SEHEMU YA 18
Irene alisita kidogo na alipoangalia watu wote
katika hoteli hiyo waliduwaa wakiwaangalia wao kwa kuepusha aibu Irene ilibidi
aeleweke tu na kusema haya nimekusamehe simama sasa , ahsante alijibu Adam
ambaye aliposimama hakusimamam hivi hivi bali alijifanya kajisahau na
kumkumbatia Irene ambaye naye kwa kuwa ni mbele ya watu aliweka mikono yake
mgongoni mwa Adam na kumkumbatia huku Adam kakamatilia kiuno daaah huyu jamaa
kweli ngombe hazeeki maini yani tabia zake zilikua zile zile kwa vijana wa sasa
wangemuita kicheche , kisha wakakaa tena kwenye meza yao na Adam akaanza maongezi yake tena kwa Irene na kumwambia , ahsante kwa
kunisamehe kisha naweza kujua mwanangu sa hivi yuko wapi na anaitwa nani , kwa
hilo siwezi kukwambia kwa sasa ila naomba please please usidhani eti kukusamehe
ndio mambo yako sawa hapana kwanza hapa una bahati sana na shukuru Mungu leo
sijui nimeamkia wapi tu haya mi naomba niende sasa
, aaah si nikupe lifti hadi kwako hata nipajue , hapana sitaki sitaki siku
nikitaka upajue utapajua kwa sasa nitakachoweza kukuhakikishia ni urafiki tu
mengine yote hapana, aaah masharti magumu hayo sawa mama nimekuelewa alisema
Adam nakuagana kila mmoja akaenda kwake , Kesho ya muda wa mchana Adam
alishangaa kumuona Irene katika viunga vya kampuni ya TBL mawazo yake yote
yalimtuma anakuja kumtafuta yeye kumbe Irene alikuja kumuumiza zaidi Adam
aliyefikiri kasamehewa hivi hivi tu kirahisi rahisi , Irene alikuja kumuona
Humphrey , Adam si akatoka anajiamini kwamba Irene anakuja kwake kwa mbwembwe
huku akitabasamu tabasamu kabla hajafika Irene alipokua Irene si akanyoosha
mikono kama mtu aliyekua akihitaji kumkumbatia mtu fulani Adam si akazani ni
yeye naye akanyoosha mikono kama anataka kumkumbatia Irene mara ghafla akatokea
mtu nyuma yake Adam na kwenda kukumbatiana na Irene alikua ni Humphrey daaah
Adam ilimuuma sana hii ilikua ni michezo ya kitoto ikichezwa na watu wazima
hahahahahaha hayo ndio mapenzi bwana hayakui yani michezo ya kitoto mtu mzima
anamfanyia mtu mzima mwenzake , huku napo sio pa kusahau kwani siku hii ndio
haswa ile siku mjenzi alikua anakabidhiwa vifaa vyake vya kazi aanze kazi
ilikua ni kazi ya kukimbiza mwenge yani namaanisha ilikua siku ya kuvunja ahadi
ya siku nyingi waliowekeana ni hawa vijana wa kizazi kipya Vatican na Martha
ndio hasa walikutana tena baada ya kutoonana kwa muda mrefu sasa nao waliona
ulikua ni muda bora wa kupinga amri za Mungu kwa kuvunja mojawapo ya amri zake
ambayo ilikua ni amri ya sita. Hawaanzagi hivi hivi bali ndani ya jiji la
miamba miamba la Mwanza vijana hawa wawili walikutana katika hoteli ya Golden
crest kupata maraha ya dunia yani duu yani daah Vatican kishamchomoa mama yake
kama laki mbili hivi za kutumia siku hiyo mtoto mwenyewe mmoja huyo chochote
atakacholilia anapewa haikua shida kupewa laki mbili na mama haya tuendelee,
baada ya vinywaji na chakula hotelini hapo sasa ulikua ni muda wa kupumzika .
Katika chumba walichokua Martha alienda kwanza kuoga humo humo bafuni na
Vatican kwa haraka haraka zake alikua tayari ameshajiaandaa yani kabaki na nguo
kama tatu mwilini mwake ambazo zilikua ni kaptula fupi na nguo ya ndani kisha
na kaushi wakati akiwa anasubiria kwa hamu kumwaga marhamu harufu marashi ya
utamu sogea wote tule humu Vatican aliweka kwenye redio wimbo wa Whitney
Houston I will always love you Martha alitoka nao taratibu bafuni akiimba wimbo
huo bila ajizi akaumwaga mchuzi mbele ya walowezi ni kile ki taulo alichokua
amekivaa alikiachia kikaanguka hadi chini pwaaa mambo hadharani karibu mwandani tuonyeshane vya ndani mimba hiyo ajali kazini hebu
karibia tusafishe nyota kila siku niwe ninakuota ilikua ni katika chumba kimoja
kitanda kimoja watu wawili wakiwa na wazo moja na wakifanya tendo moja kwa
pamoja huku hawajui kama ni wa baba mmoja aisee hatutapoteza sana muda huko wewe
kama mtu mzima ulishajua nini kilichoendelea hahahahaha jiongeze mkubwa hayo ndio
yaliyoendelea huko
0 comments:
Post a Comment