku akiweka mkono begani kwa Irene) Irene aliutoa mkono na kisha kumwambia Humphrey , nina kitu muhimu sana nahitaji kukuambia , kipi tena hicho au unataka tuoane sa hivi, hapana sio hivyo ila ni kitu muhimu sana katika maisha yangu mimi kabla ya kuwa nawe niliwahi kuwa na mpenzi na nilizaa naye mtoto mmoja ambaye ninaye kama hufahamu hilo na baba wa mtoto huyo nininini ni rafiki yako kipenzi Adam ndio alikua mpenzi wangu wa zamani na hadi sasa alikua bado ananipenda ila mi nilimkatalia na kukukubalia wewe ilikua ni sababu ili nimuumize tu Adam na kulipiza kisasi ila ki ukweli naomba msamaha kwa kuwa mimi sikukupenda kwa dhati , Irene siamini kama unanitenda hivi kweli yani mi niliamini nimepata mke wa kumuoa kumbe aisee kwa hiyo ndio tumeachana au yani Irene ukiniacha unanikumbusha maumivu ya marehemu mke wangu , Humphrey mimi kuwa na wewe haiwezekani kwa kweli yani ni kama kulazimisha pikipiki kuwa gari naomba samahani sana , Irene alimuacha Humphrey na kuondoka zake dah Humphrey aliumia sana ila ndio hivyo hakuwa na jinsi ya kufanya alijikaza kiume tu , huku kwa Martha zilitokea dalili ambazo zilimshitua sana alianza kutapika na kujisikia vibaya hivyo akaamua kwenda hospitali kujua nini kilimsumbua kiafya ndipo alipopata jibu lililomshitua sio tu kiakili bali ilikua ni mabadiliko ya kimwili " umia ujae " ndiyo kilichomtokea Martha alikua na ujauzito kama wa wiki zipatazo mbili hivi aaaaaah aliona hata aibu kumwambia ukweli baba yake na baba mtoto wake Vatican ilikua ni kipindi kigumu sana kwake ila bahati mbaya tumbo hua halifichiki ndipo mzee Adam akaanza kuona dalili kisha akaamua kumuuliza , Martha mama njoo maramoja kuna kitu nataka kukuuliza , shikamoo baba , marahaba habari yako , nzuri tu baba , ila mimi naona sio kama nzuri sana , kwa nini unasema hivyo baba , mama naona mabadiliko sana katika mwili wako wala sio unene huo hayo ni mabadiliko makubwa Martha mi sitakufanya chochote ila naomba uniambie ukweli wote

0 comments:

Post a Comment