Friday, October 09, 2015

SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI 17

                     SIRI HUFICHULIWA NA MJASIRI WOGA UKIKITHIRI
                                                 SEHEMU YA 17

haikuchukua muda akafika Irene mamamamama pwaaaa moyo wa Adam ulishituka alikua ni Irene yule yule mzuri vile vile kama zamani alipokua na miaka 17 mwenye sura ya kupendeza mwili ambao kama ulitengenezwa vile yani kama alikua bado binti kumbe mama wa miaka arobaini na kadhaa hivi Adam alibaki ameduwaa kama aliyeshangaa mwonekano mzuri wa Irene ghafla alishituliwa na sauti ya Humprey akimkaribisha Irene karibu mwalimu Irene , ahsante habari zenu, oooh salama salama Adam ,Adam unasalimiwa , Adam alishituliwa na Humprey kwani alikua bado ameduwaa huku akicheka hahaha salama tu mawazo haya, Humprey bila kuchelewesha muda akaanza utambulisho Adam huyu hapa anaitwa Mwalimu Irene ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi kitangiri , ooooh nashukuru kumfahamu huku akimpa Irene mkono , Irene naye akasita kidogo kisha akampa mkono Adam na Adam naye akatambulishwa kwa Irene , Irene huyu ni rafiki yangu kipenzi anaitwa Adam ni muhasibu mkuu wa TBL , oooh nashukuru kwa kumfahamu alisema Irene. Kisha Irene aliagiza chakula alichohitaji na kukaa Adam hakuacha kumtupia jicho Irene kwa chini chini mwishowe kama ka mchezo wakawa wanatupiana macho kwa kuibia mithili ya kutegeana yani huyu anamwangalia mwenzie kisha anapindisha macho na mwenzake pia anamuangalia mwishowe hadi Humprey akataka kuwashitukia na akauliza vp mnafahamiana au naona wote kwa pamoja wakaitikia aaaa hapana wala hatufahamiani , aaah sawa nilidhani mnafahamiana. Adam alianza kukumbuka zamani na kujiuliza kama Irene alikua mwalimu wa kitangiri basi ndio yule aliyewasiliana naye kitambo kipindi mwanae alipopotea shule pia akaanza kufungua simu yake na kutafuta namba ya Irene aliyoiifadhi miaka iliyopita kwenye simu yake Mungu saidia akaipata bwana hapo hapo akaanza uchokozi ulikua ni uchokozi wa kubip zaidi ya mara tatu akamudu kukatisha mazungumzo ya Irene na Humprey ila Irene kwa kukomesha akazima kabisa simu hapo akamkomesha kabisa kisha mazungumzo yao yakafana na kua vyema na sasa Humprey akapanga kutupa nanga za kiutu uzima na hapa akaanza pole pole ki hivi sasa mwalimu unalifikiriaje lile swala langu nililokugusia kipindi kirefu , jamani huniachi hata nifikirie kidogo jibu lako nitakupa tu , haya ngoja nisubiri, Adam kwa chini chini si akakaza macho kwa Irene hapo ndipo Irene alipochukua maamuzi magumu ni ya kusogea karibu na Humprey kisha akamwekea mkono juu ya mabega yake na kumwambia unajua nini Humprey unaonekana mwenye nia sana na mimi sasa naona wacha nikupe nafasi japo nijaribu nione kwa sababu nyinyi wanaume hua hamtabiriki mwanzoni mnaonyesha kama mna upendo kisha baadae mkipata mnachokihitaji hukimbia na kutuacha wapweke (Irene alimaanisha hivyo kama kumuumiza Adam kwa mafumbo) , aaah hayo mi siwezi kufanya mi bwana najua kutunza wanawake wala sitokuumiza na utu uzima wangu kweli huu nifanye mambo ya vijana hayo siwezi ,alisema Humprey , Huku Adam aliumia roho zaidi yale mapenzi ya zamani kwa Irene alikua bado anayo na aliumia kuona Irene anakwenda kwa Humphrey kiulaini kumbe Irene naye alifanya hivyo kumuumiza Adam asikie maumivu aliyoyapata yeye miaka kadhaa iliyopita na kweli Adam aliumia kabisa sema alijikaza kwa kuwa ilikua mbele ya rafiki yake. Kisha makutano hayo yaliisha na kila mmoja alimuaga mwenzake na kuondoka ilikua ni furaha kwa Humphrey na kilio kwa Adam na sasa Adam aliona acha ajaribu nafasi yake kwa kumpigia simu Irene , huku Irene akiwa na furaha kwamba kamkomesha Adam mara simu ikaita akapokea haloo nanana ( Adam alipata kigugumizi ) naongea na mwalimu Irene tafadhali , ndio mimi nikusaidie nini ,(Adam akakaza sauti kwa kukalipia) nimesema sitaki ujinga nataka unionyeshe mwanangu na unileze ni kwa nini miaka yote hiyo hupo hapa hukuwahi kunitafuta , wewe baba una wazimu kwanza naongea na nani we unapiga simu tu na kuanza kufoka unamfokea nani hebu kama umekosea namba bora ukate au useme we nani , (Adam kwa upole) aaaah samahani sana mi naitwa Mr Adam ni menejaaa, wala hata usimalizie ehe shida yako nini ? Una wazimu hivi ulidhani kuwa sitoishi uliponiacha na mimba yangu sasa umekosea njia mtoto wako hutamjua wala hana jina lako niache na maisha yangu niishi kwa raha kwanza nitamwambia rafiki yako kwamba unanisumbua , aaaaah basi basi yaishe Irene tukutane basi tuongee yaishe mi naomba msamaha najua nilikuumiza ila nina sababu zangu njoo tuongee nitakwambia ukweli wote , tafadhala tafadhali sana sitaki unipotezee muda wako na uongo wako wa tangu zamani , hapana naapa kweli sitatumia muda mwingi kukueleza naomba tafadhali , haya sawa wapi na saa ngapi, mmmh ni pale lenana hotel saa kumi jioni nadhani utakua umeshamaliza kazi zako, hayo hayakuhusu haya nitakuja, haya kwa he haloo haloo, kabla hajamaliza simu ilikua tayari ilishakata , kesho yake muda ulipofika kweli baada ya kazi Irene alikwenda Lenana Hotel pasiansi na kukutana na Adam, kwa mbwembwe kabla Irene hajakaa Adam akamvutia kiti na kumruhusu akae kisha akamuuliza Irene angetumia kinywaji gani na kuagiza, maongezi yakaanzishwa na Adam mwenyewe aisee siamini japo miaka imekwenda Irene we bado ni mzuri vile vile na mrembo wa kuvutia kwa kweli sichoki kukuangalia nikikumbuka zamani nilivyokupenda hadi moyo unaniuma , eeeeeh wewe baba sikuja kwa hayo hebu eleza shida zako haraka mi niondoke naona kama unanichelewesha , aaah samahani kwa hilo unajua tangu tuachane kijijini sijaacha kukufikilia wewe yani upendo wangu kwako bado upo ule ule , (Irene huku akitaka kunyanyuka) wewe hebu usiniletee mambo ya kizamani historia ambayo ilishafutika kichwani mwangu kama huna la kuniambia mimi naondoka , aaaa basi basi najua unanichukia sana kwa mambo niliyokutendea ila naomba samahani sana naomba msamaha kwa hilo Irene kuna sababu nyingi zilizonifanya kukuacha kijijini , kama zipi , nyingi tu, hazina majina au kumbe nia yako ilikua kunichezea na kukimbilia mjini , hapana hapana , ila , ila matatizo madogo tu , aaaah sawa hayo matatizo madogo ndio yananifanya na mimi nikuache sa hivi , usifanye hivyo usi , tayari Irene alinyanyuka na kutaka kuondoka Adam haraka alimdaka Irene miguu na kuing'ang'ania kwa kuikumbatia huku akiwa kapiga magoti na kichwa chake kipo usawa wa tumbo la Irene na akiwa kakiegemesha hapo akisema naomba msamaha nisamehe tafadhali Irene , mwili wa Irene ulisisimka na hisia zake zikamjia na kumrudisha mbali kumbuka ni miaka mingi hakuwahi kukutana na mwanaume yoyote kimwili sasa mkono wa Adam uliopita kiunoni mwake uliamsha hisia zake na kumkumbusha zamani sana kwa moyo wa hurumu Irene huku akiwa amemshika Adam kichwani akasema unaniaibisha bwana tafadhali simama simama , Adam akajibu siwezi kusimama hapa hadi uniambie kama umenisamehe au , Irene alisita kidogo na alipoangalia watu wote katika hoteli hiyo waliduwaa wakiwaangalia wao kwa kuepusha aibu Irene ilibidi aeleweke tu na kusema haya nimekusamehe simama sasa 

0 comments:

Post a Comment